Mzee Makamba: Watu wazuri huwa hawafi ndio sababu Kinana yupo na Jakaya yupo!

Mzee Makamba: Watu wazuri huwa hawafi ndio sababu Kinana yupo na Jakaya yupo!

Hakuna kitu muhimu kama katiba na tume ya uchaguzi, lakini kwa hawa mafisadi hivyo ndio vitu vya mwisho na ovyo kwao kuliko chochote, tunahitaji nchi inayojielewa na kulinda haki kwa kila mtu na uchaguzi ulio huru, hayomambo ya umeme na maji ni muhimu na rahisi zaidi kuliko kutawaliwa na hawa wakoloni weusi, huyu mzee anazingua sana
 
Mkuu kama Magufuli angekuwa kweli kama hivyo mnavyomuelezea kwamba alikuwa anauwa watu hovyo basi angekuwa keshawamaliza hawa watu maana aliwajua toka yupo hai asingewaacha walikuwa wabaya wake, labda tuseme aliona noma au kuna namna iliyomfanya ashindwe kuwauwa kama alivyokuwa anauwa hovyo hao wengine.
Ben Saanane aliuawa kwa jambo la kijinga kabisa. Lissu alitaka kuuawa kwa jambo la kijinga kabisa. Magufuli alitumia nguvu kubwa kabisa za dola na fedha kujaribu kuua upinzani. Hakujua kuwa maadui zake halisi walikuwa ndani ya CCM wakimwimbia mapambio. Wale vijana waliokamtwa wa kusheherekea kifo chake walikuwa kama kafara tu. Walioshehekea na kufanya tafrija za siri nadhani mnaanza kuwaona wanajitokeza mmoja mmoja. Mna cha kujifunza!
 
Kwahiyo mkapa na magufuli waliokufa walikua wabaya? Anazeeka vibaya huyo mzee
Kwa nini unasema anazeeka vibaya? Hivi hata alipokuwa kijana aliwahi kuwa tofauti? Mbona huyu baba maisha yake yote ameishi kwa unafiki na kujipendekeza? Hawa ndiyo wamefanya mpaka sasa miaka 60 ya Uhuru Dar maji yanatushinda. Ukiwa na vibwengo kama hivi nchi inaliwa na wachache tu.
 
Kagame yuko hai, museveni yuko hai, Nyerere hatunae tena, Karume hayupo, wala uhai sio kitu cha kutolea mfano wowote, watoto wao kua na vyeo wasipofushwe macho mambo hubadilika saa na muda wowote
Amelamba asali hadi inampalia huyu Mzee!
 
Back
Top Bottom