Rais Samia: TAKUKURU wamefuta kesi za kubambikizia 147, Polisi na nyie jitazameni
Sijawahi kumuona Samia kama Rais mwenye kujua mamlaka yake toka akiwa makamu wa Rais na mpk sasa Rais kwa mujibu wa katiba 35/7
 
Utendaji kazi wake umeingia doa, kwa kuwa huyo mwendazake, anayedaiwa kuwa ndiyo aliyekuwa anamuagiza kufanya uovu wote huo, ametangulia mbele ya haki...........

Sasa balaa kamuachia IGP Sirro, ambaye ameelezwa hadharani na Rais Samia Suluhu, kuwa Jeshi lake ndilo linawabambikia kesi raia wasio na hatia!
Matukio mengi wamepiga watu wa usalama, na polisi kuchunguza hawawezi.
 
Kama huyu Rais aliacha kujiuzulu akiwa makamu, nani atafanya hivyo?

Maana inaonesha hakukubaliana vitu vingi sana vilivyokuwa vinatendeka enzi hizo ila aliendelea kukalia kiti cha umakamu.
 
Akiwa waziri wa mambo ya ndani enzi za utawala wa Nyerere, kuna issue ilitokea Shinyanga siikumbuki vizuri iliyohusu wizara yake akaona isiwe tabu akamuandika barua Nyerere kumuomba ajiuzulu akakubaliwa.
Mwishoe akawa Rais huku na huku, hii ndio heshima ya kuwa responsible!
 
Nimemsikia mama akisema TAKUKURU wamefuta kesi 147 walizowabambikia watu. Pigia mstari neno KUBAMBIKIA. Yani TAKUKURU wanakiri mbele ya Rais kuwa waliwabambikia watu kesi na wamekubali kuzifuta. Nimewaza sana kuhusu hao waliobambikiwa, familia zao, watoto wao na ndugu zao.

Nimemkumbuka rafiki yangu Abraham Ngoti ambaye TAKUKURU walimkamata huko Dodoma wakidai kuna kiasi kikubwa cha pesa kimeingizwa kwenye account yake. Akatakiwa kujieleza ni za nini? Wakamsafirisha usiku kama jambazi wakamleta Dar. Wakamuweka mahabusu yao kule Upanga.

Baada ya siku mbili TAKUKURU wakasema amejinyonga akiwa mahabusu. Familia haikukubaliana na taarifa hiyo kutokana na mazingira ya kukamatwa kwake hadi kufariki. Alijinyongaje mahabusu? Hakukua na ulinzi? Je inawezekana kujinyonga kwa kutumia suruali ya jeans? Inawezekana kujinyonga dirishani hadi kufa bila kujitetea kwa kushika nondo za dirisha? Inawezekana kujinyonga miguu ikiwa imegusa chini?

Maswali haya ndio yaliyofanya familia yake kuomba iundwe tume huru ifanye uchunguzi juu ya kifo cha ndugu yao. Lakini hakuna kilichofanyika. Waliambiwa maiti yenu hiyo hapo, mkazike.

Nimejaribu kuwaza hivi kama alibambikiziwa kesi kama hawa 147 anajisikiaje huko alipo. Kama wafu wanaona yanayoendelea duniani pengine anawalaani sana TAKUKURU.

Nampongeza mama kwa jitihada zake za kuibadilisha TAKUKURU. Nampongeza pia kwa kutoa maelekezo kwenye vyombo vingine kama Polisi na ofisi ya DPP. Lakini naomba atilie mkazo maelekezo hayo maana kuna wengi wamebambikiwa kesi na wanasota gerezani.

Mdude Nyagali anateseka rumande zaidi ya mwaka mmoja. Kila siku Jamhuri inaomba kesi isogezwe mbele kwa sababu ushahidi haujakamilika. Lakini ni Jamhuri hiyohiyo iliyosema imemkamata Mdude na kete za heroine nyumbani kwake. Kama kweli walimkamata na heroine ni ushahidi gani zaidi wanatafuta mwaka mzima?

Mazingira kama haya ndio yanafanya familia ya Mdude ihisi kwamba huenda kesi ya ndugu yao ni ya kubambikiziwa pia. Mama tafadhali ingilia kati. Taifa limepita kipindi kigumu sana wakati wa mwendazake, ni wakati sasa wa kuponya majeraha. We need truth and reconciliation.!

