Leo alfajiri nilipokuwa napitia vichwa vya habari vya magazeti mbalimbali, nimekutana na kichwa cha habari kilichonistajabisha sana...eti "Ufisadi Mkubwa Awamu ya Tano"
Kinachinishangaza ni kuwa "watendaji wakuu wa awamu ya tano, ni wale wale wa awamu ya sita" wakiongozwa na Bibi Samia.
Kwanini mamlaka husika zisiwachukulie hatua?
Ufusadi wa awamu ya tano ni mzuri sana kwani kuputia ufIsadi huo...
Ndoto za muasisi wa taifa hili zilitimia hasa serikali kuamia Dodoma, mradi wa umeme (Japo zipo juhudi za wazi kukwamisha) na nchi yetu ilitoka katika daraja ya umasikini na kuwa nchi ya uchumi wa kati wa chini.
Huduma za kijamii zilitolewa, tena zingine bila malipo, raslimalI za umma zililindwa sana, japo baadhi ya watanzania walizuia juhudi hizo waziwazi.
Kwanini sasa inakuwa hivi?
Mafsadi ya nchi hii, yaliyobanwa kwa muda wa miaka 5 ya JPM yamefunguliwa minyiroro, yana hasira na njaa ya kufisadi...kabla ya kufisadi yanataka kutuaminisha kuwa awamu iliyopita haikufanya chochote, yanashindwa kutambua kuwa JPM alikuwa rais ili atuineshe mwanga na sisi tumeuona na tutaendelea kuufuata daima.
USHAURI KWA AWAMU YA SITA ( Ambayo kimsingi watendaji wake wengi walihudumu awamu ya tano)
Tengenezeni legacy yenu, kujaribu kufuta legacy ya JPM kwa taifa hili ni sawa na kujaribu kukimbia kivuli chenu" Jua likichomoza lazima kivuli kitatokea tu.
Miezi ya hivi karibuni, jua la mfumuko wa bei limechomoza na kivuli cha mazuri ya JPM yameonekana dhahiri.
NADHANI ULE UTABIRI WANGU UMEANZA TIMIA,
NAwakumbusha tu kwa wale ambao hamjui kinachoendelea,
AWAMU YA SITA ili ifisadi vizuri lazima ichafue awamu ya tano, maana wanajua macho ya watanzania yameamka!
Najua hata hapa JF kuna vijana wanalipwa kuchafua serikali ya JPM cha kusikitisha hadi moderators wa jukwaa hili pendwa wameingia katika huu mkenge...si ajabu uzi wangu kufutwa.