Mwigulu: Tumesikia malalamiko ya Watanzania kuhusu tozo za miamala na Rais ametoa maelekezo ya kuzitazama upya
Mama ni msikivu sana. Mwigulu alipotosha baraza kwa hizi kodi za mshikamano
Tatizo ni aina ya Wabunge waliopo pale mjengoni,zaidi ya 80% hawakuchaguliwa na wapiga kura wameingizwa pale kwa mabavu ya vyombo vya dola kwa agenda moja tu ya kwenda kumuandalia mwendazake utawala wa kifalme,hivyo hawana deni kwa wapiga kura wao otherwise wangeipinga hii moja kwa moja. Ni hasara kwa Taifa letu kuwa na wabunge wengi toka CCM.
 
Mhe. Rais naye ameguswa na jambo hili, amesikia maoni ya Watanzania wote, ameshatoa maelekezo kwamba tuyafanyie kazi haya malalamiko ambayo wananchi wanayatoa." - Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba.

"Nitoe rai kwa wananchi kuwa Serikali imesikia malalamiko ya wananchi na tayari tumeendelea kuyafanyia kazi, Waziri Mkuu ameshaitisha kikao kesho kuendelea kupitia masuala haya haya."

"Kwa sababu hii ni sheria ya Bunge, na tayari imeshapitishwa na inatakiwa kutekelezwa, lakini kuna maeneo ambayo yanaangukia kwenye kanuni ambazo zinaangukia Wizara ya Fedha na Wizara ya Teknolojia ya Mawasiliano."

Mwigulu Muongo hakuna cha Mh Rais wala nini ,Miamala imeshuka kwa kiwango kikubwa sana na kuhofia kwamba hadi kodi waliyokuwa wanaipata itashuka......Tozo ni mihimu kwa maendeleo ila waliyoiweka ni kubwa sana ,hawaoni wenzao wa REA ukinunua umeme wa elfu 1 unakatwa Tsh 25 hata mtu haufeel..
 
Mheshimiwa waziri👇CCM kuchukua madaraka ya hii nchi ni tulipigwa pakubwa sana.
1452391_1479182254035.jpg
 
Hapo waziri wa fedha ameshaumbuka tayari,mwenyewe juzi alihojiwa Tbc akasema kitu kikishapitishwa na bunge hakuna awezaye kubadili...sasa iyo taarifa inavyokuja na kusema wanakaa kikao najiuliza je waziri wa fedha nae atakuwepo kikaoni
 
Eti Rais na waziri wake wote wasomi wa uchumi!!

Nafikiri ni uchumi wa maganda ya korosho

Huku mtaani nawapa tu taarifa mpesa zishaanza kufungwa.

Failed state!

Watu wengi hasa watanzania hawajui tofauti ya Economics and Finance. Uchumi sio finance, profesion ya Finance hajulikani vzr hivyo watu hupelekea kuwapa wizara ya fedha watu wa uchumi ambao hawana utaalamu kabisa kwenye mambo ya finance. Watu wa finance ndio walitakiwa zaidi kwenye wizara ya fedha maana finance zaidi ni katika mambo ya kutafuta mitaji, kuwekeza, kujua athari za vyanzo vya kodi etc etc. Uchumi kama uchumi ni too much nadharia. Ndio maana huyo Mwigulu hajui vzr anacho fanya hapo wizarani.
 
Mwigulu Muongo hakuna cha Mh Rais wala nini ,Miamala imeshuka kwa kiwango kikubwa sana na kuhofia kwamba hadi kodi waliyokuwa wanaipata itashuka......Tozo ni mihimu kwa maendeleo ila waliyoiweka ni kubwa sana ,hawaoni wenzao wa REA ukinunua umeme wa elfu 1 unakatwa Tsh 25 hata mtu haufeel..
Huu ndio ukweli!
 
Kuna muda wanafanya mambo kujaribu akili za Watanzania. Katika hili la miamala ni wazi wamechemka hata kama wananchi watafanya miamala siyo kwa kiwango kile ambacho kulikuwepo zamani.

Nchi yetu sote tuijenge bila kuumiza watu wa hali za chini, mawakala wa mitandao ya simu wanalia, watumiaji huduma wanalia, wananchi wanalia yaani taifa limegeuka uwanja wa kilio.

Hatuwezi kuwa taifa la hivyo, wananchi wako tayari kulipa kodi ila si kwa kukomoa hivi. Mnaweza kurudi na kufuma upya hiyo tozo mbona miamala inafanywa kwa wingi sana pesa mtapata hadi mtaridhika.

