unprejudiced
JF-Expert Member
- Jan 27, 2017
- 3,503
- 2,865
Kijiji fulani vilitokea vita kati ya kabila X na kabila Y. Katika vile vita kabila X walionekana kushindwa. Basi maaskari wake watatu walifanikiwa kukimbia na kujificha kwenye shimo fulani ardhini.
Wakiwa chini wamejificha juu kuna majani wakapita wanajeshi wa kabila Y wakamkanyaga askari mmoja wa kabila X. Yule askari akang'aka kwa hasira.
Askari 1: "jamani kwa nini tunakanyagana?"
Wale askari wakagundua kuna mtu pale chini wakamchoma mkuki akafa.
Mwenzake kule chini akamfokea yule aliyechomwa mkuki
Askari 2: "kwa nini na wewe unasema?"
Wale askari Y wakagundua kuna mtu mwingine wakamchoma Mkuki. Akafa. Akabaki Askari mmoja aliyejificha naye akaropoka.
Askari 3: "Aheri ya mimi sijasema"
Naye wakamgundua wakamchoma mkuki akafa.
Ole Sabaya kilichomponza ni kule kusema. Kama angenyamaza watanzania walikuwa wameshasahau mabaya yake. Alipoenda kulalamika kwenye TV kuwa anakanyagwa ndipo alipo haribu.
Makonda amekuwa smart. Hajamwambia Sabaya "kwa nini na wewe unasema?" Maana angewashtua watu nao wakaanza kuchimbua yake. Makonda amenyamaza kimya.
Watanzania wamesahau zile shutma zooote zilizomhusu Makonda.wameridhika tu kuwa kwa sasa si Mkuu wa Mkoa.
Je hakuna ambaye amewaza kwenda kufungua kesi ili haya mambo kama yalikuwa kwel yakomeshwe? Je Makonda alikuwa anasingiziwa ule uhalifu na uhalamia?
Pongezi kwa Makonda. Pamoja na kukanyagwa ameendelea kunyamaza. Maana akisema tu kuwa "anakanyagwa" watu watagundua uwepo wake.
" Aheri ya mimi sikusema"
Acha umbeya. Kama una uhakika na ushahidi, Nenda mahakamani. Mnaboa sana, mwanadamu anatumia akili na ufundi kumpiga mtu majungu. Kwa aina ya uandishi huu, ungeweza kupeleka ushahidi mahakamani na kumshtaki. Acha kuvunja heshima watu.