Papa Francis: Mapenzi ya Jinsia Moja siyo Kosa, siyo Uhalifu, lakini ni Dhambi
Siyo kila dhambi ni uhalifu. Ujangili ni uhalifu lakini siyo dhambi. Uzinzi ni dhambi ila siyo uhalifu. Kubaka ni dhambi, ni kosa pia ni uhalifu.
Jambo huwa lina hesabika ni uharifu kutokana na sheria ya nchi husika ww hapo umetolea uzinzi kuwa sio uharifu lakini sio uharifu kwa mujibu wa sheria za nchi yako lakini nchi nyingine uzinzi ni uharifu kama uharifu mwingine na ukifanya unaenda jera.

Papa alicho kosea ni kuisemea dunia nzima.
 
Dhambi ya kipekee unachomwa na moto wa gesi, mkaa au kuni??
Ushoga sio dhambi ya kipekee iliyosababisha moto sodoma? Anyways, mm nimekuwa nikidhani ushoga kwa wakristo ni dhambi ya kipekee sana huenda nilikuwa wrong.

Basi kwa sababu ushoga na pampas ni mapacha, wanaume tukubaliane kuwa ni dhambi ya kipekee isiyofaa hata kama papa hataki.
 
Hello Wadau.

Papa Francis wa RC ya Vatican ameupiga Mwingi Kwa Kuunga mkono ushoga na kusema Mashoga sio wahaliifu, na kwamba ni Wana wa Mungu pia.🙄🙄

Haijaeleweka mara Moja ikiwa huu ndio Msimamo wa Kanisa Katoliki au ni maoni ya binafsi ya Papa Francis.

Commets ziwe fupi fupi tafadhali.

------
Papa Francis amekosoa sheria zinazoharamisha mapenzi ya jinsia moja kuwa "sio haki", akisema Mungu anawapenda watoto wake wote jinsi walivyo na kuwataka maaskofu wa Kikatoliki wanaounga mkono sheria hizo kuwakaribisha watu wa LGBTQ kanisani.

"Kuwa mpenzi wa jinsia moja si kosa," Francis alisema wakati wa mahojiano Jumanne na The Associated Press.

Francis alikiri kwamba maaskofu wa Kikatoliki katika baadhi ya sehemu za dunia wanaunga mkono sheria zinazoharamisha mapenzi ya jinsia moja au kubagua jamii ya LGBTQ, na yeye mwenyewe alitaja suala hilo kwa maneno ya "dhambi".

Lakini alihusisha mitazamo hiyo na asili ya kitamaduni na kusema maaskofu hasa wanahitaji kupitia mchakato wa mabadiliko ili kutambua utu wa kila mtu.

"Maaskofu hawa wanapaswa kuwa na mchakato wa uongofu," alisema, akiongeza kwamba wanapaswa kutumia "huruma, upole, kama Mungu ana kwa kila mmoja wetu".

Baadhi ya nchi 67 au mamlaka duniani kote zinaharamisha shughuli za ngono za watu wa jinsia moja zilizokubaliwa, 11 kati ya hizo zinaweza au kutoa hukumu ya kifo, kulingana na Human Dignity Trust, ambayo inafanya kazi kukomesha sheria hizo. Wataalamu wanasema kwamba hata pale ambapo sheria hazitekelezwi, zinachangia unyanyasaji, unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya watu wa LGBTQ.

Nchini Marekani, zaidi ya majimbo kumi na mbili bado yana sheria za kupinga mapenzi ya jinsia moja kwenye vitabu, licha ya uamuzi wa Mahakama ya Juu wa 2003 kutangaza kuwa ni kinyume cha katiba.

Umoja wa Mataifa mara kwa mara umekuwa ukitoa wito wa kukomeshwa kwa sheria zinazoharamisha mapenzi ya jinsia moja , ukisema zinakiuka haki za faragha na uhuru wa kutobaguliwa na ni ukiukaji wa majukumu ya nchi chini ya sheria za kimataifa kulinda haki za binadamu za watu wote, bila kujali mwelekeo wao wa kijinsia au utambulisho wa kijinsia.

Akitangaza sheria kama hizo "sio za haki", Francis alisema Kanisa Katoliki linaweza na linapaswa kufanya kazi ili kukomesha. "Lazima ifanye hivi. Ni lazima ifanye hivi,” alisema.

