Papa Francis: Mapenzi ya Jinsia Moja siyo Kosa, siyo Uhalifu, lakini ni Dhambi
Hello Wadau.

Papa Francis wa RC ya Vatican ameupiga Mwingi Kwa Kuunga mkono ushoga na kusema Mashoga sio wahaliifu, na kwamba ni Wana wa Mungu pia.🙄🙄

Haijaeleweka mara Moja ikiwa huu ndio Msimamo wa Kanisa Katoliki au ni maoni ya binafsi ya Papa Francis.

Commets ziwe fupi fupi tafadhali.

------
Papa Francis amekosoa sheria zinazoharamisha mapenzi ya jinsia moja kuwa "sio haki", akisema Mungu anawapenda watoto wake wote jinsi walivyo na kuwataka maaskofu wa Kikatoliki wanaounga mkono sheria hizo kuwakaribisha watu wa LGBTQ kanisani.

"Kuwa mpenzi wa jinsia moja si kosa," Francis alisema wakati wa mahojiano Jumanne na The Associated Press.

Francis alikiri kwamba maaskofu wa Kikatoliki katika baadhi ya sehemu za dunia wanaunga mkono sheria zinazoharamisha mapenzi ya jinsia moja au kubagua jamii ya LGBTQ, na yeye mwenyewe alitaja suala hilo kwa maneno ya "dhambi".

Lakini alihusisha mitazamo hiyo na asili ya kitamaduni na kusema maaskofu hasa wanahitaji kupitia mchakato wa mabadiliko ili kutambua utu wa kila mtu.

"Maaskofu hawa wanapaswa kuwa na mchakato wa uongofu," alisema, akiongeza kwamba wanapaswa kutumia "huruma, upole, kama Mungu ana kwa kila mmoja wetu".

Baadhi ya nchi 67 au mamlaka duniani kote zinaharamisha shughuli za ngono za watu wa jinsia moja zilizokubaliwa, 11 kati ya hizo zinaweza au kutoa hukumu ya kifo, kulingana na Human Dignity Trust, ambayo inafanya kazi kukomesha sheria hizo. Wataalamu wanasema kwamba hata pale ambapo sheria hazitekelezwi, zinachangia unyanyasaji, unyanyapaa na ubaguzi dhidi ya watu wa LGBTQ.

Nchini Marekani, zaidi ya majimbo kumi na mbili bado yana sheria za kupinga mapenzi ya jinsia moja kwenye vitabu, licha ya uamuzi wa Mahakama ya Juu wa 2003 kutangaza kuwa ni kinyume cha katiba.

Umoja wa Mataifa mara kwa mara umekuwa ukitoa wito wa kukomeshwa kwa sheria zinazoharamisha mapenzi ya jinsia moja , ukisema zinakiuka haki za faragha na uhuru wa kutobaguliwa na ni ukiukaji wa majukumu ya nchi chini ya sheria za kimataifa kulinda haki za binadamu za watu wote, bila kujali mwelekeo wao wa kijinsia au utambulisho wa kijinsia.

Akitangaza sheria kama hizo "sio za haki", Francis alisema Kanisa Katoliki linaweza na linapaswa kufanya kazi ili kukomesha. "Lazima ifanye hivi. Ni lazima ifanye hivi,” alisema.

Francis alinukuu Katekisimu ya Kanisa Katoliki kwa kusema wapenzi wa jinsia moja lazima wapokewe na kuheshimiwa, na hawapaswi kutengwa au kubaguliwa.

"Sisi sote ni watoto wa Mungu, na Mungu anatupenda jinsi tulivyo na kwa nguvu ambayo kila mmoja wetu anapigania utu wetu," Francis alisema, akizungumza na AP katika hoteli ya Vatican anakoishi.

Sheria hizo ni za kawaida barani Afrika na Mashariki ya Kati na ni za wakati wa ukoloni wa Waingereza au zimeongozwa na sheria za Kiislamu.

Baadhi ya Maaskofu wa Kikatoliki wameziunga mkono kwa nguvu kwamba zinaendana na mafundisho ya Vatikani ambayo yanachukulia vitendo vya mapenzi ya jinsia moja kuwa "vina machafuko ya asili", huku wengine wakitaka zibatilishwe kama ukiukwaji wa utu msingi wa binadamu.