Malisa GJ

1621424155830.jpeg
 
Nimejikuta naimba:
🎼 Mungu ibariki Tanzania
Dumisha uhuru na umoja....🎼

Hapo pa Dumisha... ingebidi tuongeze - Amani, Utu Wema, Haki n.k.
 
Kwa idadi ya kesi alizotaja, Mh. Rais kathibisha kwamba kuna kesi nyingi za kubambikizwa ktk taasisi za kulinda haki. Mitaani haya tumeyajua siku nyingi. Maana nyingine ni kwamba pia kuna wafungwa wa kubabikizwa. Yeye akiwa ni mwenye madaraka juu ya hao wabambikizaji, amechukuwa hatua gani za kinidhamu? Hatupendi kusikia kwamba nimewaambia TAKUKURU sasa nawaambia Polisi, so what

Ukisha waambia wakawaachia waharifu kwa jina la kubambikizwa na hao wabambikizaji wakabaki ofisini, kuna maana yoyote? Na inavyoonekana sasa kutakuwa na mtindo mpya wa kujitoa ktk mikono ya sheria; toa kitu kidogo na unaachiwa kwa kubambikizwa kama rais anavyotaka kusikia. Tumetangaziwa walioachiwa, tutangazieni na waliobambikiza watu kesi.
 
Kwa idadi ya kesi alizotaja, Mh. Rais kathibisha kwamba kuna kesi nyingi za kubambikizwa ktk taasisi za kulinda haki. Mitaani haya tumeyajua siku nyingi. Maana nyingine ni kwamba pia kuna wafungwa wa kubabikizwa. Yeye akiwa ni mwenye madaraka juu ya hao wabambikizaji, amechukuwa hatua gani za kinidhamu? Hatupendi kusikia kwamba nimewaambia TAKUKURU sasa nawaambia Polisi, so what

Ukisha waambia wakawaachia waharifu kwa jina la kubambikizwa na hao wabambikizaji wakabaki ofisini, kuna maana yoyote? Na inavyoonekana sasa kutakuwa na mtindo mpya wa kujitoa ktk mikono ya sheria; toa kitu kidogo na unaachiwa kwa kubambikizwa kama rais anavyotaka kusikia. Tumetangaziwa walioachiwa, tutangazieni na waliobambikiza watu kesi.
Kamtoa mbungo hapo takukuru
 
Mambo ya kubambikizia kesi za kizushi wale watu mnaotofautiana kimawazo hazikuwepo wakati wa utawala wa Kambarage, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na hata sasa Mama Samia hataki kitu hiki. Heri mimi sijamtaja mwendazake kuwa ndiye pekee aliyeendekeza biashara hii uchwara.
 
Kama TAKUKURU ambacho ni chombo kilikuwa kinaaminiwa lkn bado kilikuwa na mchezo mchafu wa Kubambikizia watu kesi.

Basi tufahamu kuwa pia tabia hiyo hiyo ya kubambikizia na kuonea inawezekana kabisa kuwa inafanywa ndani ya taasisi/idara za serikali,

hivyo hakuna budi
Mhe. Rais akatumia Jicho la tatu la SIRI kuchunguza tabia za uonevu na ukandamizaji wa haki za watumishi zinazo fanywa na baadhi ya viongozi dhidi ya watumishi wao ktk Idara zote za serikali.

wapo watumishi wanaonewa sana na kubambikiwa tuhuma mbalimbali kwa sababu tu haelewani na kiongozi wake n.k, wapo watumishi wanalia na kuteseka kwa uonevu unao endelea ndani ya idara za serikali kwa kuwa bambikizia tuhuma za kimaadili ili tu kuwafukuza kazi au hata kuwa wekea kikwazo cha kupanda cheo.
wapo wanao minywa na kuchafuliwa kwa makusudi na hakuna wa kuwatetea kwa sababu tu kiongozi wake ameamua na hawezi kushindana nae,
huo ni uonevu mkubwa sana unao fanywa kwa siri na hakuna wa kubaini wala kuhoji.

hii ni dhambi kubwa inayo endelea mafichoni, ni vyema Mhe. Rais akaondoa uonevu na utesaji unaofanywa mafichoni yaaani ndani ya idara za serikali.

