Profesa Assad: Hakuna bandari inayouzwa, ni uelewa mdogo wa watu

Profesa Assad: Hakuna bandari inayouzwa, ni uelewa mdogo wa watu

"HAKUNA BANDARI INAYOUZWA, NI UELEWA MDOGO WA WATU" - Prof Assad

Points Muhimu kwenye mahojiano ya Profesa Assad pale Channel Ten kwenye kipindi cha Dira ya Uchumi

▶️Hakuna Bandari Inayouzwa, ni uelewa mbaya tu wa watu. (Sikiliza zaidi)

▶️Ukomo hauwekwi kwenye IGA, bali kwenye mikataba ya chini (Projects Agreements). (Sikiliza Zaidi)

Profesa Assad ametoa majibu mazuri kabisa, na huyu ndio Profesa wa kweli sasa, sio wale wengine akina Tibaijuka na Shivji, wachumia tumbo tu, Sikilizeni nondo kutoka kwa Prof.

Ndugu zangu za kuambiwa changanya na zako.
 
Ujumbe wake ni muhimu, unajua kwanini Magu alimkataa?. Unajua kwanini Magu alikuwa akiwakataa wasomi wenye akili huru?. aliishi na wasiwasi wa kufunikwa na uwezo wao haswa intelligence yao.
Jibu ni Moja alimkataa Kwa sababu alifichua wizi wa pesa za Umma zikiwemo hizo bil.100 zilizokutwa nyumbani kwake.

Mengine ni kujivaragua Kwa sababu ya akili ndogo aliyoisema Asad
 
Ni kweli kabisa hakuna palipoandikwa inauzwa lakini pia hakuna palipoandikwa inakodishwa wala kupangishwa hivyo basi.

Kama haiuzwi
Kama haikodishwi
Kama haipangishwi

Maana yake ni moja tu inatolewa bure...

Zaidi Assad naye anataka kugeuka mchumia tumbo.

Maana yeye anazungumzia bandari moja tu wakati IGA inasema bandari zote Tanzania na miundombinu yake.

Mwambie kachelewa kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app

Sidhani makamanda wanapinga uwekezaji...
Tatizo mkataba na haraka haraka hizi..
Haraka haraka za kutaka kutekeleza makubaliano ya huu mkataba wakati wananchi wanalalamika ni dalili tosha huu ni mkataba wa kifisadi!

Assad anataka akumbukwe kuwa bado yupo yupo lakini katika mahojiamo yake hajielekezi kwenye contentious issue ambayo ni terms za huo mkataba!!

Nobody is against investing at our ports but we want the country to benefit and not loose because of such investments. The country to loose or gain from foreign investments depends on the terms of the contracts that are signed by consenting parties!

Assad has not understood that the said contract gives monopoly powers to DpWorld hence no other operators will be allowed without their consent!!

It’s not to the interest of the country that DP World should be given a go ahead.

Samia anaweza kudharau maoni ya Wananchi na kuwasikiliza hao CHAWA wake, lakini huko mbele when the chips are down atakuwa peke yake hatamuona chawa hata mmoja!! Pengine atabakia na Abdul bas!
 
Huyo ni CAG, jaribu kutafuta uelewa mpana wa kazi alizofanya kabla hujaponda maoni yake kwa kigezo kuwa yanayofautiana na fikra zako.

Huyo anakagua kila taasisi na uelewa wake kwenye masuala ya kiuchumi haumzuii kuwa na uelewa kwenye masuala ya uwekezaji pale TPA.

Watu wangu wanateketea kwa kukosa maarifa - Biblia.
Ofisi ya CAG ina wataalamu wa fani mbalimbali na yeye kama yeye analetewa taarifa na wafanyakazi wa chini yake. Huyo yeye kama yeye hawezi kuingia ofisi zote kukagua
 
Kitu nawapendea waislamu ni kusimama na maamuzi yoyote ya muislamu mwenzao, no mater what!
Na huu mkataba kwa sehemu kubwa wanaoupinga ni Wakristo na ndio waliofungua ht kesi kule Mbeya.
Huku Waislam nao wanaunga mkono na kuna mawakili waislam wanataka kufungua kesi...
 
Ona sasa unabishana na aliyekuwa mdhibiti na mkaguzi wa mahesabu ya serikali yaani mashirika yote anajua kwa undani hali ya fedha ya serikali kuliko hata wewe ila sasa unambishia 😂
kwani ndio msahafu kuwa ukiwa mkaguzi ndio unajua kila kitu, ona sasa alivyojiweka uchi kumbe kichwani ni mgonjwa, mfundisheni sio kila kitu lazima uongee, vingine vina mipaka, waache wengine pia waseme. hata TLS waliandika yeye anakwenda kichwa kichwa kwenye media,
 
Ni kweli kabisa hakuna palipoandikwa inauzwa lakini pia hakuna palipoandikwa inakodishwa wala kupangishwa hivyo basi.

Kama haiuzwi
Kama haikodishwi
Kama haipangishwi

Maana yake ni moja tu inatolewa bure...

Zaidi Assad naye anataka kugeuka mchumia tumbo.

Maana yeye anazungumzia bandari moja tu wakati IGA inasema bandari zote Tanzania na miundombinu yake.

Mwambie kachelewa kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hawa akina Assad ndo washauri uchwara wa Samia
 
Hiyo ndio rangi halisi ya Assad.
Assad ni fisadi mzoefu akiwa kwenye bodi ya NSSF; mradi wa DEGE BEACH ni matunda ya ufisadi wao na rafiki yake Ramadhani Kitwana Dau!!
 
Points Muhimu kwenye mahojiano ya Profesa Assad pale Channel Ten kwenye kipindi cha Dira ya Uchumi

[emoji3504]Hakuna Bandari Inayouzwa, ni uelewa mbaya tu wa watu..
Huyu anachoongea ni kwa sheria gani anayotumia?

Au naye afungue kesi dhidi ya wale waliofungua kesi Mbeya.
 
Taarifa zake za ukaguzi WA TPA , TICTS na miradi mwingine ya NSSF, KADCO, KIWiRA , Loliondo inasemaje na kushauri vipi
 
Back
Top Bottom