Mwigulu: Tumesikia malalamiko ya Watanzania kuhusu tozo za miamala na Rais ametoa maelekezo ya kuzitazama upya
Hili jambo toka siku ya kwanza Zungu anatoa wazo lilikataliwa ila walionekana kulikumbatia kwa vile wao si waathirika wakubwa wa vikodi hivyo vidogovidogo. Tumekuwa na taifa linalotegemea mawazo ya watu 300 kuongoza watu milioni 59. 77!! Taifa gani hilo sasa.

Wananchi wanaelewa wapi pa kushika na wapi pa kutoshika ila nyie mliopo juu mmepigwa upofu na bado mkiambiwa mnavimba, tuna viongozi wenye maajabu sana.
Soma hii hapa

 
Mhe. Rais naye ameguswa na jambo hili, amesikia maoni ya Watanzania wote, ameshatoa maelekezo kwamba tuyafanyie kazi haya malalamiko ambayo wananchi wanayatoa." - Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba...
Sheria ya bunge kwani amri kumi za Mungu ishindwe kubadilika!.

Tumeshudia enzi za Nyerere, Bunge iliwahi kupitisha sheria yakupandisha bei ya unga wa sembe na bei yaunga ikapanda, wananchi walivokuja juu kwa kulalamika Nyerere akatoa amri bei ishuke! na ikashuka, basi Rais Samia hana budi kufanya kama alivofanya Baba wataifa, kuhusu kisirani hii ya tozo la muamala wa simu.
 
Mhe. Rais naye ameguswa na jambo hili, amesikia maoni ya Watanzania wote, ameshatoa maelekezo kwamba tuyafanyie kazi haya malalamiko ambayo wananchi wanayatoa." - Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba...
Kitu cha kwanza unachotakiwa kufanya Mwigulu ni kujiuzulu haraka
 
Tozo za kizalendo sijatumia mobile money almost a week
Nimejua kumbe inawezekana
Waziache tu hizo tozo maana walikuwa wanaona tunafaidi sana
 
Nimeshangazwa kuona maagizo ya Rais kwa Waziri wa Fedha eti waangalie upya suala la Tozo za simu.

Hivi Rais alikuwa hajui ataenda kuingiza Tsh ngapi mpaka sasa ndo anakuja kukurupuka kama hajui lolote hivi.

Yaani Wizara inaandaa bajeti, bajeti inaenda bungeni inajadiliwa, inapita alafu sasa anatoka Burundi huko anakuja kusema angalieni upya.

Futa kabisa maana huko tunalipa VAT.
 
Nilisema haijawahi kutokea waziri wa Fedha kutokea mkoa wa singida tangu nchi ipate uhuru. Sasa yameonekana. Jiuzulu babu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Huyo ni waziri tu!

Fikiria yule mbelgiji alitaka awe rais!
 
Bado swali langu ni imekuwaje alisaini huo muswada?

Hiyo si muhimu mjomba. "Mbagusiro" wakiendelea kuveshwa yao sisi inatuhusu nini?

IMG_20210719_113908_861.jpg


Strategy nzuri ya vita - watenganishe na usiwanyime njia ya kutokea!

Cc: Babati
 
Kitu cha kwanza unachotakiwa kufanya Mwigulu ni kujiuzulu haraka
Nilisema hapa kuwa hawa wanatuchezea akili

 
Amesain sheria tarehe 30 june leo anatoa maelekezo na hapo aliteua mpaka mshauri wake wa uchumi

20210719_112848.jpg
 
Sisi tunaamini utafiti na pilots zinapoteza muda na kutuchelewesha.
Mambo yatajipa tu.

Amandla....

Acha tu mambo ya kwenye biashara inahitajika watu wabobezi kutoa ushauri wa kitaalamu maana effect yake huwa ni kubwa sana kama mtu akikurupuka ,kile walichokuwa wanakitarajia hawatokipata na kile walichokuwa wanakipata kitashuka.

Nakumbuka mwanzoni mwa 2000 kulikuja open shoes flani hivi kama anavyotengeneza Kanye west ,vilikuwa vinauzwa kama sikosei elfu 30 hivi na walikuwa wanavaa mastar/wasanii wa bongo fleva na mablazameni.

Sasa kuna tangazo la Juice ya yebo yebo walilitoa na moja ya mtu aliyekuwa anafanya hilo tangazo alivaa hivyo viatu ,hauwezi amini vile viatu vilishuka bei kutoka elfu 30 hadi elfu 2 na vikadharaulika sana na kupachikwa jina hadi leo vinaitwa "YEBO YEBO" lakini YEBO ilikuwa ni JUICE.
 
Mhe. Rais naye ameguswa na jambo hili, amesikia maoni ya Watanzania wote, ameshatoa maelekezo kwamba tuyafanyie kazi haya malalamiko ambayo wananchi wanayatoa." - Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba...
Sheria siyo hoja,

Rudini bungeni haraka mkarekebishe hiyo sheria, hatuwezi kuendelea kuwaumiza wananchi kisa sheria ambayo mna uwezo wa kuibadili
Magufuli alisitisha matumizi ya KIKOTOWO licha ya kuwa alishasaini kuwa sheria!
 
Back
Top Bottom