Rais Samia atoe amri Paul Makonda naye akamatwe kwa Tuhuma zake zinazoendana na za Ole Sabaya

Na majizi yanayoiba kwa kalamu myapigie kelele yadakwe.....
sio kina Manji mnapiga kelele waachiwe
alafu kina mako... Wadakwe mtakuwa kumbafu nyie
 
Paul Christian Makonda mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam aliyepumzishwa ashitakiwe? Ashitakiwe kwa kosa gani? Huyu alikuwa karibu sana na Magufuli na kila alilolifanya lilibarikiwa na Magufuli.

Unapomshitaki Makonda tafsiri yake ni kwamba umemshitaki marehemu Magufuli. Ashitakiwe kwa kosa la kuvamia Clouds na mabunduki? Magufuli alimlinda katika hili.

Ashitakiwe kwa kosa la kula fedha za Tasaf? Magufuli alimlinda katika hili.

Ashitakiwe kwa kosa la kuingiza yale Makontena yake bandarini kinyume na sheria na taratibu? Magufuli alimlinda katika hili.

Ashitakiwe kwa tuhuma za kumshambulia Mh.Tundu Lissu? Magufuli hakutaka na hakuweza hata kuthubutu kutaja jina la Tundu Lissu mpaka anakufa.

Ashitakiwe kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka likiwemo kosa la blackmail?
 
Nashangaaa kwa nini yupo uraiani Mpaka sasa , Magufuli ndio Alimtuma akawaibie na kuwatishia matajiri atawapa case ya uhujumu uchumi?

huo ni ujambazi kama wa sabaya, kaangalie nyumba yake ya Oysterbay ndio ujiulize. Huyu dogo hizi hela alitoa wapi ya kujenga na kununua kiwanja

range na magari ya kifahari anayoendesha yeye na mke wake yote aliwapokonya wafanyabiashara
 
Paul Christian Makonda mkuu wa mkoa wa Dar es salaam aliyepumzishwa ashitakiwe?
Ashitakiwe kwa kosa gani?....
Ukiona ya Sabaya ujue Ni mwendelezo wa wote waliofanya uovu uzuri jinai haifi.
 
Mimi nashauri watu wote washtakiwe Ile baadhi ya watu wafurahi.
 
Waliodhurumiwa na huyo mtu wajitokeze wakafungue kesi mahakamani bila shaka utakuwa mwanzo mzuri wa haki
 
Bashite alikua akifatwa na mtu mwenye case au aliyedhulumiwa haki yake unamfata kwa sababu ya kuomba msaada upate haki yako lakini anauliza kwanza una million 70 ya kunipa ? Yule Jambazi alikubuu
 
Kanyanyasa, Katesa na Kapora sana tu.

Kaua, katupa sana mahiti kwenye viroba coco beach kapora magari kwa matajiri

atuambie hela za kujenga ile nyumba anayoishi sasa oysterbay na kiwanja alipata wapi ? Range Rover aliyompa mke wake na magari anayoendesha ya kifahari ametoa wapi hela, mansion aliyojenga mwanza Katoa wapi hela bashite ni Nyangumi haki itendeke kwa wote sabaya na bashite

sabaya alikua akienda kutapeli na Kurdish’s wafanyabiashara alikua anasema hiyo ni Makonda style
 
Hakuna Ushahidi Wa Maandishi kwamba Magufuli alimtuma!
Abebe msalaba wake!
waswahili wanasema tumbo linaponzaga makalio...
 
Mimi nadhani ili haki ionekane kutendeka watu wote wanaotajwa tajwa mitandaoni washitakiwe.
 
Yani unajua hapa lazima tuelewe kwamba 95% ya ungoz wa serikari ya mwendazake haukua mzuri hasa hawa RC,DC eidha kwamakusudi waljua wanachofanya, point yangu nikua sabaya anawajibika Kwa makosa yaliyo tokana natuhuma za raia wa hai,sasa ili kuleta tafasiri nzuri ya uwajibikaji ilifaa nawenzake pia washitakiwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…