Mwigulu: Tumesikia malalamiko ya Watanzania kuhusu tozo za miamala na Rais ametoa maelekezo ya kuzitazama upya
CCM ni janga la taifa, yaani wana create tatizo alafu wanatupa matumaini ya kulitatua….
 
Pia wabunge waanze kukatwa kodi kama watu wengine serikali itakusanya zaidi ya bilion 70 kwa mwaka, huu ndiyo uzalendo wanaohubiri siyo tukatwe sisi wao wasikatwe kwenye posho na mishahara yao.

Hata sisi bado kuna kodi kwenye miamala ya mpesa nakadhalika kama hao unaowasema ulaya na marekani. Hiyo PayPal kutuma pesa na kupokea kama ni kirafiki na kindugu ni bure tu, isipokuwa kibiashara ndo wanakata 3% ya amount. Kawaongopeeni wajinga
 
Acha tu mambo ya kwenye biashara inahitajika watu wabobezi kutoa ushauri wa kitaalamu maana effect yake huwa ni kubwa sana kama mtu akikurupuka ,kile walichokuwa wanakitarajia hawatokipata na kile walichokuwa wanakipata kitashuka...
[emoji28][emoji28][emoji28],nimekumbuka yeboyebo!
 
Mambo mengine wawe wanafanya tathmini wenyewe kabla hawajasababisha usumbufu huku kwa wananchi
 
Na hasara walioiingizia makampuni ya simu kwa siku sita hizi nazo watazilipa? Ni wazi biashara imeshuka na makampuni yamepata hasara tangu utekelezaji wa hiyo sheria ulipoanza rasmi.

Mtu mmoja na kigenge cha watu 300 wanayatia makampuni hasara na kuikosesha serikali mapato stahiki na bado mtu huyo anaendelea kukalia ofisi ya umma. Very shameful!

Huu ni uchumi na fedha sio majaribio, ukifanya error moja tu kwa siku moja umesababisha hasara ya pesa nyingi, kuna siku hii nchi itakosa mwekezaji hata mmoja, ikiwa watu wa aina hii wataendelea kushika wizara nyeti kama hizi.
 
Haiwezi kuwa sheria bila Rais kusaini sasa wakt anasaini hakuona au hakusoma hii ni mara ya 4 anapingana na kile alichokisaini kuanzia kuteua then kutengua ndani ya masaa 24,swala la mabando,then miamala ya simu sijui kitafata nini tunaweza jikuta siku moja tupo vitani kwa watu kufanya vitu then baadae kuvibadili sasa sijui mkiingia vitani mtakuja kubadili nini tu?
Yaani,mkuu inashangaza sana,eti Mama kasikia kilio,Kwahio wakati anasaini alikuwa anasaini kitu gani?au ndio kutafuta kiki?
 
Chonde chonde sheria mliipitisha wenyewe, msitafute njia za kuvunja sheria za nchi, ni takwa la kikatiba kuheshimu sheria tulizoziweka wenyewe !
 
Hakuna ni NCHI DUNIANI iliweza kuongeza uchumi (economy) wake kwa kuongeza au kupandisha KODI (TAX) huwo ndio ukweli .

Serikali iwe wazi tu kwa WANANCHI wake iwaeleze ukweli tu ndio jambo la msingi wache ngojora ngojera Sio tu kila siku wakiulizwa Kuhusu DENI la TAIFA wanasema DENI letu ni DENI imilivu.

Hivi WA-TANZANIA hamjui ya kwamba hii maradi yote inayo jengwa ni Mikopo tena mikopo mengine ni ya RIBA kubwa hasa na baado haija kamilika na inahitaji hela zaidi .

Sasa kinacho fanyika ni kuonyesha ya kwamba serikali inauwezo wa kukusanya mapata yake kwenye source mbalimbali ili iweze kuendelea kupata hiyo mikopo kwenye hizo EVIL INSTITUTIONS huku ikilipa MBILLIONS of shillings kila mwezi kwa ajili ya kuserve tu interest rate every month.

Na hii ni Rasha Rasha tu baado kilio kitakuja zaidi ya hapa kwasababu hakuna wanacho jua zaidi ya kuongeza kodi ....DENI LA TAIFA NI Sh 60.9 Trillion sio lelemama .
 
Nilisema haijawahi kutokea waziri wa Fedha kutokea mkoa wa singida tangu nchi ipate uhuru. Sasa yameonekana. Jiuzulu babu
Hii ya waziri kutoka Singida au Mtwara au Mara haina uhusiano wowote na kinachoendelea pamoja na matatizo yake....
 
Kabla ya sheria kupita, lazima maoni ya wananchi yachukuliwe, walikurupuka nini au kulikuwa na haraka gani? Eti mama msikivu, ina maana akili yake ndogo haikumwambia hii kitu haikuwa sahihi?

Wasifiaji endeleeni kusifia, kwangu mimi ni ujinga mtupu unaendelea!
 
Back
Top Bottom