Ukitaka maendeleo ni Kodi. Kwenye hili hakuna mbadala wake.

Bila kufanya hivi Hawa machinga ambao ndio wanamiliki uchumi siku hizi na Kodi hawalipi unategemea utawapata wapi
 
Yaani huduma za mobile money zilikuwa zimekaa poa sana hadi pale serekali imeamua kuharibu kila kitu kama kawaida. Tamaa, Mimi nadhani wabunge hawa wakatwe kodi maana wanaenjoy wakaati sisi maskini tunapigika. Inshort tunafanya kazi kwa nguvu kulish familia na viongozi wa serekali.
 
Kwa nini miamala ya bank hakuna tozo na ukaamua kung'ang'ana na miamala ya walala hoi watu wa chini kabisa ,je wenye akaunti banki sio watanzania ,onyesha hekima na siyo kiburi kwa kufuta hilo hata kama sheria imepitisha uliwauliza wananchi
 
Mwanasiasa yeyeto ambae mtoto wake wa primary analipa ada milioni 10 na apandi daladala Katu hawezi panga bajeti rafiki kulingana na maisha ya mtza
 
Mhe. Rais naye ameguswa na jambo hili, amesikia maoni ya Watanzania wote, ameshatoa maelekezo kwamba tuyafanyie kazi haya malalamiko ambayo wananchi wanayatoa." - Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba.....
Huyu rais hawezi toboa sababu hana msimamo.
 
Lazima usome chochote ambacho kinahusu kuweka sahihi
Yaani unaamini kabisa Rais wa nchi atakaa na kuanza kusoma mikataba, na miswada?! Atasoma mikataba na miswada mingapi?! Na nimekuuliza, wakati Rais anakaa kusoma mikataba na miswada, wakati huo Mwanasheria Mkuu wa Serikali anafanya kazi nini, na ameajiriwa kwa kazi ipi?
 
Naona tozo zimerudi kama kawa.
 
Jamani Mama atafanya mangapi? Musaidieni kuondoa kodi mzigo kwa wananchi sio mpaka watu waandamane.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…