Uchaguzi 2020 Samia Suluhu Hassan: Askari wa Serikali ya CCM akipiga mtu risasi 3 akamkosa atawajibika

Uchaguzi 2020 Samia Suluhu Hassan: Askari wa Serikali ya CCM akipiga mtu risasi 3 akamkosa atawajibika

Nani amekwambia hawachunguzi kwani jarada limefungwa? Mrudisheni dereva aje ayatambue magari yale yaliyokamatwa. Uchunguzi unaanza na maelezo ya watu wazima muhimu waliokuwepo eneo la tukio. Hata ao wachunguzi wa nje wataanza na hao.
Waanze na walitoa kamara za CCTV pale area d Dodoma wakat polisi walisha SEMA zipo
 
Lissu amlete dereva Watanzania tupate ukweli. Kitendo cha kumficha dereva Ubeligiji kinafikirisha sana.

Pia maajabu mengine ya dunia. Lissu amekaa upande wa abiria ambao ni kushoto, risasi zinapiga mlango wa gari tena karibu na kitasa cha kufungulia mlango halafu zinajeruhi mguu wa kulia badala ya mguu wa kushoto!!

Mbaya zaidi na cha kushangaza mguu ulio upande risasi zinakotoka haukuguswa hata na risasi moja.

Halafu anasema alilaza kiti! Sasa wakati risasi zinamiminika alipata wapi nafasi hiyo. Pia ina maanaalipolaza kiti aliinua mguu wa kulia ukawa unapigwa huo tuuu!!

Pia alama za risasi kwenye gari zipo juu na sio usawa wa kiti kilicholazwa na mtu akalala!! Mama yupo sahihi kabisa!!

Queen Esther

..TL aliumia mwili mzima.

..hoja kwamba kwanini ameumia mguu wa kulia na siyo kushoto ambako risasi zilitokea haina uzito.

..kama umefuatilia TL utaona kwamba hata mkono wake wa kushoto una vyuma, na haukunjuki, hivyo umeumia kuliko mkono wa kulia.

..risasi inayopiga mfupa na kuuvunja, inaweza kuwa na madhara kuliko risasi iliyopiga msuli/nyama na kutokea upande wa pili. hicho ndicho kilichosababisha TL akaumia mkono wa kushoto kuliko wa kulia, na akaumia mguu wa kulia kuliko kushoto.

..mimi naamini Polisi wanapaswa kumhoji aliyeondoa walinzi wa area D siku ya tukio. Aliyechukua uamuzi huo atawaeleza ni nani alimtuma kufanya hivyo na itasaidia kuwabaini waliopanga na kutekeleza shambulizi lile.
 
Hizo sio risasi ni magoroli ya ndege, wewe unajua risasi kweli?
Nikuulize ww ikiwa unazijua risasi?
Nimeanza kuzichezea mwaka 2005 nikiwa volunteer kikosi kimoja huko iringa, nikaenda malezi kikosi kingine huko mtwara, 2007 kozi huko Pwani, 2013 nikaachana na kazi za utumwa baada ya kutoka OP nchi jirani, sasa sijui utanieleza nn kwenye guns, ammunition, explosives,
 
Lissu itakuwa alipigwa risasi na Wadeni wake au alikua anachukua wake za watu, ndiyo hayo matatizo kajisababishia!!
Mkuu una kipaji kikubwa sana cha kutambua mambo, namshangaa Siro hajakupa kitengo pale makao makuu!! Kumbe wasio julikana, ni rahisi kuwapata?!!
 
Na weledi wao wote CIA na Ndugu zao walimfanyia Fidel Castrol majaribio mangapi ya kumuua na yote walishindwa. Sasa itakuwaje mama atoe boko kiasi hiki? Atuambie ulinzi na CCTV nani alitoa?
 
Lakini mama kasema kweli risasi 16 kwa ashari mwenye mafunzo ni ngumu aisee...
Kwa nchi zingine zenye amani kama yetu Jeshi la Polisi linakuwa na kikosi maalum za Silaha za Moto "Police Armed Response" Hawa ndio wanakuwa specialized na mabunduki, kulenga Shabaha n.k Police wengine wanakuwa wanatoa huduma za kijamii tu kama ulizi patrol n.k

Sent from my POT-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Watu wanafata ushabiki tu nahili jambo kipo kitu ndani yake! Hivi unawezaje kurudi kwenye nchi unayowindwa na serikali husika huku ukiomba ulinzi huohuo!.. kipo kitu nyuma ya pazia.

Mama samia kasema ukweli hata msimlaumu.. kwa serikali njia za kumtaka mtu zipo nyingi tu lkn sio kwa namna ile ya lissu.. hayo maswali ya CCTV sijui walinzi n.k yatakuwa na majibu tu tatizo kuwekwa hadharani.
Ndugu kwa ufupi tu, jinsi serekali ilivyo handle swala la shambulizi dhidi ya Lissu, ilijiwekea mazingira ya kutuhumiwa. Binafsi naungana na Lissu kuituhumu kuwa inahusika na shambulizi lile.
 


=======
Mama Samia Suluhu Hassani ambaye ni mgombea mwenza wa kiti cha urais kupitia Chama cha Mapinduzi(CCM) amesema kuwa anawaomba wafanye kampeni kwa amani wakipita wawasikilize wala wasigombane nao.

Amesema kuwa wapo wagombea watakwenda kuwaambia kuwa walivunjwa miguu na mwingine alimsikia akisema kuwa alipigwa risasi 16.

''Watakuja kuwaambieni wameunjwa miguu lakini waulizeni ilikuwaje wakavunjwa miguu, wengine jana nilisikia mmoja anasema amemimiwa risasi 16 nataka niwaambie huyo sio askari wetu wa serikali ya chama cha Mapinduzi, askari wetu akipiga mtu tatu akamkosa atawajibika sikwambii askari aliefundishwa akapiga 16 huyo mtu atoke mzima".

Kumbe na hili limeanza kuwa takataka! Lilikuwa jimama lenye maadili sasa, limekengeuka
 
Back
Top Bottom