Francis alinukuu Katekisimu ya Kanisa Katoliki kwa kusema wapenzi wa jinsia moja lazima wapokewe na kuheshimiwa, na hawapaswi kutengwa au kubaguliwa.

"Sisi sote ni watoto wa Mungu, na Mungu anatupenda jinsi tulivyo na kwa nguvu ambayo kila mmoja wetu anapigania utu wetu," Francis alisema, akizungumza na AP katika hoteli ya Vatican anakoishi.

Sheria hizo ni za kawaida barani Afrika na Mashariki ya Kati na ni za wakati wa ukoloni wa Waingereza au zimeongozwa na sheria za Kiislamu.

Baadhi ya Maaskofu wa Kikatoliki wameziunga mkono kwa nguvu kwamba zinaendana na mafundisho ya Vatikani ambayo yanachukulia vitendo vya mapenzi ya jinsia moja kuwa "vina machafuko ya asili", huku wengine wakitaka zibatilishwe kama ukiukwaji wa utu msingi wa binadamu.

Mnamo mwaka wa 2019, Francis alitarajiwa kutoa tamko la kupinga kuharamishwa kwa mapenzi ya jinsia moja wakati wa mkutano na vikundi vya haki za binadamu ambavyo vilifanya utafiti juu ya athari za sheria kama hizo na kile kinachoitwa "matibabu ya ubadilishaji".

Hatimaye, papa hakukutana na makundi, ambayo badala yake yalikutana na mtu Nambari 2 Vatikani, ambaye alithibitisha tena "hadhi ya kila mtu na dhidi ya kila aina ya vurugu".

Siku ya Jumanne, Francis alisema kuna haja ya kuwa na tofauti kati ya uhalifu na dhambi kuhusiana na mapenzi ya jinsia moja.

"mapenzi ya jinsia moja si kosa," alisema. "Sio uhalifu. Ndio, lakini ni dhambi. Sawa, lakini kwanza tutofautishe kati ya dhambi na uhalifu.”

"Pia ni dhambi kukosa hisani," aliongeza.

Mafundisho ya Kikatoliki yanashikilia kwamba ingawa wapenzi wa jinsia moja lazima waheshimiwe, vitendo vyao "vina machafuko ya asili". Francis hajabadilisha mafundisho hayo, lakini amefanya kufikia jumuiya ya LGBTQ kuwa alama mahususi ya upapa wake.

Kuanzia na tamko lake maarufu la 2013: "Mimi ni nani kuhukumu?" alipoulizwa kuhusu kasisi aliyedaiwa kuwa ni mpenzi wa jinsia moja , Francis ameendelea kuhudumu mara kwa mara na hadharani kwa jumuiya ya wapenzi wa jinsia moja na waliobadili jinsia .

Akiwa askofu mkuu wa Buenos Aires, alipendelea kutoa ulinzi wa kisheria kwa wapenzi wa jinsia moja kama njia mbadala ya kuidhinisha ndoa zao, jambo ambalo mafundisho ya Kikatoliki yanakataza.

Licha ya mawasiliano hayo, Francis alikosolewa na jumuiya ya Wakatoliki wa LGBTQ kwa amri ya 2021 kutoka ofisi ya mafundisho ya Vatikani kwamba kanisa haliwezi kubariki muungano wa watu wa jinsia moja "kwa sababu Mungu hawezi kubariki dhambi".

Vatikani mwaka wa 2008 ilikataa kutia saini tamko la Umoja wa Mataifa lililotaka kukomeshwa kwa mapenzi ya jinsia moja, ikilalamika kuwa maandishi hayo yalikwenda nje ya upeo wa awali na pia yalijumuisha lugha kuhusu "mwelekeo wa kijinsia" na "utambulisho wa kijinsia" .

Katika taarifa yake wakati huo, Vatikani ilizitaka nchi kuepuka "ubaguzi usio wa haki" dhidi ya wapenzi wa jinsia moja na kukomesha adhabu dhidi yao.


Chanzo: BBC Swahili
Na ikumbukwe litakalo funguliwa Duniani na mbinguni linafunguliwa, papa awe makini
 
Wewe ni mkatoliki?
The worst Pope in history! He is teaching against the church teaching! He has turned the Vatican to be a pagan state!