Mnamo mwaka wa 2019, Francis alitarajiwa kutoa tamko la kupinga kuharamishwa kwa mapenzi ya jinsia moja wakati wa mkutano na vikundi vya haki za binadamu ambavyo vilifanya utafiti juu ya athari za sheria kama hizo na kile kinachoitwa "matibabu ya ubadilishaji".

Hatimaye, papa hakukutana na makundi, ambayo badala yake yalikutana na mtu Nambari 2 Vatikani, ambaye alithibitisha tena "hadhi ya kila mtu na dhidi ya kila aina ya vurugu".

Siku ya Jumanne, Francis alisema kuna haja ya kuwa na tofauti kati ya uhalifu na dhambi kuhusiana na mapenzi ya jinsia moja.

"mapenzi ya jinsia moja si kosa," alisema. "Sio uhalifu. Ndio, lakini ni dhambi. Sawa, lakini kwanza tutofautishe kati ya dhambi na uhalifu.”

"Pia ni dhambi kukosa hisani," aliongeza.

Mafundisho ya Kikatoliki yanashikilia kwamba ingawa wapenzi wa jinsia moja lazima waheshimiwe, vitendo vyao "vina machafuko ya asili". Francis hajabadilisha mafundisho hayo, lakini amefanya kufikia jumuiya ya LGBTQ kuwa alama mahususi ya upapa wake.

Kuanzia na tamko lake maarufu la 2013: "Mimi ni nani kuhukumu?" alipoulizwa kuhusu kasisi aliyedaiwa kuwa ni mpenzi wa jinsia moja , Francis ameendelea kuhudumu mara kwa mara na hadharani kwa jumuiya ya wapenzi wa jinsia moja na waliobadili jinsia .

Akiwa askofu mkuu wa Buenos Aires, alipendelea kutoa ulinzi wa kisheria kwa wapenzi wa jinsia moja kama njia mbadala ya kuidhinisha ndoa zao, jambo ambalo mafundisho ya Kikatoliki yanakataza.

Licha ya mawasiliano hayo, Francis alikosolewa na jumuiya ya Wakatoliki wa LGBTQ kwa amri ya 2021 kutoka ofisi ya mafundisho ya Vatikani kwamba kanisa haliwezi kubariki muungano wa watu wa jinsia moja "kwa sababu Mungu hawezi kubariki dhambi".

Vatikani mwaka wa 2008 ilikataa kutia saini tamko la Umoja wa Mataifa lililotaka kukomeshwa kwa mapenzi ya jinsia moja, ikilalamika kuwa maandishi hayo yalikwenda nje ya upeo wa awali na pia yalijumuisha lugha kuhusu "mwelekeo wa kijinsia" na "utambulisho wa kijinsia" .

Katika taarifa yake wakati huo, Vatikani ilizitaka nchi kuepuka "ubaguzi usio wa haki" dhidi ya wapenzi wa jinsia moja na kukomesha adhabu dhidi yao.


Chanzo: BBC Swahili
Ukristo dini ya mchongo
 
Hamna papa wala sangara !!.kitabu Chao kinasema ni dhambi ila yeye anajifanya antetea means kaenda against haw ndo viongozi wa kupiga mpaka kufa kabla hawajabidili kwa matamanio ya nafsi zao.

Fuateni ukristo sio wazungu mtakuja pakuana bure.
Kweli kaka unachosema na wale wa visiwani ungewaambia waufute uislamu sio waarabu maana wadau kupaka hena watoto wa kiume na kula ndogo wanadai sunna!!!
 
Ungekuwa fair katika mjadala huu kama ungelitaja kwa jina Jimbo ambalo mbele ya Mungu unashuhudia kuwa ndugu walihukumiwa kwa kosa la ndugu yao
Huyo Padre kwenye picha aliamua kupinga hizi Clinic halali za abortion! Kuna States wamehalalisha abortion na juhudi kama hizi ni kinyume kisheria. Hivyo huyo Padre amekutwa na hatia maana hizo Clinic ni halali.

Hivyo hivyo ndoa za mashoga zikihalalishwa maana yake popote pale ukisema ni ushetani hao mashoga na mashirika yao wanakupeleka mahakamani! Utahubiri tena dhambi ya ushoga? Sijui nyinyi hata mnaelewa kinachoendelea!

