Rais Samia: Hatukutoa fursa ya Mikutano ya hadhara watu wakavunje sheria, wasimame kutukana, kukashifu na kuchambua dini za wengine

Rais Samia: Hatukutoa fursa ya Mikutano ya hadhara watu wakavunje sheria, wasimame kutukana, kukashifu na kuchambua dini za wengine

Naamini si lengo la Mh. Rais kuminya Democrasia, isipokuwa kuna wahuni ambao kwa haraka haraka ni kama wanataka kuonesha wanamsaidia Mh. Rais ingawa kiuhalisia sio kweli.
Mh. Rais awaite na kuwakanya ili kutoendeleza negativity zinazoharibu umoja wa kitaifa na maridhiano kwa sababu hata wakati Mh. Rais anafanya maridhoani hawajui what was her good intention !!
Unaweza ukawa sahihi, lakini ni jukumu la Rais kukemea huo uhuni adharani ili watu wajue hujuma anayofanyiwa na hao wahuni.
 
SSH aache hadaa na utapeli. Hata kubadilisha sheria ya tume ya uchaguzi amashindwa.

Juzi amemteua mkwe kwenda tamisemi kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa wakati mapendekezo ya hii tume mbovu iliyopo ilikuwa ni chaguzi zote zisimamiwe na tume ya uchaguzi.

She is all talk no action, atafika 2025 hakuna alichotimiza zaidi ya makongamano.
Tembelea nchi nzima uone mabadiliko kila kukicha.
 
Naamini si lengo la Mh. Rais kuminya Democrasia, isipokuwa kuna wahuni ambao kwa haraka haraka ni kama wanataka kuonesha wanamsaidia Mh. Rais ingawa kiuhalisia sio kweli.
Mh. Rais awaite na kuwakanya ili kutoendeleza negativity zinazoharibu umoja wa kitaifa na maridhiano kwa sababu hata wakati Mh. Rais anafanya maridhoani hawajui what was her good intention !!
Kama kilichoandikwa ni sahihi basi badala ya kuwakanya ameonyesha kuwaunga mkono kwa kudai kuwa "wanaovunja" sheria wanastahili kuadhibiwa. Na hii ni siku moja tu toka "wanaovunja" sheria kukamatwa Karatu.

Amandla...
 
Lakini pia kuna jambo mahsusi ambalo ndio kila mtu analisubiri la katiba, marekebisho ya katiba yetu ambalo nalenyewe limeanza kufanyiwa kazi na pengine mkutano huu ni kuelekea huko pia.
Kwani tunafanya marekebisho ya katiba iliyoko au tunaandika mpya kama ilivyokuwa rasimu ya Warioba?
Naona watawala wanataka kutupiga changa la macho.
 
Yot
Dini na siasa
E maneno nawili hayo bi ya Kiswahili fasaha na yote yanatokana na Kiarabu. Nisome:

 
Tatizo ni kuwa ni uongo. Huo ukumbi haujawahi kuwa Ikulu ( kimatumizi au kieneo) na haitakuja kutokea hivyo. Ila kwa sababu umezoea uongo huwezi kuona tatizo.

Amandla...
Kiswahili kimekupiga chenga.

Sikushangai, naamini lugha yako mama siyo Kiswahili.
 
Mikutano sio hisani ni kwa mujibu wa Katiba ya nchi.
Asitufokee… Kama umetukanwa nenda mahakamani.
Kama unaona unakerwa fanya moja achilia.
Karibu tunafika
Kumkamata Tundu Lissu jana hamkusoma alama za nyakati kwa ufupi mkuano wako leo kama ni mabalozi walihudhuria wamekuja kukamilisha maelezo subiri majibu…

Dunia jana imejua nchi ipo kwenye utawala gani..
Acha kulalamika rekebisha unapokosea…
 
Upo huru na maoni yako, kwa lipi zaidi?

Wengine tunaona kazi zake adhimu na adimu ni njema sana.

"Wengi wape lakini wengine wasikilize" - mama Samia.

Tunakusikiliza.
Weee bibi usinifokee!
 
CCM ni wapumbavu kiasi gani?? Kwahiyo huyu bibi anahisi kufanyika kwa mikutano ya hadhara ya chama ni msaada toka kwake???

Yani wamejitwika umungu mtu kiasi cha kuamini haki za raia ni msaada kutoka kwao.

Laana ya milele iwakumbe hawa ma CCM.
 
Mikutano sio hisani ni kwa mujibu wa Katiba ya nchi.
Asitufokee… Kama umetukanwa nenda mahakamani.
Kama unaona unakerwa fanya moja achilia.
Karibu tunafika
Kumkamata Tundu Lissu jana hamkusoma alama za nyakati kwa ufupi mkuano wako leo kama ni mabalozi walihudhuria wamekuja kukamilisha maelezo subiri majibu…

Dunia jana imejua nchi ipo kwenye utawala gani..
Acha kulalamika rekebisha unapokosea…
Bi mama anahisi katoa ihsan.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akishiriki Mkutano Maalum wa Baraza la Vyama va Siasa na Wadau wa Demokrasia katika ukumbi wa JNICC leo tarehe 11 Septemba, 2023 katika viwanja vya Ikulu, jijini Dares Salaam.


Kituo cha TCD kinafanya kazi vizuri tangu Rais Samia aingie madarakani, na ndie amekipa uhai. TCD ilifanya mkutano na wadau kujadili hali ya demokrasia kuelekea chaguzi za 2024 na 2025, baada ya kujadili kuna mambo tulifanyia maazimio na tutayaleta hapa.

