Papa Francis: Mapenzi ya Jinsia Moja siyo Kosa, siyo Uhalifu, lakini ni Dhambi
πΌπ‘›π‘›π‘Žπ‘Žπ‘™π‘–π‘™π‘™π‘Žπ‘Žπ’‰ π‘€π‘Ž πΌπ‘›π‘›π‘Žπ‘Žπ‘–π‘™π‘Žπ‘¦π’‰ π‘…π‘Žπ‘Žπ‘—π‘’π‘’π‘›.
 
Huwa sichangii topics ambazo watu hutumia hisia zaidi kuliko akili Ila nitajibu kwa huu upotoshaji unaofanywa na hii thread

Papa hajasema ushoga sio dhambi na hana mamlaka hiyo ya kuihalalisha dhambi maana ukisema anayo bhasi utaamini papa yupo juu ya mamlaka ya Mungu, kitu ambacho si kweli

Ila kitu alichomaanisha
"Kila uhalifu ni dhambi Ila si kila dhambi ni uhalifu"

Ndio maana hata wewe upo huru kuisaliti ndoa yako utakavyo pasipo dini kusema upigwe mawe kwa sababu si uhalifu

Kingine Mungu aliiteketeza sodoma na Gomorah kwa sababu ya homosexuality lakini gharika ya Mungu iliteketeza kila mtu. hata Yona alitumwa kuwahubiria watu wa ninawi kuwa hasira ya Mungu ipo juu yao na mji ungeteketezwa
Hivyo, utaona kuwa HASIRA YA MUNGU IPO KATIKA KILA UHARIBIFU NA UCHAFU TUNAOUFANYA

Na kama haitoshi, biblia ikaainisha wazi kuwa ni dhambi gani isiyosameheka

M A R K O 3:28-29 β€œAmin, nawaambia, Dhambi zote watasamehewa wanadamu, na kufuru zao watakazokufuru zote; bali mtu atakayemkufuru Roho Mtakatifu hana msamaha hata milele; ila atakuwa ana dhambi ya milele”.

Hivyo, wewe mzinzi, mlevi, msengenyaji, mwizi na kila aina ya dhambi, HASIRA YA MUNGU IPO JUU YETU SOTE lakini Mungu kwa rehema zake, wote ni wake na tunastahili msamaha wake tukijinyenyekeza na kufanya toba

Hivyo,kwa kauli hii, papa hajakosea [emoji1431][emoji1431]
Tupe msimamo wako Khs ushoga,
Are in or out, usilete habar za neutrality [emoji4]
 
Umeanza vizuri sana ila umekuja kumaliza vibaya, kwenye mtungi kamnyweso hapo umetukosea sana yaaani mimi nilewe niwe sawa na aliyefirwa???
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Brother yategemeana na imani yako kuwa dhambi kubwa ni ipi maana hata kwa msingi wa kawaida. Dhambi kubwa ni ile unayoitenda kwa kuikusudia
 
Dini ni utapeli na utumwa kwa waafrika.

Religion is a crowd control..

Hau hitaji kuwa na dini ili kumjua Mungu.

Hawa viongozi wa makanisa na dini ni matapeli.

Mungu habariki watu kupitia Mtu. Haijalishi huyo mtu ni kiongozi au mtakatifu kiasi gani.

Inabidi tuwe na uhusiano mzuri na Mungu na kufanya yale yaliyo mema.

Spirituality is the personal relationship with the Divine.....
Mashoga wasibugudhiwe.
 
Tunaambiwa kila siku ya kwamba Yesu alikuja duniani kwaajili ya watenda dhambi. Iweje watenda dhambi nyingine muwakaribishe makanisani tunasali nao na kuishi nao vizuri lakini mashoga muwatenge?
Kama kweli mnataka waachane na hiyo dhambi kwanini hamkai nao karibu mkiwaombea na kuwafundisha kuacha dhambi.
Wakristu ni watu wanafiki sana kuwahi kutokea hapa duniani.
Hata iweje siwezi kukubaliana na ushoga, yani waruhusu kufungisha ndoa za jinsia moja kwan hiyo ndio namna ya kuitokomeza hiyo dhambi?
Nitajie hizo dhambi nyingne unazosema tunazikaribisha.
 
