Ndoto ya wengi ni Kazi, nyumba, Familia, mwisho Gari

Bado nyumba na gari, ila nataka nianze na gari😃😃,.. Nyumba nitaishi nyumbani labda wanifukuze
Wahindi ni Matajiri wakubwa lakini wanaishi nyumba za kupanga na Wana Magari mazuri sana na Maisha mazuri sana wengine wanakaa Kwa wazazi Wao Wala hamna shida .Waswahili ndio tuna shida .Waaarabu na wapemba Matajiri sana lakini unakuta watoto wao wanaishi na wazazi Wala hakuna shida na hakuna anayelalamika

Cha msingi uchangiaji bajeti hapo nyumbani
 
Kwahio una maana wengi wana ndoto ya kupata BASIC NEEDS? Tuna safari ndefu sana.
Maisha ni basic needs tu bila kujali.kipato kidogo au kikubwa.
Ila basic needs zinatofautiana quality .Mfano basic needs ni chakula ,mavazi na malazi .Struggle zote zinajikita hapo tu sio nje ya hapo .Mtu ana struggle kuwa chakula atakachokula kiwe Cha quality ipi ya chini au juu,Mavazi atakayovaa yawe ya quality ipi ya chini au ya juu na malazi na makazi yake yawe ya quality ipi ya chini au ya juu kwake binafsi na familia yake
Kila kitu kinazungika hapo tu asilimia kubwa .Kwenye quality ya basic needs kuanzia mhusika na familia yake na ukoo wake
 
nakubaliana na ww mkuu maana vikwazo vipi vingi wachache sana wamejitoa
Utaanzaje kuwaza kuwa na Kiwanda ikiwa umezaliwa nyumba ya kupanga mpaka unakuwa ni kulala kwenye makochi huku wenzio wanazaliwa baba mkubwa anamiliki Kiwanda cha nondo na mabomba, baba ni contractor mkubwa anaekula tender za serekali kila mwaka. Baba mdogo ana kampuni ya Transport and Logistics malori ni kibao yanaenda Transit Congo, Mengine Zambia. Mjomba ni Waziri wa viwanda na uchukuzi. Hapo kuwa maskini ni kupenda wewe tu.
 
mkuuu umepangilia hadi nimeogopa 😂😂😂😂
 
Wenye talent wanapaa fasta.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…