Uchaguzi 2020 NEC yamuita Tundu Lissu kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya Taifa

Sisi wananchi tunataka kampeni za kistaarabu za wagombea kunadi sera tuwasilikilize tufanye maamuzi Sasa Kama wagombea watakuja majukwaani na matusi na lugha za kashfa tutawapimaje?

Tume mmepewa mamlaka ya kusimamia uchaguzi nchi hii Kama mgombea yoyote kafanya kosa la kiaadili achukuliwe hatua bila kujali ukubwa wake walal ukubwa wa chama chake. Tume simamieni sheria
 
Lisu ni debe tupu!

Ukiona mtu anakutaja sana ujue umemzidi.

Lakini pia mwacheni Lisu aropoke atakavyo maana ni sehemu ya tiba kwa yaliyomkuta.

Lisu ni debu tupu.
Nani kakudanganya? Kama ni debe tupu mbona mmeacha kunadi ilani yenu mmebaki kusubiri atasema nini ili mujibu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaha mnamuombea poo?!

Anamshambulia mgombea mwenzake, sasa ataanzaje kuishambulia serikali?!

Serikali ni sote watanzania we vipi?!

Umeoa wapi mchezaji anakabana namashabiki na kuacha kukaba wachezaji wa team pinzani?!
Pia timu ikifanya vibaya anaeshambuliwa na kufurumushwa ni kocha, kwanini serikali iwe ya Magufuli, flaiova za Magufuli, Tanzania ya Magufuli, barabara za Magufuli alafu huyo Magufuli mwenye mali zake akishambuliwa wanalia lia?
Watulie kama walivokua wakitulia Magufuli alipokua anashangiliwa na kusifiwa.

Sent from my TECNO K9 using JamiiForums mobile app
 
Sipo hapa kumuuliza Mkapaau Bashiru,ninakuuliza wewe uliekuja na hoja ya time huru hapa.
Ikiwa wewe mwenyewe hauwezi kusimamaia hoja unazozianzisha mpaka nimtafute mkapa(RIP) au Bashiru, nataka nikushauri uache mkumbo wa kubeba hoja sehemu bila kuelewa misingi yake ni nini.
 
Sifa zilizokuwa zinamwagika mfululizo kwa jenzi za mabarabara si kwa serikali ya chama cha mapinduzi bali zilienda kwa Rais magufuli vumilieni na lawama ziende kwake pia
 
Pamoja na kusifu jibu ulilopewa, ambalo ni sahihi kabisa, bado unakomaza shingo tu?
Ina maana hukuelewa jibu au unazi umekuzidi kimo kiasi huwezi kuona kitu chochote kilicho tofauti na yaliyomo akilini mwako?
 
Ngoja nikusaidie kidogo, pamoja na kuona uwezo wako wa fikra ulivyo chini sana. Tume inaweza kuundwa kwa njia mbalimbali na bila ya kutegemea manazi wa chama kimoja pekee.
Kama bado huelewi hiki, wewe huwezi kuelewa chochote.
Uwezo wangu wa kufikiri utaonekana ni mdogo kutona na udogo wa ubongo wa mtu anaetaka kujibu hoja zangu.Subiri hoja za hoyehoye userereke nazo.
 
Sipo hapa kumuuliza Mkapaau Bashiru,ninakuuliza wewe uliekuja na hoja ya time huru hapa...
Wapi nilikuambia ukamuulize Mkapa na Bashiru? soma nini nimeandika bila jaziba . usipindishe hoja please
 
CCM mmeanza lini siasa za kuheshimiana hasa huyu mgombea wenu asie na breki mdomoni...
Kuliko kujifariji ni afadhari mkaendelea na maisha yenu tu kutafutia watoto wenu unafuu wa maisha,ni bora zaidi kuwa huna chama kuliko kushabikia upinzani huu wa kipuuzi tu
 

Suala la kuwa na mahaba na chama fulani sio dhambi,shida ni kuonesha hayo mahaba hadharani!Swali lilipaswa kuwa watumishi wa tume wanapata wapi ujasiri wa kuonesha mahaba yao au kupendelea bila woga?

Na hapa ndio linakuja suala la msimamizi wa sheria ndio huyo ambaye amewateua viongozi wa tume!Hivyo hawana woga wa kuwajibishwa kwa maana wanampendelea huyo mwenye mamlaka!

Majibu ya haya yote ni katiba mpya itakayopunguza mamlaka ya Rais na kuzipa taasis nguvu zaidi kutekeleza majukumu yao kwa uhuru!
Kwanini marekani wameweza?

Sisi hatujashindwa ila kwasababu mfumo unawabeba watawala basi wanaukumbatia!
 
Hatimaye kamati ya maadili Nec yamuita mgombea Uras kupitia chama Cha demokrasia na maendeleo "chadema" kwa ajili ya mahojiano zaidi.
 
Pamoja na kusifu jibu ulilopewa, ambalo ni sahihi kabisa, bado unakomaza shingo tu?
Ina maana hukuelewa jibu au unazi umekuzidi kimo kiasi huwezi kuona kitu chochote kilicho tofauti na yaliyomo akilini mwako?
Hutapata mtu asifungamana na chama chochote,zaidi ya kufanya balancing kama ilivyo sasa.Tatizo lenu mmeshajijengea mawazo kuwa kila anaeteuliwa na Rais Basi lazima ataunga juhudi πŸ˜‚, na ndio maana kelele za tume huru kwenu hazitaisha.
 
Inatosha kushughulika na mtu kama wewe.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ huna hoja.
Nimekuelewa πŸ™πŸ™
 
Malalamiko ya Tundu Lisu anapaswa kuyaelekeza ama kwa serikali au kwa bunge linaloisimamia serikali lakini siyo kwa Dr Magufuli kama mgombea...
Ila yeye MagufuLi akisema β€œmtu kashiba ugali anakuja kusema ndege hazina faida kwani alikuja kutoka nje kwa bajaji?” Hii siyo persanal?
 


Tume ya Jaji Fransic Nyalali iliyoundwa mwaka 1991 ilipendekeza mfumo wa vyama vingi na tume huru ya uchaguzi.

Aidha Tume ya Jaji Ropbert Kisanga iliyoundwa mwaka 1999 ilisema hatua ya wajumbe wa tume kuteuliwa na rais ambaye anaweza kuwa kiongozi wa chama kinachotawala katika utendaji wao ama watakuwa na upendeleo kwa chama husika ama watalipa fadhila kwa aliyewateua.

Mapendekezo mengine ni yale ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya Jaji Joseph Warioba ambayo iliona umuhimu wa kubadili muundo wa tume ya uchaguzi na kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi.

Katika kitabu chake cha My Life, My Purpose, Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa, anashauri kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi ili kuimarisha demokrasia barani Afrika.

Anasema muundo wa tume umekuwa ukilalamikiwa kutokana na upatikanaji wa viongozi wake hivyo, kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi itakayokubalika na vyama vyote vya siasa ndiyo chachu ya kulea na kukuza demokrasia nchini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…