Uchaguzi 2020 NEC yamuita Tundu Lissu kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya Taifa

Uchaguzi 2020 NEC yamuita Tundu Lissu kufika mbele ya Kamati ya Maadili ya Taifa

Malalamiko ya Tundu Lisu anapaswa kuyaelekeza ama kwa serikali au kwa bunge linaloisimamia serikali lakini siyo kwa Dr Magufuli kama mgombea...
Kayataka mwenyewe.. AMekiteka chama na kuanza kuita serikali ya CCM kama Serikali ya Magufuli... Acha Lissu amnyooshe vizuri.. Tutaheshimiana
 
Je, ni nani anagombea Kiti cha urais? Ni serikali , bunge au ni Magufuli?? Tundu Lissu shikiria hapo hapo
 
Lissu anakosoa sera sio mtu, anakosoa miundo ya taasisi ndio maana anasema atalifumua jeshi la polisi, Chadema itakuja na sera ya majimbo, ataimarisha uchumi wa kanda zote bila ubaguzi kama anaofanya Magufuli, kusema hivyo ni kumshambulia mtu.
Anaposema Magufuli kampa tenda fulani.

Wewe inakuingia akilini kweli?
 
Enough is Enough lazima Lissu ajue kwamba hii ni nchi sio mbuga ya fisi. Haiwezekani mtu kila akisimama ni matusi tu. Mambo ya kipumbavu sana, unagombea halafu unaitukana Tume? Kwanini anagombea kama hana imani na Tume?Lazima atiwe adabu.
 
Hakuna anayetafuta 'Tume' toka kwa malaika. Jaribu kutumia akili kidogo alizokujaliya Mwenyezi Mungu.
Hakuna aliedai tume utafutwe kutoka kwa malaika, na ndio maana hata hawa waliopo sio malaika.
 
Nimekukubalia hilo wazo ni zuri, lakini tupate wapi watu wasiofungamana na upande wowote wa kisiasa🤔? Kwa mfano wewe ukiwekwa kwenye tume Ni lazima tu utakuwa upande wa CHADEMA, hata Kama ungechaguliwa na Magufuli,ambae yeye Ni CCM.
Kuwa upande fulani ndani ya nafsi yako ni jambo moja,ila kupendelea upande mmoja ni jambo lingine!

Watu wa Tume ambao ni makada wa CCM wanafanya upendeleo wa wazi kwasababu wanajua wanalindwa na seeikali ya CCM hivyo hawawezi kuchukuliwa hatua za kisheria!Mfano ni hao waliokatwa na wakurugenzi lakini wakashinda rufaa,kungekuwa na kuwajibishwa sidhani kama wangekatwa kinyemela!

Tuseme ndii wamgekuwa wamewakata wagombea wa CCM bila sababu za msingi,unadhani wangeachwa hivi hivi?

Mfumo wa uongozi katika nchi yetu ni mbovu sana,hata Nyerere alisema katiba imempa mamlaka makubwa sana!Kiasi kwamba akipatikana rais akaitumia vibaya basi watanzania tumekwisha!Hii maana yake ni kwamba haki inabaki kuwa utashi wa Rais!Akiamua kufukia mashimo basi hata ulaghai na udhulumati hugeuzwa haki na hakuna wa kuchukua hatua!
 
Salaam wana jamvi,leo ni Siku ambayo mgombea urais WA chama cha demokrasia na maendeleo anatakiwa kufika mbele ya kamati ya maadili.pamoja na mambo mengine yawezekana kamati ya maadili ikamkuta na kosa kulingana na kanuni za uchaguzi,kutokana na hill naomba NEC was one beak at any a kosa Kwa kumpa adhabu ya kumsimamisha kufanya kampeni.maana Kwa kufanya hivyo watakuawanamuongezeavumaarufu na nguvuvzaidi kwenye kampeni zinazoendelea.na wasilisha.
Suala la kumuongezea umaarufu halipo kwenye kanuni yoyote ya Tume, Tume inaongozwa kwa Sheria kwa hyo akikutwa na kosa la wazi kabisa asiadhibiwe kwa sababu ya kumpa umaarufu? Hii hoja ya hovyo kabisa na Tume nao wakikubali kuongozwa na hoja dhaifu Kama hizi basi wajue wamepotea.