Hata mahojiano yaliyopita na kuleta kelele nyingi alisema Kanisa haliwezi kubadili mafundisho lakini anaunga mkono hizo "civil right". Huoni anajichanganya tu huyu?
20230125_165257.jpg


Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Hakupaswa kuonedha kufungamana nao kwa aina yeyote ile, kuwapokea na kuishi nao kwa upendo ni kusapoti kile wanachokifanya kuwa n sahihi
Tunaambiwa kila siku ya kwamba Yesu alikuja duniani kwaajili ya watenda dhambi. Iweje watenda dhambi nyingine muwakaribishe makanisani tunasali nao na kuishi nao vizuri lakini mashoga muwatenge?
Kama kweli mnataka waachane na hiyo dhambi kwanini hamkai nao karibu mkiwaombea na kuwafundisha kuacha dhambi.
Wakristu ni watu wanafiki sana kuwahi kutokea hapa duniani.
 
Kiongozi wa kanisa katoriki papa Francis amekisoa sheria zinazo haramisha Ushoga na kuwataka baadhi ya maaskofu wanao ziunga mkono sheria hizo kuacha Mara moja.
Kwa mujibu wake ana sema ushoga si uharifu, wala mashoga si waharifu bali na wao ni watoto wa Mungu hivyo kuwasakama ni dhambi.
Amesisitiza kuwa mapenzi ya jinsia moja sio kosa wala si dhambi.


Screenshot_20230125-163645.jpg
 
Huo ni mtazamo wako lakini yeye kaamua KUPASUA JIPU.
Inasikitisha sana hii ni aibu kwa taasisi kubwa kama ROMAN CATHOLIC, huku kwetu viongozi wanalipinga vikali lakini sidhani kama hii nguvu itaendelea kuwepo kama top leader anasapoti. Hili litaleta mpasuko kati ya wanaosapoti na kupinga.
 
Tunaambiwa kila siku ya kwamba Yesu alikuja duniani kwaajili ya watenda dhambi. Iweje watenda dhambi nyingine muwakaribishe makanisani tunasali nao na kuishi nao vizuri lakini mashoga muwatenge?
Kama kweli mnataka waachane na hiyo dhambi kwanini hamkai nao karibu mkiwaombea na kuwafundisha kuacha dhambi.
Wakristu ni watu wanafiki sana kuwahi kutokea hapa duniani.
Wanapenda makasiriko.
 
huo ugomvi naupata kuanzia kwenye familia yetu hata jamii inayonizunguka.

Jana nimekutana na sheikh mmoja wa mitaa ya home kaniuliza Mbona huonekani??, nikamwambia mambo mengi tu. Alivyoondoka mi nikamwangalia kisha nikajisemea "colonialism was a deadly weapon*
🤣🤣🤣🤣🤣Kaka umetisha🤣🤣🤣
 
General hajakosea, kwa sababu Mungu na wahuruma sana, kwake Mungu pamoja na kuwa hiyo dhambi ya kukufuru Roho mtakatifu isiyo sameheka lakini bado asilimia kubwa ya maandiko ya Mungu yana msema ni mwenye kusamehe na kusahau, vipi ikiwa umemkufuru Roho ukatubia hatakusamehe na kusahau hilo kosa? Japo maelezo ya kina ni namna gani hiyo inayoweza kumkufuru Roho hakuna anae weza kutuambia.

(Nisamehewe kusema hivi) alichokosea Papa ni amejaribu kuwatetea kwa namna fulani kama kosa la kawaida kwa hao ndugu wa mapenzi ya jinsia moja, ubaya wa haya makosa ni kwa kizazi na kizazi, kama kizazi kilichotutangulia kingeachilia mianya kama hii unadhani hali ingekuwaje kwa sasa.

Ijulikane mwanaume ndiye anasimamisha kila kilicho simama, kuanzia familia taifa dini na dunia kwa ujumla, wengi wetu tumeona jinsi walivyo wanaume wanaoingikiwa jinsi walivyo, ni dhaifu sana, imagine asilimia zaidi ya 60 ya vijana wote wawe hivyo! Unadhani kuna kinachoweza kuwa kama kilivyo ? Kutakua na dini na kutakua na hao mapadre kweli?
Vipi kwa taifa ,vipi kwa familia na jamii kwa ujumla?

