Rais Samia: Kuna mtu kakopa benki zetu 5 katoweka

Rais Samia: Kuna mtu kakopa benki zetu 5 katoweka

Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo wakati akipokea Ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) Ikulu Jijini Dar es salaam amehoji kuhusu mikopo chechefu na kusema kuna baadhi ya Maafisa wa Benki wanashirikiana na Wateja kupitisha mikopo kinyume na inavyotakiwa kisheria.

“Kuhusu mikopo chechefu na yenyewe unajiuliza why mikopo chechefu?, hivi ingekuwa Benki zinazotoa mikopo ni Benki binafsi kwenye rekodi zao kungekuwa na mikopo chechefu?, kusingekuwa, wetu sisi wa Serikali wanashindwa nini mpaka kunakuwa na mikopo chechefu?, kuna ushirikiano baina ya Maafisa wa Benki na hao wanaoenda kukopa, andika nitakupitishia ukipata chako hiki changu hiki, hailipiki tunasema mikopo chechefu”

“Kuna Mtu, Mfanyabiashara kakopa Benki zetu sita sijui tano Mabilioni kila Benki, kachukua fedha yetu kaitoa nje na yeye kaondoka, leo tunasema mikopo chechefu mlipompa huyu!, dhamana zote alizoweka ni feki, zote feki, kama sio ushirikiano kitu gani?

Lakini Watu wanazunguka tunawatazama, wapo na wanajua walichokifanya, hii mikopo chechefu itachechemea mpaka tujirekebishe na inapochechemea na Nchi inachechemea”

WANAJAMVI HEBU TUJUZANE HUYU ANAYETAJWA HAPA NI NANI?

Hivi mpaka hapo yule Mwigulu anatosha??
 
Kuna Raos amewahi chukua hatua dhidi ya mafisafi na wabafhirifu wa mali za umaa? Nakumbuka mmoja yeye alijua anadeal na wapinzani tu, hiyo nguvu angeiyumia kuwawajibisha hawa wezi tungeona nafuu
Magu kwenye madhimisho ya mahakama (ilikuwa miaka 100 ya mahakama),aliongea mbele ya jaji mkuu kwamba wazipush kesi za mafisadi ambazo kwa kinywa chake alisema kama kesi zingeendeshwa serikali ilikuwa na uwezo wa kuingiza 300+tn.Baadae mawakakili,l,wanaharakati wakiongozwa na wale madada waaojiita mashangazi,wanasiasa na baadhi ya NGO,wakadai rais dikteta anaingili uhuru wa mahakama.

Ndio maana Magu alikuwa anawambia mfisadi watoe hela aondoe kesi mahakamani, watu mkalalamika anapora hela za watu nk.

Sasa ulitaka afanye nini wakati mpaka majaji walimkwamisha.

Hii nchi ukicheka na kima lazima watakurudisha nyuma.
 
.........rais Samia kwa sasa anafahanu mengi kuhusu uongozi wa nchi serikali na watendaji Kwa ujumla lakini yeye ni mtu mwenye subira na mvumilivu sana..... ndo maana watu wanaona kama mambo yanaharibika au hachukui hatua, hii sio kweli huyu mama ni menda haki.......na niseme tu zinakuja siku ambazo mama atachukua hatua kali sana Kwa baadhi ya watendaji na watu hawataamini........ni swala la muda tu......
Acha kutupanga Mkuu!
Kwani Samia ni mgeni serikalini,anasubiri nini kuchukua hatua!
 
Kwahiyo Sa100 utaenda na mwigu tena kukopa Ili kufidia HASARA hiyo ya mabenki halafu wananchi wanaolala njaa ndo walipie Riba na mikopo hiyo?

Sa100 unapewa Ripoti Badala ya kuchukua hatua, unarudisha mpira Kwa Takukuru na vyombo vilivyoshindwa kuzuia wizi huo?

Siamini ni mfanyabiashara Kaiba, ni CCCCCM wamechota pesa za maandalizi ya uchaguzi 2024.
 
Kuna sehemu nilimsikia Rais wetu akisema mnaiba fedha zote hizo za nini? Hamtosheki?
Harafu kasema : Kama mmeshindwa kuwatoa hao wabadhirifu wa fedha za umma basi wahamisheni vituo vyao vya kazi muwapeleke kule kwenye sehemu za mapato madogo!
 
.........rais Samia kwa sasa anafahanu mengi kuhusu uongozi wa nchi serikali na watendaji Kwa ujumla lakini yeye ni mtu mwenye subira na mvumilivu sana..... ndo maana watu wanaona kama mambo yanaharibika au hachukui hatua, hii sio kweli huyu mama ni menda haki.......na niseme tu zinakuja siku ambazo mama atachukua hatua kali sana Kwa baadhi ya watendaji na watu hawataamini........ni swala la muda tu......
Hiyo si kweli mama amesinzia mno. Mwamba alikuwa halali si kwa kutaka sifa bali ku detect huu upuuzi wa majizi. Sasa yeye anasubiri tuuuu kazi kucheza mdako
 
Back
Top Bottom