Tume isimamie Sheria Kama siku zote akikutwa na kosa adhabu zipo wazi ili iwe fundisho kwa wengine ukimuacha mtenda kosa kwa hoja dhaifu hivi je mwingine kesho akifanya the sama mistake nae utamuacha au utamchukulia hatua? Na ukimuacha tutafika? Ukimchukulia hatua si ndio mwanzo wa kuonekana Tume ni upande mmoja?
 
Swali langu limekuwa gumu kwako,kwasababu unalikwepa sana.Subiri hoja za wadau wengine userereke nazo.

Si Gumu kwani hata huyo kiongozi wa CCM, Mkapa alisema kuwa tunahitaji tume huru . Yaani yeye hajui maana ya Tume huru??

Hivi Bashiru aliposema ikiwepo Tume huru, CCM haiwezi kushinda , hivi haelewi maana ya Tume huru ??

Ni wewe tu unayejifanya huelewi ndio unakuja na story mpya

Hivi wale wanaosimamia mechi za Yanga na Simba hutoka mbinguni?
 
Una kipaji kikubwa Sana cha upumbavu
Hakika. Anataka kauli kama "sileti chakula sijaleta tetemeko", " ndani ya utawala wangu mwenye hatasoma", "Mimi ni jiwe sishauriki" nk. badala ya kulaumiwa yeye binafsi ilaumiwe serikali?

Serikali inalaumiwa kwenye Sera lakini makosa mengi ya Magufuli hayakuwa ya serikali wala ya CCM bali yake mwenyewe. Tena aliyosema Lissu ndani ya huu mwezi mmoja ni kidogo mno ngoja baada ya kesho tumuorodheshee mengine ayatoe.

Kuwaambia kina mama wapanuliwe vizuri hadharani hiyo ni adabu? Yaani hata hilo ilaumiwe serikali? Au mask za corona hazifai eti ziko kama sidilia za wanawake? Ni mengi na yatawekwa hadharani tuu, mbona Trump anayahimili yale alikuwa anaropoka?
 
Lisu ni debe tupu!

Ukiona mtu anakutaja sana ujue umemzidi.

Lakini pia mwacheni Lisu aropoke atakavyo maana ni sehemu ya tiba kwa yaliyomkuta.

Lisu ni debu tupu.
 
Kuwa upande fulani ndani ya nafsi yako ni jambo moja,ila kupendelea upande mmoja ni jambo lingine! Watu wa Tume ambao ni makada wa CCM wanafanya upendeleo wa wazi kwasababu wanajua wanalindwa na seeikali ya CCM hivyo hawawezi kuchukuliwa hatua za kisheria!Mfano ni hao waliokatwa na wakurugenzi lakini wakashinda rufaa,kungekuwa na kuwajibishwa sidhani kama wangekatwa kinyemela!..
Mkuu umejibu vizuri kuliko wote waliojaribu kuikabili hoja yangu hapo juu. Ingawa tukubaliane kwamba hakuna sehemu unaweza kupata watu wasiofungamana na upande wowote wa kisiasa.

Hata Sasa time inalalamikiwa na CHADEMA kwasababu watu wake wamelalia upande wa CCM, laiti kama watu wa tume wangekuwa upande wa CHADEMA, Amini kwamba walalamikaji wangekuwa ni CCM.

SWALI LANGU:Tunawezaje kupata time Yenye watu wasiofungamana na upande wowote wa kisiasa,hata Kama hawatateuliwa na Rais aliepo madarakani?
 
Hakuna aliedai tume utafutwe kutoka kwa malaika, na ndio maana hata hawa waliopo sio malaika.
Ngoja nikusaidie kidogo, pamoja na kuona uwezo wako wa fikra ulivyo chini sana. Tume inaweza kuundwa kwa njia mbalimbali na bila ya kutegemea manazi wa chama kimoja pekee.

Kama bado huelewi hiki, wewe huwezi kuelewa chochote.
 
Back
Top Bottom