=======
Mama Samia Suluhu Hassani ambaye ni mgombea mwenza wa kiti cha urais kupitia Chama cha Mapinduzi(CCM) amesema kuwa anawaomba wafanye kampeni kwa amani wakipita wawasikilize wala wasigombane nao.
Amesema kuwa wapo wagombea watakwenda kuwaambia kuwa walivunjwa miguu na mwingine alimsikia akisema kuwa alipigwa risasi 16.
''Watakuja kuwaambieni wameunjwa miguu lakini waulizeni ilikuwaje wakavunjwa miguu, wengine jana nilisikia mmoja anasema amemimiwa risasi 16 nataka niwaambie huyo sio askari wetu wa serikali ya chama cha Mapinduzi, askari wetu akipiga mtu tatu akamkosa atawajibika sikwambii askari aliefundishwa akapiga 16 huyo mtu atoke mzima".
Kauli hiyo ni "msiba"na kwa waislamu ukitokea msiba tunasema "innalillah wainaillahi rajuun".mama samia Suluhu iangalie ahera yako kuliko kuliko kumuangalia aliyekuteua kuwa running mate.