Kwani Kanisani tunatambuana kwa dhambi zetu? Hata muda wa meza ya Bwana kila mtu anaenda kwa kupima hali yake ya kiroho. Kanisa halijawahi kutenga mashoga ila kama huo ushoga ni bayana kasisi anaweza kukataa kukupa Ekaristi ila sio kukatazwa kupata huduma zingine za wokovu kama kitubio, kusali misa bila kupokea Ekaristi n.k

Haya mambo yakipata hizo "civil right" alafu shoga akajiunga seminari mkimfukuza ni kinyume cha sheria maana hizo seminari zinasajiliwa kisheria pia.

Sisi wote wadhambi tuombe "civil right" ? Wanaojiuza nao wakipata nguvu nao tuwatambue kisheria then shule ikijua mwanachuo anajiuza asiguswe sababu ni halali?

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Hata iweje siwezi kukubaliana na ushoga, yani waruhusu kufungisha ndoa za jinsia moja kwan hiyo ndio namna ya kuitokomeza hiyo dhambi?
Nitajie hizo dhambi nyingne unazosema tunazikaribisha.
Ni wapi amesema ndoa za jinsia moja zimeruhusiwa.? Labda imenipita hii nionyeshe tafadhali.

Pia hakuna mahali amekwambia uukubali ushoga, ukatae na uendelee kuukataa lakini mashoga ni binadamu kama binadamu wengine wanaofanya uzinzi na ufiraji ambao wapo humu kwenye huu uzi kuupinga ushoga.
 
Kwani Kanisani tunatambuana kwa dhambi zetu? Hata muda wa meza ya Bwana kila mtu anaenda kwa kupima hali yake ya kiroho. Kanisa halijawahi kutenga mashoga ila kama huo ushoga ni bayana kasisi anaweza kukataa kukupa Ekaristi ila sio kukatazwa kupata huduma zingine za wokovu kama kitubio, kusali misa bila kupokea Ekaristi n.k

Haya mambo yakipata hizo "civil right" alafu shoga akajiunga seminari mkimfukuza ni kinyume cha sheria maana hizo seminari zinasajiliwa kisheria pia.

Sisi wote wadhambi tuombe "civil right" ? Wanaojiuza nao wakipata nguvu nao tuwatambue kisheria then shule ikijua mwanachuo anajiuza asiguswe sababu ni halali?

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
Padre akikataa kumpatia shoga ekaristi atakuwa amebagua. Kwasababu padri huyo huyo anampatia mtu ekaristi akifahamu fika huyu ni mzinzi, mlevi au mwizi. Mbona hawabagui hao?

Pia tambua ya kwamba kuna nchi ambazo prostitution imeruhusiwa na wamewekewa sheria kodi wanalipa vzr tu.

Na kama nyie wakristu mnaamini ya kwamba Mungu ndo anatoa hukumu iweje mlete makasoriko kwenye hili? Mnamsaidia Mungu kuhukumu ama vipi?
 
Ni wapi amesema ndoa za jinsia moja zimeruhusiwa.? Labda imenipita hii nionyeshe tafadhali.

Pia hakuna mahali amekwambia uukubali ushoga, ukatae na uendelee kuukataa lakini mashoga ni binadamu kama binadamu wengine wanaofanya uzinzi na ufiraji ambao wapo humu kwenye huu uzi kuupinga ushoga.
Tayari imesharipotiwa tukio la ndoa ya jinsia moja ndani ya kanisa katoliki mwaka jana 2022. Haya ni matunda ya kuwakumbatia mashoga, hawafukuzwi kanisani lakini hawapaswi kuonesha kuwasapoti hadi kufikia ndoa.
Na kauli kama hizi zinawafanya hao mashoga kuwa na nguvu na kuona ni haki yao kuishi hivyo( ni dhambi kama ulivyosema) dhambi haikumbatiwi inakemewa na kutokomezwa.
 
Kiongozi wa kanisa katoriki papa Francis amekisoa sheria zinazo haramisha Ushoga na kuwataka baadhi ya maaskofu wanao ziunga mkono sheria hizo kuacha Mara moja.
Kwa mujibu wake ana sema ushoga si uharifu, wala mashoga si waharifu bali na wao ni watoto wa Mungu hivyo kuwasakama ni dhambi.
Amesisitiza kuwa mapenzi ya jinsia moja sio kosa wala si dhambi.View attachment 2495357
Fake news![emoji30]
 
Back
Top Bottom