Swali: Dunia bila Mwanaume je nani angemlinda Mwanamke?


TBH labda hayo yote yangeweza kufanyika bila uwepo wa mwanaume, sikubaliani na mleta mada wakati huo huo sikubaliani na mawazo yako kwamba mwanamke hawezi kuwa na akili/uwezo wa kufanya hayo uliyoandika

Kauli yako hapo chini inaamisha mwanaume ndiye aliyeshikilia uzao peke yake, kivipi? Bila mwanamke mwanaume anaweza kuendeleza kizazi peke yake kwa namna gani?

"Hivi duniani mngekuwepo wanawake watupu, kizazi cha binadamu kingekuwepo mpaka leo kwenye uso wa dunia?"
 
Kama yote yanaweza kufanyika bila mwanaume mbona hatuoni mchango wa wanawake. Mbona wanawake hatuoni wakija na chanjo na tiba za maginjwa. Hatuwaoni wakibuni satellite za kwenda kuvhunguza uko anga za mbali? Hatuwaoni wakijenga madaraja, magorofa, hstuwaoni wakiunda vyombo vya moto? Kama hatuwaoni wakifanya hayo sasa hivi utatuaminisha vipi wangeweza kuyafanya wakiwa peke yao?

Baada ya mwanamke kupewa elimu na access zote kama mwanaume tulitarajia kuona ongezeko la mainjinia, wanasayansi n.k lakini so far kitu ambacho feminism imekifanikisha kwa ufanisi ni kupandikiza chuki za kijinsia pamoja na kuvunja msingi wa ndoa na ustawi bora wa jamii

Kizazi cha binadamu namaanisha ya kwamba mwanamke peke ake angeweza kuzuia hayo majanga kama magonjwa peke yake.
 
Ugunduzi Muhimu wa Kisayansi
  • Marie Curie (1898): Aligundua vipengele vya kikemia vya radium na polonium na kuanzisha nadharia ya mionzi (radioactivity), jambo lililopelekea kuundwa kwa mashine za kwanza za X-ray zilizotumika vitani.
  • Rosalind Franklin (1952): Alipiga picha maarufu ya "Photograph 51" kwa kutumia miale ya X, ambayo ilionyesha kwa mara ya kwanza muundo wa DNA (double helix).
  • Dorothy Hodgkin (1964): Aligundua muundo wa atomiki wa dawa ya penicillin, vitamini B12, na insulin kwa kutumia teknolojia ya X-ray crystallography.
Uvumbuzi wa Kiteknolojia na Nyenzo
  • Ada Lovelace (1843): Alitengeneza algorithm ya kwanza ya kompyuta iliyokusudiwa kutumika kwenye mashine ya mapema ya kimekanika, na kuweka msingi wa utengenezaji wa programu (software) za kisasa.
  • Hedy Lamarr (1941): Alivumbua mfumo wa mawasiliano wa frequency-hopping, ambao leo hii ndio msingi wa usalama wa mifumo ya Wi-Fi, GPS, na Bluetooth.
  • Grace Hopper (1952): Alivumbua compiler ya kwanza ya kompyuta, ambayo hutafsiri lugha ya binadamu kwenda kwenye lugha ya msimbo (code) inayoeleweka na kompyuta.
  • Stephanie Kwolek (1965): Alivumbua Kevlar, nyuzi ngumu ya sintetiki yenye nguvu mara tano zaidi ya chuma, inayotumika sasa duniani kote kutengeneza makoti yasiyoingia risasi.

Kizazi cha binadamu namaanisha ya kwamba mwanamke peke ake angeweza kuzuia hayo majanga kama magonjwa peke yake.

??? 😃
 
Hawa wote uliowataja ukifatilia zaidi utakuta Kuna wanaume walikuwa nyuma Yao.

Mfano huyo wa kwanza Marie curie alikuwa akifanya kazi Katika maabara ya Mume wake Piere Curie Ambae ndie kinara wa mambo ya Radioactivity (mionzi).

Kwaiyo hainishangazi kusikia Marie curie amegundua hiki au kile ilihali alikuwa na gwiji la mionzi bwana Piere Curie.
 

Mwanamke kahusika ama hajahusika? Mind you haujui/sijui kahusika kwa % ngapi
 
Huo ni muendelezo wa mambo ambayo tayari yalishawekewa msingi na mwanaume. Microscope ya kuziona hizo atom ilibuniwa na nani? Mwanaume. Telescope ya kupiga picha ilibuniwa na nani? Mwanaume. Nina uhakika hao wote uliowataja kuna mentors wa kiume walikua nyuma yao

Mwanamke ameanza kushine juzi juzi tu baada kukuta kila kitu tayari kishatengenezewa mifumo na mwanaume. Kama mwanamke akibaki peke yake kuna tatizo jipya kabisa litatokea atashindwa kuli-brainstorm.
 
