Papa Francis: Mapenzi ya Jinsia Moja siyo Kosa, siyo Uhalifu, lakini ni Dhambi
Acha justfication papa kakosea sana kukubali nchi zikubali mapenzi ya jinsia moja ni kukubali ushoga kwenye jamii, ni kukubali dhambi nilitegemea yeye ndiyo akataze nchi za ulaya kupitisha sheria za aina izoo ila yeye ndyo kahalalisha wakubaliwe hakuna mtu asiyetenda dhambi na wote ni watoto wa Muumba lkini waje kanisa kutubu na kuacha siyo waje ndani ya kanisa kma watu wa jamii izoo na kanisa halitakiwi kutambua mapenzi au ndoa za namna iyoo
Nimekuambia tuache unafiki, tuzungumze ukweli ndipo itakuwa rahisi kuondoa tatizo. Nchini kwako ulishasikia kuna kesi inaunguruma mahakamani ya Jamuhuri dhidi ya shoga?
 
Kwenda zako huko, yaani unawatetea mashoga
Sio mashoga tu, hata wazinzi, wezi, wasema uongo wapo katika jamii zetu, tunajifariji tu kujifanya sisi ni wasafi. Isitoshe katika familia yako kuna mtu ambaye ni mzinzi, mwizi, msema uongo, shoga nk ila mitandaoni unajidai kuwa tuwatenge. Huko kwenye familia mmemtenga?
 
Kama sio kosa, uhalifu, lakini ni dhambi, sasa kosa na uhalifu sio ni aina ya dhambi? Sasa yeye kazi yake sio kuwaelekeza hao mbinguni? Je, anachukua hatua gani dhidi ya dhambi hiyo? Hivi Yesu wa Nazareti wakati akiwa duniani alilishughulikia suala ili kivipi?

Hivi ile ya Sodoma na Gomola (kama ni kweli) kulikuwa hakuna serikali au serikali kama ilikuwepo ilihalalisha suala hilo?

Nature inaonesha vitendo hivyo sio sahihi. Halafu kuna sayansi inachochea mambo hayo, badala ya kuwa na sayansi ya kuzuia mambo hayo.
Kwan kila kosa ni dhambi?
Kuoa binti aliyevunja ungo ni dhambi? (bila kujari umri wake)
Na kuoa binti aliyevunja ungo (akiwa mwanafunzi may be form two) sio kosa?
Sio kila kosa n dhambi
Makosa yana ainishwa na sheria
Dhambi/uhalifu zina ainishwa na vitabu vya dini
 
Kwa hiyo umepaniki kijana tuliza jazba mambo ni taratibu....narudia kusema hakuna kiongozi wa kweli wa dini ya kiislamu anayeunga mkono ushoga na usagaji,sijamaanisha ulichoelewa.
 
Huyo papa ameongea lini na mungu akaambiwa hivyo anavyosema?? Hawa waroma nao majanga asee
 
Ni hivi, kwa sheria za nchi ya Italia, sio kosa. Lakin kwa sheria za Mungu ni dhambi. Tatizo liko wapi hapo?
 
Baadhi ya mafundisho ya kikatoriki yanakinzana na biblie hivo basi viongonzi wanahaha ni namna gan biblie ifanyiwe uchakajuaji ili wahalalishe niaovo kwa jamii,ukienda kichwa kichwa utanunua biblia ya hovyo,refer amri10 za Mungu ambavyo zimechezewa huko roma

Uzuri Pope si wa Katoriki.
Sie kama Wakatoliki hatubagui na hatuhukumu.
Mzinzi, Mwizi, Tapeli na Shoga wote wanafanya vitendo ambavyo ni dhambi lakini wakija kanisana tutasali nao.
 
Read between the lines, Anyway,

- Ni kweli sote ni wa Muumba

-Ni kweli kwa nchi zilizohalalisha ushoga, inakuwa si uhalifu.

Ila je, amesema sio dhambi?
Yeye kwan ni mwanasheria au Kiongoz wa Dini, Kiongoz wa Dini kazi yake ni kuikemea dhambi yoyote ile bila kujali kama ni uhalifu au laa kwa sheria za Kidunia.
Hayo makanisa yanaunga mkono ushoga. PERIOD
 
Yeye kwan ni mwanasheria au Kiongoz wa Dini, Kiongoz wa Dini kazi yake ni kuikemea dhambi yoyote ile bila kujali kama ni uhalifu au laa kwa sheria za Kidunia.
Hayo makanisa yanaunga mkono ushoga. PERIOD
Kasema si uhalifu, sasa ukitaka aseme ni uhalifu wakati sheria za nchi husika zimeruhusu? Na poa kasema ni dhambi sababu dini yake hairuhusu hayo mambo, ulitakaje sasa?
 
Kasema si uhalifu, sasa ukitaka aseme ni uhalifu wakati sheria za nchi husika zimeruhusu? Na poa kasema ni dhambi sababu dini yake hairuhusu hayo mambo, ulitakaje sasa?
Biblia anayoifuata inasemaje kuhusu ushoga si ni dhambi! Kwann anaonesha kuitetea kwasbb tu si uhalifu, sijui unanielewa vzur
 
Kuna watu walitegemea pope atoke aseme mashoga wote wachinjwe au wanyongwe! Jamani kaelezea vyema kwamba katika dini Ushoga ni dhambi kama dhambi zingine kwahiyo wakristo tusiwatenge mashoga kama tusivyowatenga wadhambi wengine bali tuwakaribishe kwa Bwana tuwaoneshe Ubaya wa matendo yao na tuwaombee kwa Mungu ili waache njia zao wamrudie Muumba maana wote tu watoto wa Mungu.

Ukimtenga shoga wakati mzinzi unaishi naye nyumba moja kwa Mungu hajajiongezea kitu! Lutu hakuwakimbia watu wa Sodoma aliendelea kuishi nao na kujumuika nao huku akiendelea kuwahubiria hukumi ya Mungu ikayowapata endapo wasipobadiri nyendo zao. Kama angejitenga na wale watu hata vitabu vya dini visingemwandika mpaka leo hata escort ya Malaika wa Bwana hasingeipata hivyo nafasi yake kwenye ufalme wa Mungu ingekuwa zile siti za nyuma kabisaa lakini sasa yawezekana amekaa siti za mbele au katikati
 
Juzi bwana.. jamaa mmoja alivyoona hi taarifa kutoka BBC nahisi alisikitika Sana. Hakutegemea hivyo. Yeye aliamini BBC wamemmezesha mzee maneno na Kwamba hakutamka hivyo. Yeye Ni muumini was ndoa za kiasili mume - mke..Bbc kuona hivyo wakakimbilia kumuonesha video wakati si kawaida yao kujibizana na wafuasi wake
 
Si kasema ni dhambi kwa mujibu ea imani yake? Ulitakaje sasa?
Anaitetea dhambi kwa kuwa si uhalifu😁😁, so funny...kimantiki anachomanisha huyo Kiongoz wako ni kwamba ushoga ni dhambi ila si uhalifu kwaio wasipingwe, means kwamba anaunga mkono ushoga....wakat yeye ndo ilibid awe wa kwanza kupinga na kuikemea kwamba isifanywe hiyo dhambi
 
Back
Top Bottom