Lord Denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 23,491
- 57,973
Wewe unataka Watanzania kushiriki au Wauaji kupata stahiki zao?Swali kwako na kwa wengine wengi tulioweka matumaini yetu yote huko ICC.
Hawa waliofungua kesi "Intelwatch Madrid Bar Association na Human Rights Institute", wana uhusiano gani na Tanzania?
Sihoji wao kuhusika kwenye kesi hiyo; lakini natamani sana kama kuna waTanzania ndani ya taasisi hizo ndio wawe mstari wa mbele kwenye shughuli hii muhimu inayowahusu waTanzania wenyewe..
Kuna waTanzania walioshiriki kufungua kesi kupitia huko ICC na sasa wamejumuishwa kwenye hizi taasisi?
Sifurahii hata kidogo sisi kufanyiwa kazi kana kwamba ni watu tusiojiweza kabisa.
Ni lazima tuwe na ushiriki katika jambo muhimu kama hili linalotuhusu wenyewe.
Siwezi kushangilia hata kidogo kama hakuna ushiriki wetu wa moja kwa moja.