Mhe. Rais ondoa uonevu huu ktk mifumo ya serikali.
tunaomba Haki itawale kila mahali.
dhuluma na uonevu kamwe visiachiwe ktk awamu hii ya 6.

Endapo dhuluma na uonevu utakapo komeshwa ndipo Mungu atakavyo bariki nchi Yetu.
Mungu ibariki Tanzania,
ondoa dhuluma na ukanadmizwaji wa haki za watu haswa wasio na wa kuwatetea.
 
Hii ni baada ya kutakiwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuondoa kesi za kubambika.

====




Rais Samia Suluhu: Kwenye suala la wingi wa mahabusu, labda niseme kwamba jana nikiapisha majaji nililigusia hili, uharakishwaji wa kesi na nimezitaka taasisi zote ikiwemo jeshi la polisi ambalo uchunguzi unaanza kwenu kuharakisha chunguzi za kesi mbalimbali zilizopo ili kuharakisha kesi kusikilizwa na iadha kufutwa au mtu kuhukumiwa ipasavyo lakini pia niongee na jeshi la Polisi kupunguza kesi za kubambikiza.

Kuna mlolongo mkubwa wa makesi ya kubambikiza, huu ukipungua na mahabusu watapungua, kwasababu wengi wapo wanasubiri kuhukumiwa, kesi haiendi, ushahidi hakuna, mpelelezi anashindwa kupeleka kesi kwasababu hakuna ushahidi.

Niombe sana, nilizungumza hili na TAKUKURU, wameweza kufuta kesi 147 ambazo waliwabambikizia watu, kwahiyo nanyi Jeshi la polisi jikagueni kama kuna za aina hiyo nazo zifutwe ili tupunguze wingi wa mahabusu kwenye majela yetu.
lakini pia niongee na jeshi la Polisi kupunguza kesi za kubambikiza.

Kuna mlolongo mkubwa wa makesi ya kubambikiza, huu ukipungua na mahabusu watapungua, kwasababu wengi wapo wanasubiri kuhukumiwa, kesi haiendi, ushahidi hakuna, mpelelezi anashindwa kupeleka kesi kwasababu hakuna ushahidi.
[emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji3064][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji2827][emoji24][emoji24][emoji24]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Source ya taaarifa iko wapi mkuu?
[emoji1541][emoji1541][emoji1541][emoji1541][emoji1541][emoji1541]
Leo katika hafla ya juwaapisha majaji wapya Mh Rais Samia Suluhu Hasani amewataka jeshi la polisi, ofisi ya mwendesha mashtaka na Mahakama kuhakikisha wanaharakisha michakato ya kesi mbali mbali ili kutoa haki wa watuhumiwa badala ya kuchelewesha haki za watu.

Hili linakuja ikiwa ni kiasi cha mwezi mmoja tu ambapo Tito Magoti afisa ktk Shirika ka haki za binadamu HRLC alitoa siri na kuelezea kadhia wanazopata watuhumiwa wa kesi mbali mbali huku barua hiyo ikielekezwa kwa Mh Rais.m

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo kesi zote 147 zilikua za kuumiza watu wasiyo na hatia? kweli ngozi nyeusi hatupendani...yaani mtu anaona rahaa kwa mwenzie kupoteza rasilimali zake bila hatia yoyote.
Mkuu niombeni nikipata bilions kadhaaa mie afrika napotea. Kiongozi anaumia kuzidiwa hela na mwananchi wa kawaida. Yaaani msomi wa tra anaumia kuzidiwa hela na std4 failure. Shida ya wasomi kichwani wanajua wapo smart kutafuta hela.yaani elimu yenyewe kakariri wewe walichogundua wenzake akaingia kwenye mtihani akayatapika akapata first class. Akajua kuwa na mtaani atakuwa first class pia kutakuwepo ushindani.

Tra mfano huwa wanasumbua Sana wafanyabiashara wasio na elimu ya biashara. Yaani wanawatoa hela ya bure tu.

Pia afrika Kuna visasi na vinyongo sana.mtu akifanikiwa mwingine anaumia anatamani aanguke ili apumue.

Ndo Mana watu wenye Dola bilioni moja afrika ngozi nyeusi sijui ni dangote tu.
Kama yupo mwingine niambieni
 
Back
Top Bottom