Serikali ipunguze kodi kwenye hii miamala na makato pia yapunguzwe kisha mtafurahi kwa jinsi ambavyo mamilioni ya miamala yatafanywa na watumiaji. Ila mkitaka kukomoa na sisi tutatafuta njia nafuu kwetu.
 
ukimsikiliza kwa makini Mwigulu, utagundua upstairs ni mweupe na muongo, na anadhani kila mtu yupo kama yeye. Nashangaa economist hawezi kuona madhara ya ushauri wa hovyo kama huo kwenye kodi za miamala. Mme-exhaust vyanzo vyote vya kodi mmekosa mnarudisha kodi za aibu!!!!!. Miongoni mwa vitu vinavyotanabaisha usomi wa watumishi wa wizara ya fedha, ni aina ya kodi wanazotoza. Ukikuta nchi inatoza kodi za hovyo tayari unajibu.
Mnasubiri huyo chotora wa Kariakoo awashauri upuuzi wake na nyie kwa usomi wenu mnachukua tu!!!
 
Mhe. Rais naye ameguswa na jambo hili, amesikia maoni ya Watanzania wote, ameshatoa maelekezo kwamba tuyafanyie kazi haya malalamiko ambayo wananchi wanayatoa." - Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba.

"Nitoe rai kwa wananchi kuwa Serikali imesikia malalamiko ya wananchi na tayari tumeendelea kuyafanyia kazi, Waziri Mkuu ameshaitisha kikao kesho kuendelea kupitia masuala haya haya."

"Kwa sababu hii ni sheria ya Bunge, na tayari imeshapitishwa na inatakiwa kutekelezwa, lakini kuna maeneo ambayo yanaangukia kwenye kanuni ambazo zinaangukia Wizara ya Fedha na Wizara ya Teknolojia ya Mawasiliano."
Rais na Waziri wake wote muflisi. Jambo hili au tozo hizi lilitakiwa kupimwa na Rais na Waziri wake kwanza iwapo ni jambo ambalo ni "practical" kwa Watanzania wa kawaida kabla halifikia utekelezaji.

Na hapa ndio unaweza kuona kuwa Bunge ni dhaifu kiasi gani. Kwa maneno mengine Bunge limebinafsishwa na kuwa kitengo cha serikali. Wananchi wamekosa watu wa kuwasemea Bungeni.
 
Mama ni msikivu sana. Mwigulu alipotosha baraza kwa hizi kodi za mshikamano

Tumsaidie Mama kuisafisha hii nchi. Inawezekana kuwa hahusiki na fyongo nyingi za hawa jamaa:

IMG_20210704_051559_619.jpg

NB: It's not done until it's done!
 
Huu ndio ukweli!

Yaani Lameck Madelu(Mwigulu) ndio Mchumi Daraja la kwanza halafu anafanya mambo bila kufanya utafiti wa kina , kitendo walichofanya kuongeza gharama(tozo) kimeshusha transactions kwa kiwango kikubwa sana na hata wakirudisha kama mwanzo bado ile effect yake itaendelea kwa muda!! Wenzetu kabla hawajaingiza kitu live huwa wanafanya tafiti za kina na pilots kwanza za kutosha.
 
Rais na Waziri wake wote muflisi. Jambo hili au tozo hizi lilitakiwa kupimwa na Rais na Waziri wake kwanza iwapo ni jambo ambalo ni "practical" kwa Watanzania wa kawaida kabla halifikia utekelezaji.

Na hapa ndio unaweza kuona kuwa Bunge ni dhaifu kiasi gani. Kwa maneno mengine Bunge limebinafsishwa na kuwa kitengo cha serikali. Wananchi wamekosa watu wa kuwasemea Bungeni.

Mwigulu nadhani anashindwa kuwaelewa watz ,sisi waTZ tunamaindi vitu vidogo sana ,tuko tayari kutembea kilomita moja kwenda kununua unga kilo 2 uliopunguzwa Tsh 100 na kuacha duka lililo mita 20 kutoka mlangoni mwake.
 
Hili jambo toka siku ya kwanza Zungu anatoa wazo lilikataliwa ila walionekana kulikumbatia kwa vile wao si waathirika wakubwa wa vikodi hivyo vidogovidogo. Tumekuwa na taifa linalotegemea mawazo ya watu 300 kuongoza watu milioni 59. 77!! Taifa gani hilo sasa.

Wananchi wanaelewa wapi pa kushika na wapi pa kutoshika ila nyie mliopo juu mmepigwa upofu na bado mkiambiwa mnavimba, tuna viongozi wenye maajabu sana.
 
Back
Top Bottom