Yote haya umeandika in one way or another kuna ukosefu wa mwanaume mwenye busara kwenye maisha yako,
pole
 
Mwanamke kahusika ama hajahusika? Mind you haujui/sijui kahusika kwa % ngapi
Kuhusika sio issue.
Hata wewe hapo kama ungekuwa ni mke wa Piere Curie kwa Jinsi jamaa alivyo gwiji na Ile maabara yake toshelezi hata wewe tungekuwa tunakusoma kuwa umegundua Rays.

Swali jee asingekuwepo Bwana Piere Curie na Ile Lab yake,, Bi. Marie curie angeweza kufanya yote aliyofanya??
 
Mambo uliyoandika ni mambo madogo sana mkuu pengine uwezo wako mdogo wakufikiri. Anyway ,, huyo aliyesema kuhusu dunia kuwa salama sio kweli ,, mbona kuna wanawake wanao ua? Na kufanya maovu mabaya sana ? Lakini kwa upande wako hayo mambo uliyosema hakuna ushahidi kwamba jinsia ya kike itashindwa kuyafanya maana ni mambo yanayohitaji kutumia akili . Na sii ajabu kuna wanawake ambao ni madaktari wakati wewe ni mwalimu. Issue ya msingi hapa dunia haingewezekaba kuwepo kwa jinsia moja peke yake watu wangezaliana vipi? Nadhani hii ndio ingekuwa pwenti ya msingi kwako
 
Kwaiyo mkuu kuwepo madaktari wanawake na Wanaume walimu inajenga hoja Gani kwako??
 
Kwaiyo mkuu kuwepo madaktari wanawake na Wanaume walimu inajenga hoja Gani kwako??
Najaribu kumweleza huyo bwana mdogo kuwa atoe hoja za msingi . Kuonesha umuhimu wetu na kuwa dunia hainge wezekana kwa jinsia moja ,, lakini yeye amejikita kwenye mambo ya ugunduzi na taaluma nikamwambia hivyo ni vitu vinavyojifunzika na masuala ya akili hayaangalii jinsia ,, ingekuwa Ukiwa mwanaume inatosha kuwa mgunduzi basi sisi wanaume wa tanzania tungegundua madawa ndege n.k lakini kutokugundua haina maana kuwa sisi ni wanawake na waliogundua haina maana kuwa wamegundua kwasababu ni wanaume bali kwasababu wana maarifa na wameyatumia vizuri. Hoja ya msingi nikuwa bila uzao dunia isingekuwa na watu. Na uzao nilzima sisi tuwepo na wanawake nao wawepo.
 
Wanawake wangelindwa na nyoka,

Kwanza wanawake siyo weak kama wanavyotuaminisha, wamejiweka hivyo kama njia tu ya kurahisisha maisha, they can do anything man can do.

 
Kuna sehemu nimeandika hapo. Kama hatuoni wakiyafanya sasa hivi, nini cha kutuaminisha wangeweza kufanya wakiwa peke yao?
 
Ivo unavotaka dunia haitaki sasa
 
Hoja yake inamashiko.
Anajaribu kuonesha gunduzi nyingi kama sio zote tangu huko nyuma kabisa ni za wanaume.

Wanawake wamekuja kuonekana muda Ambao tayari almost Kila instrument,, Kila apparatus,, Kila formula,,, Kila lawa/principle Kila Calculations vimeshawekwa na Wanaume Kisha Wao kuvitumia kugundua hiki au kile.

Mfano Daktari wa kike Kila anachotumia hospitali kuanzia vifaa Hadi taaluma yenyewe hiyo ni innovations za wanaume kadhaa.

Anachojaribu kuhoji Ndugu Natafuta ajira ni kwamba wanawake wao wangeweza Kuyafanya hayo yote Pekee Yao??

Pia anajaribu kuhoji Leo hii ikitokea Kuna jambo jipya kabisa halipo Kwenye literatures likahitaji utatuzi jee wanawake wataweza ku brainstorm Wenyewe kama wanaume hawatakuwepo??

NB:Hapa Hatujadili Namna ya ku_utilize knowledge au kuweza kukalili mavitabu darasani na mwisho kuwa Daktari au Kuwa Mwalimu,, tunajadili Brain Capacity ya kusolve au kuinnovate something from nothing.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…