Shaka apiga ‘stop’ agizo la kuzuia bodaboda, bajaji kuingia katikati ya Mji wa Dar
Ccm kwa drama dah
“CCM kimepokea na kufuatilia malalamiko ya wananchi mbalimbali ikiwamo, machinga, waendesha bodaboda, sanjari na malalamiko hayo, CCM kinaungana na Rais Samia katika dhamira yake ya kuona nchi yetu inapangwa vizuri na kuwa kivutio kwa kuwapanga vema machinga na wafanyabiashara wengine
Tengeneza tatizo, tatua tatizo fake, jipongeze
 
Watalii wanakuja kwa maelfu kila wiki. Tembea usiishie kwenda chooni na kurudi ilipo laptop yako. Toka nje uione dunia halisi ilivyo.
Wale tulioambiwa wanakuja kwa maelfu wakati wa chuma JPM , kwani walikuwa wachache!? Au nyie wengine mnabadilika badilika kama bendera inavyofuata upepo!?
 
Mimi naona hawa ccm waache porojo za kisiasa, kupangwa na kuhamishwa ni vitu viwili tofauti. Tena kunapohusishwa na kuharibu au kupora mali za hao wahamishwao kwa kisingizio cha kupangwa.
 
Chama kitapata tabu sana kumnadi mgombea wake 2025 kwa staili hii ya kukandamiza watu wa hali ya chini na kuwakumbatia mabeberu.

Inashangaza sana kuona mwananchi akinyimwa haki ya kuwa na kipato.

Basi serikali iwalishe.
 
Hii nchi ina vituko sana.Agizo Hilo ni kwa Serikali au kwa wananchi.
 
Wale tulioambiwa wanakuja kwa maelfu wakati wa chuma JPM , kwani walikuwa wachache!? Au nyie wengine mnabadilika badilika kama bendera inavyofuata upepo!?
Ukweli ni kuwa watalii wanakuja kwa wingi, nyinyi wengine mnaishi na hasira nyingi zisizo na sababu. Hakuna wa kukusaidieni.
 
Ccm inueni kilimo nchini Ili kupunguza idadi ya machinga na bodaboda mijini, Hakuna apendae kufanya Kazi hizo shida ni njaa.
Soko la mazao ya kilimo China ni kubwa Sana litumieni
 
Ccm wateteni wapiga kura zenu.Ni upumbavu kabisa baadhi ya watu kudai eti mji unachafuliwa KILA mtza yeyeto anayo haki ya kuwepo mjini
 
Akikamatwa mwenye pikipiki kwa kuingia mujini, Shaka hataenda field kuzuia ukamataji.

Tufikie sehemu taaluma (badala ya emotions) ziamue mambo yetu! Ni tabia hii ya maamuzi yanefanya Dar kuwa mji mkubwa usiopangwa ktk afrika mashariki na kati. Makazi yasiyopangwa!!
Yule anatetea wapiga kura wake wanaonewa
 
Shaka ndie nani?
Ni mtendaji wa serikali?
Tusipokuwa makini tutajikuta kuna siku mtu kama huyu atasema mchana tulale na usiku twende kazini.
 
Daaah jamaa ameongea kwa Uchungu sana,
Asante Sana CCM kusimama na wananchi wakati wote,
Chama lazima kitetee waliokiweka madarakani,

Hongera Rais Samia,
Hongera Chongole
Hongera Shaka,
#KAZIIENDELEE
Amosi makala na wale wamamgambo wanawatimua hao wahuni ni wa chadema?
 
Huyo matacor ni nani katika serikali. [emoji34][emoji34][emoji34][emoji34][emoji34] Unajua ifike wakati na sisi raia tuanze kuwa wakali.

Huyo shaka sijui takataka gani ana wadhifa gani katika serikali hadi apingane na kiongozi wa mkoa. Fala sana huyo.
 
Katibu wa Halmashauri kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Ndugu. SHAKA HAMDU SHAKA leo Oktoba 31 atazungumza na waandishi wa vyombo vya Habari kuanzia saa 6 mchana ofisi Ndogo za CCM - LUMUMBA Dar es salaam...
Kama nani? Katika utumishi wa umma watanzania tuwe makini sio Kila mtumishi wa CCM Ni mtumishi wa umma naomba nieleweke jamani.
 
Ukweli ni kuwa watalii wanakuja kwa wingi, nyinyi wengine mnaishi na hasira nyingi zisizo na sababu. Hakuna wa kukusaidieni.
Team JPM chuma wenzako uliowasaliti ndio wana hasira. Kwani walikuomba msaada uwasaidie!?
 
Back
Top Bottom