Serikali: Walimu sasa kufanya mtihani wa kupima uwezo kabla ya kuajiriwa

Utakuwa ni upumbavu wa hali ya juu.
Kwa nini iwe kwa walimu tu na si kada zingine?
Kwani walimu ndiyo waliopitisha Azimio la kubinafisishwa kwa Bandari yetu pendwa?
Huyo Prof ni Prof uchwara kabisa.
Yaliyomshinda Mungai J,anataka kuyarudia.
Anawashwa huyu!
 
Kuna kada unapata kazi bila usaili?
 

Hivi kuna taaluma Gani inachukua wenye ufaulu mkubwa tofauti na ualimu mfano udocta:uwe na D 3 yaani phys,chem,bios hiyo ni 4 ya 28 (vyuo vyote ngazi ya certificate na diploma)
Engineer:uwe na D 2 za masomo ya science somo lolote (vyuo vyote ngazi ya certificate na diploma )
Uhasibu😀 4 za masomo yeyote
Na kozi zingine zilizobaki sifa ni hizohizo..
Sasa UALIMU MWISHO NI DIV 3 ...sasa utasemaje ualimu ni chaguo la mwisho ndugu mtoa mada

NB: kama ningeambiwa nichague kazi basi ni UALIMU
 
Haaaa kumbe huwa Kuna kampeni za uwaziri?
Uwaziri ni nafasi za uteuzi, ili uwe waziri lazima kwanza uwe mbunge. Hii ndio mfano wa MWALIMU MKUU, lazima kwanza uwe Mwalimu. Au kuna usaili wa kuwa MWALIMU MKUU?
 
Wasisahau kuwapelekea na package ya mishahara kuanzia M1 na posho ya kufundishia na posho ya nyumba.

Otherwise waache ujinga.
 
Uwaziri ni nafasi za uteuzi, ili uwe waziri lazima kwanza uwe mbunge. Hii ndio mfano wa MWALIMU MKUU, lazima kwanza uwe Mwalimu. Au kuna usaili wa kuwa MWALIMU MKUU?
Ndo maana inabidi ateuliwe Kisha afanyiwe usaili ili nae tumpime uwezo wake
 
Huu mtihani tuanzea na wanasiasa tuanze na wagombea Uraisi tuje kwa wabunge tumalize na madiwa.
Wabunge, rais na madiwani mitihani yao ni uchaguzi, mkiwachagua ina maana mmeona wanafaa...
 
Kurudisha hadhi gani ambayo ualimu umewahi kuwa nayo hapa nchini!
Ualimu haujawahi pewa hadhi.
Huko vijijini walimu waliheshimika kwa sababu walikuwa wanaweza kula mboga yenye mafuta mwisho wa mwezi tofauti wanakijiji wengine?
 
Niliombwa kushiriki usaili kwenye halmashauri moja, wakati huo mimi nikiwa mtumishi kutoka serikali kuu kwenye hiyo wilaya. Sasa akaja jamaa mmoja aliyeomba nafasi ya uhasibu,na kuna bwana alikuwa ndiye acting DT wa hiyo halmashauri akaanza kumpiga maswali. Jamaa akiulizwa swali anawasahihisha kwanza wanaomuuliza kwamba nadhani kwenye swali lenu mnamaanisha hiki na hiki na then anatoa majibu. Kuna muda akawa anawapiga shule wanaomuuliza maswali akiwemo huyo acting DT. Baada ya maswali machache ilibidi wamuache na kumuambia asubiri nje maana alikuwa anawaaibisha.. [emoji23] [emoji23]
 
Hivi haya mambo Huwa mnayajuaje!? Wewe ni mkaguzi!? Kwan wakaguzi hujui ni walimu nao walikimbia!?
 
Na yeye ndo tunapendekeza afanyiwe usaili pengine anauwezo mdogo halafu hatujui
Yeye ashafanyiwa na wananchi kama mbunge. Elewa kuwa Waziri lazima uwe Mbunge, afu waziri ni mshauri wa Rais lazima uelewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…