Jamaa_Mbishi
JF-Expert Member
- Jun 15, 2013
- 10,181
- 7,382
Wachache wanaohujumu nchi yetu ni wale wanaotaka kutisha watu na kuwanyamazisha kwavile tu wanaongea wale wasiyopeenda kuyasikia!!!
Wachache wanaohujumu nchi yetu ni wale wanaotisha wamiliki wa vyombo vya habari kwavile tu magazeti yao hayakuandika drama zao!!!
Wachache wanaohujumu nchi yetu ni wale wanaotumia askari wetu wakiwa na silaha za kivita na kwenda kuvamia vituo vya habari kulazimisha urushwaji wa habari za kipumbavu!!!
Wachache wanaohujumu nchi yetu ni wale wanaowaambia wauza mihadarati kwamba wewe na wewe mnauza mihadarati kwahiyo kesho kutwa nendeni polisi kuripoti wakati wanajua kabisa ukifanya hivyo unawapa fursa ya kupoteza ushahidi!!!
Hao, na wengine sawa na hao ndio wahujumu wakubwa wa nchi hii including wewe mwenyewe unayeona suala la kushambuliwa Nape halituhusu na bila shaka unaona hata suala la kuvamia Clouds nalo halikuhusu kwa sababu wewe ni kwakilishi wa hao wahujumu!!!!
Clouds hata ichomwe moto ni sawa tu, wale ni wauza unga....nani asiyejuwa hivyo? Mwacheni rais wetu kipenzi asafishe nchi. Tunataka Tanzania yenye heshima si ya kilele mama.