Too much confusion against church teaching! Mkristo unapaswa kulijua Kanisa na mafundisho yake, utakuja wakati even the devil himself anaweza kukaa pale Vatican!

Pope hapaswi kufundisha kinyume na maandiko wala mapokeo! Huu ni uasi. Bishops should publicly denounce this nonsense. Sitaki hata kutaka kumuelewa alitaka kumaanisha nini!

Rest in peace Pope Benedict. The church is in a war from within! Pray for the church.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Huwezi kusema sio uhalifu hali ya kuwa nchi nyingine kuna sheria zinazo utambua kama uharifu.
Kitu chochote uhesabika kama uharifu kutokana na sheria ya nchi husika na ndio maana unaweza kuta Tz kitu fulani ni uharifu kwa sababu ya sheria zetu lakini ukaenda kenya ukakuta hakichukuliwi ka uhalifu.
Sasa huyo papa hayo mamlaka ya kuamlia dunia nzima kuwa huu ni uharifu na huu sio uharifu ameyatoa wapi?
Laiti ungeelewa ninachojadili hapa na comments kama mbili zilizopita na zinazofuata wala usingeandika haya uliyoyaandika hapa
 
Fake news![emoji30]
20230125_135321.jpg
 
Duuh sipati picha ushoga uruhusiwe, kudadeki ntaanza kutembea na mafyekeo mfukoni, dume lenzangu lije linitongoze nafyekelea mbali pumbaf na nusu *****
 
Dah, nimecheka sana. Haya mambo haya yanachekesha sana.

Utashangaa Serikali ikisema mashoga wote wauawe, utashangaa baada ya siku mbili humu JF nabaki mimi na labda Maxence Melo tu, wengine pamoja na kelele zenu nina wasiwasi na hatma zenu!
Tunajua namna ya kujikinga. Ukilijua hili ni zombi dawa yake kama uwezi kemea pepo mwaga mbio hakuna jinsi.
 
Uzinzi ni dhambi kubwa sawa na ushoga nashangaa watu wanafanya Uzinzi then wanaona sio dhambi hizi nchi za Dunia ya tatu zina wajinga wengi ktk Mambo ya dini.
Usitafute justification, kama wewe unatinduliwa mtaro endelea kutinduliwa tu.
 
Wewe siijui imani yako but hili tuliweke hivi!!!

Leo mtaani pana shoga mpagani ametaka kusikia neno la Mungu abadilike ila akapendezwa na mafundisho ya Kanisa Catholic halafu ikawa Askofu wa jimbo husika alishatoa kauli kwamba jamii hiyo haitakiwi hapo Kanisani unadhani atathubutu kuingia?hapa nimezingumza mfano ndani ya Marekan

Kwenye bold ktk post yako kiongozi wetu mkuu Yesu Kristo alishatuonya "ya Kaiser apewe Kaiser (heshima kwa katiba za nchi ambako waumini wanaishi) ya Mungu apewe Mungu (kutowafukuza wale wanaohisiwa kuwa na dhambi sana.

Ni vitu vipo wazi ukitaka kusikia unachotaka wewe sawa but taratibu zote zimeandikwa ndani ya kitabu.

Tambua uovu una nguvu,hata wasio waovu kesho watakuwa waovu KWA kigezo mbona fulani anafanya.
 
Huyu papa anaunga mkono utoaji mimba kuunga mkono ushoga sio ajabu kwake
 
Ni wapi imeonyesha kaisemea dunia nzima? Kuna nchi hata haiutambui ukristo, na sio wakristu wote kiongozi wao ni papa.
Papa ni kwaajili ya wakatoliki.
Yeye kakosoa sheria zinazo haramisha ushoga kwa maneno mengine ameziambia nchi zote duniani zilizo haramisha ushoga kuwa wana chofanya sio sahihi na waziondoe hapo ndo alipo kosea.
 
Dhambi yoyote ni kosa, yeye kama anashikishwa ukuta aseme tu mbona hata tembea yake inaonesha ni mtu gani.
 
KWA nchi za kiislamu katiba yao uzinzi ni dhambi na uhalifu pia. Kidini na kisiasa pia
 
Back
Top Bottom