Serikali: Walimu sasa kufanya mtihani wa kupima uwezo kabla ya kuajiriwa

WalA walimu wa watu siyo kama hawana akili ,ualimu ni kada ya pili kuwa na watu wenye matokeo mazuri kwenye ufaulu wao Tanzania,ishu tuu wengi background ya familia zao ni masikini ,wengi wanaozarau walimu ukikuta kafaulu sana ana diploma ya nursing ameingia Kwa kupata DDD D olvel na wakati walimu wengi Wana angalau div 3 kwenda juu
 
Tumeanza kufeli kama taifa kwenye maeneo mengi nyeti
Misingi isipokuwa imara hata paa nalo haliwezi kuwa imara,
Elimu yetu inachangamoto nyingi kwenye ngazi ya msingi!
Mifumo ya nyuma irudishwe
Kufaulu kidato Cha pili twende na wastani
Shule za msingi walimu wawepo wenye uwezo
 
Hivi haya mambo Huwa mnayajuaje!? Wewe ni mkaguzi!? Kwan wakaguzi hujui ni walimu nao walikimbia!?
mkaguzi hana jeuri ya kumkagua deeply mwalimu kwa sababu naye ni mwalimu huenda alikuwa kilaza na doja mkubwa wa kufundisha kibabaishaji. Yeye atimize majukumu yake arudi wilayani. Walimu wazoefu wa kazi hawaogopi wakaguzi
 
We kweli ndo ujui kitu ungejua hakuna madarasa magumu kufundisha kama hayo uliyoyataja apo
yale madarasa hutaka walimu watu wazima waliotulia wasio na papara na blabla. Pandeni juu acheni kukimbilia darasa la tatu na nne, au mshuke huko chini awali, la kwanza na pili. Kiujumla mwalimu unatakiwa ujue kufundisha madarasa yote
 
Ni ujinga mwingine na upotevu wa rasilimali pesa na muda wa vijana. Hiyo mitihani mliowafanyisha huko vyuoni haitoshi?
 
Walimu wengi ukiwapiga chenga kidogo wanapotea
 
Utumishi wanatakiwa wawe makini katika usaili wao
 
Huyu waziri ni pasua kichwa anahangaika na mambo ya hovyo kuliko mambo ya maana. Ajifunze kwa wenzake km Mwigulu, Mbarawa au January wanaofanya mambo makubwa ya kusaidia nchi. Waziri unadeal na petty issues zisizo na mashiko. Huo mtihani utahusu nini, mtu amekaa miaka 6 mtaani na frustration unawaza kumwongezea stress? Mbona ana roho ya kikatili hivyo? Yeye akitungiwa mtihani sasa hivi ana uhakika atafaulu? Ni mtihani wa nini kwanza, masomo aliyosomea miaka 3 chuoni? Ukiwa na waziri profesa anajihangaisha na mambo ya hovyo namna hii ni aibu. Abadilishwe wizara ameshalewa huko Elimu.

Mi sijawahi kuona Mkenda akifanya jambo la maana. Wahadhiri wa vyuo vikuu binafsi wanalipwa mishahara midogo kuliko walimu wa shule wala hana habari nao. Badala angalau serikali itengeneze utaratibu wa kutoa ruzuku kusaidia vyuo vikuu binafsi angalau viweze kuwalipa wahadhiri wake vizuri na kuweza kuongeza mishahara yao kila mwaka km vyuo vya umma. Taasisi zote za elimu zinawaelimisha watanzania. Sasa hivi vyuo vikuu binafsi vinaajri wastaafu na waliopo wana miaka zaidi ya 20 hawajawahi kuongezewa mishahara. Walimu wa shule mambo yao mengi yako TAMISEMI, waziri wa elimu ange-deal zaidi na vyuo vikuu, vyuo vya elimu ya kati na vyuo vya diploma. Ni kama amekosa ubunifu na amekosa mwelekeo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…