Kinachopaswa ni kupinga, kukataza, kukemea , kuchukua hatua kali hata kwa gharama ya uhai , ili kuokoa kizazi kijacho.

I'm so sorry kwa maoni yangu

Yote uliyoyaongea nayaelewa na kwa akili za kibinadamu ni sawa lakini kwa kuwa tunamuongelea Papa kwa kauli yake bhasi inabidi tumpime kwa matakwa ya Mungu na si matakwa yetu

Papa kasema si haki kwa nchi mfano kuwatolea hukumu ya kifo kitu ambacho kwa agano la kristu kipo sawa kwa sababu msamaha huja kwanza pale mtu atakapoomba toba

Hivyo, ukimuua mtu unamuondolea nafasi ya kutubu

Je, vipi wakisema kwenye amri za Mungu, mtu akivunja hata moja auwawe

Je, ni nani atasimama.. Jibu HAKUNA

Hiyo ndio mantiki ya papa katika msingi wa kuamini kuwa kila binadamu anastahili nafasi ya kuishi na kuomba toba

Kuhusu mantiki zetu za kibinadamu, tupo sawa kwa ubinadamu wetu lakini hatuwezi kulazimisha iwe ni mantiki ya agano jipya unless tulifute ili kurudia sheria za Musa ambapo hata mwanamke mzinzi.. Angehukumiwa kupigwa mawe hadi kufa
 
General hajakosea, kwa sababu Mungu na wahuruma sana, kwake Mungu pamoja na kuwa hiyo dhambi ya kukufuru Roho mtakatifu isiyo sameheka lakini bado asilimia kubwa ya maandiko ya Mungu yana msema ni mwenye kusamehe na kusahau, vipi ikiwa umemkufuru Roho ukatubia hatakusamehe na kusahau hilo kosa? Japo maelezo ya kina ni namna gani hiyo inayoweza kumkufuru Roho hakuna anae weza kutuambia.

(Nisamehewe kusema hivi) alichokosea Papa ni amejaribu kuwatetea kwa namna fulani kama kosa la kawaida kwa hao ndugu wa mapenzi ya jinsia moja, ubaya wa haya makosa ni kwa kizazi na kizazi, kama kizazi kilichotutangulia kingeachilia mianya kama hii unadhani hali ingekuwaje kwa sasa.

Ijulikane mwanaume ndiye anasimamisha kila kilicho simama, kuanzia familia taifa dini na dunia kwa ujumla, wengi wetu tumeona jinsi walivyo wanaume wanaoingikiwa jinsi walivyo, ni dhaifu sana, imagine asilimia zaidi ya 60 ya vijana wote wawe hivyo! Unadhani kuna kinachoweza kuwa kama kilivyo ? Kutakua na dini na kutakua na hao mapadre kweli?
Vipi kwa taifa ,vipi kwa familia na jamii kwa ujumla?

Kinachopaswa ni kupinga, kukataza, kukemea , kuchukua hatua kali hata kwa gharama ya uhai , ili kuokoa kizazi kijacho.

I'm so sorry kwa maoni yangu
Mkuu hoja yako kuhusu udhaifu wa watu wenye mapenzi ya jinsi moja ni ajabu kidogo. Katika historia tuna mifano wa wale mashujaa wa Ugiriki wa Kale, ambako mapenzi ya jinsia moja yalikuwa kawaida sana. Hao walipanga vikosi maalum vya jeshi vilivyofanywa na wapenzi wawili-wawili . Jisomee hapa "Sacred Band of Thebes". Hawakuwa wengi (maana washoga si wengi duniani) lakini walikuwa hodari sana. Pende usipende, visa hivi kuhusu udhaifu wao havina msingi...
 
Dini ni utapeli na utumwa kwa waafrika.

Religion is a crowd control..

Hau hitaji kuwa na dini ili kumjua Mungu.

Hawa viongozi wa makanisa na dini ni matapeli.

Mungu habariki watu kupitia Mtu. Haijalishi huyo mtu ni kiongozi au mtakatifu kiasi gani.

Inabidi tuwe na uhusiano mzuri na Mungu na kufanya yale yaliyo mema.

Spirituality is the personal relationship with the Divine.....
 
Back
Top Bottom