Kuhusu Katiba, mchakato wa kupata katiba mpya uweze kuendelea, lakini kwa muda uliopo huenda tunaweza tusipate Katiba Mpya. Lakini mabadiliko ya katiba yanaweza kufanyika ikiwemo kufanya mabadiliko kifungu cha 74 cha Katiba ili tume huru iweze kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025.

Pawepo mgombea binafsi, kufanyia marekebisho kifungu cha 39 (2) cha katiba ya sasa kuhusu Rais na kifungu cha 67(1) kuhusu wagombea ubunge. Kuwa Rais atangazwe akishinda kwa zaidi ya 50% ya kura kwa hiyo kurekebisha kifungu cha 41 (6) na uchaguzi wa Rais uweze kuhojiwa mahakamani hivyo kubadilisha kifungu cha 41 (7).

JENISTA MHAGAMA, WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE NA URATIBU)
Amemshukuru Rais Samia kwa kukubali kuwa mgeni rasmi kwenye mkutano huu.

Kwenye siku tatu za Mkutano huu, wajumbe watashiriki kujadiliana ni namna gani taifa letu litaimarisha na kuboresha demokrasia hapa nchini.

Pia, tathimini ya maoendekezo ya kikosi kazi yatajadiliwa kwenye mkutano huu.

Rais Samia amedhihirisha kuwa ni kiongozi anayezingatia utawala bora na kutenda haki kwa watanzania wote.

SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
Leo tunapokutana na kuzungumza mapendekezo ya kikosi kazi ni mapendekezo ambayo wote wadau wa siasa nchini wameyaleta kwa pamoja.

Tutapishana tu kwa jinsi ya kusukuma utekelezaji, huyu anataka kalileta leo lifanywe kesho, mwingine ana subira kidogo, lakini wote maono yetu ni kama yanaenda pamoja.

Tayari Serikali imeanza kuchukua hatua ya baadhi ya mapendekezo ya kikosi kazi na mnayajua, kwa mfano kuruhusu Mikutano ya hadhara, tayari imeruhusiwa watu wanakwenda na tunawasikia yanayosemwa huko.

Lakini pia tulishauriwa kuunda kanuni za kuendesha hiyo mikutano ya hadhara, zimeundwa na zinatekelezwa, hilo limeshafanyika.

Lakini pia kuna jambo mahsusi ambalo ndio kila mtu analisubiri la katiba, marekebisho ya katiba yetu ambalo nalenyewe limeanza kufanyiwa kazi na pengine mkutano huu ni kuelekea huko pia.

La mikutano ya hadhara, tumeruhusu tukiwa na nia ya vyama vya siasa vizungumze wananchi wasikie sera zao, mada zao, mipango yao ili vyama vikue na virudishe watu wale walio wapoteza, vyama visimame, viwe madhubuti, tukienda kwenye uchaguzi kila chama kimejijenga vya kutosha na ndio maana ya kutoa fursa hii ya mikutano ya hadhara.

Hatukutoa fursa ile watu wakavunje sheria, watu wakasimame kutukana, watu wakasimame kukashfu, watu wakasimame kuchambua dini za watu. Lakini sishangai kwanini haya yanatokea, kwa sababu ya kuzungumzwa hakuna.

Tulianza na katiba, tukaenda ikakatika katikati, bandari imeenda sasa katiba tena. Tumieni hiyo fursa kajijengeni kwa wananchi, elezeni sera zenu, mtafanya nini, ili wananchi warudi wawaunge mkono ili tukienda kwenye uchaguzi vyama vyote vimejijenga vizuri.

Uendeshaji wa Tanzania unahitaji fikra za kila mtu, hakuna mtu mwenye hati ya kuimiliki, hata kitoto kilichozaliwa yeye kina haki, ili tuendeshe vizuri kila kundi litoe mawazo tuendeshe nchi yetu.

Niseme tena, fursa hii iliyotoka isiende kuharibu neema na baraka aliyotupa Mungu. Isiende kuharibu misingi ya uendeshaji nchi hii wazee wetu waliyotuachia.

Lingine, hakuna aliye juu ya sheria. Kila anayefanya makosa sheria itamshika. Kama umekiuka sheria, sheria itakushika. Ajenda yetu kubwa kama watanzania ni kudumisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa.

Tulitoa uhuru wa maoni, maoni mengi sana yanatoka kwa watanzania, tunayaona, mazuri tunayachukua na mengine unayapima maoni yao. Nina kikundi maalumu kinachoangalia maoni yote maoni na kuchukua yale mazuri na kuyaweka kwenye mipango yetu kuyafanyia kazi.

Kuna uhuru wa maoni lakini huu uhuru wa maoni una mipaka yake, sio tu kisheria, hata kibinadamu.

Yaani nimesikiliza hotuba ya Maza, ije mvua lije jua lazima aendelee 2025... Labda kwa mapenzi ya Mungu mambo yabadilike.

Eti anadai Watanzania hawajui katiba. Sasa sijui wakati akiwa Spika wa Bunge la katiba alikuwa haijui hilo.

Hivi kuna nchi gani ambazo wananchi wake wanaijua katiba tofauti na nchi yetu!?
 
Kwamba wametoa Fursa ?!!!!

Sio kwamba ni Haki ya Kikatiba ? Ni pale ambapo Haki inageuka kuwa Hisani ndipo utakapojua hawa sio Watumishi wetu wala Viongozi bali ni Watawala....
 
Back
Top Bottom