Mjadala unaomfuta mwanaume au mwanamke ili kuonyesha kuwa dunia ingekuwa sahihi zaidi jinsia moja isingekuwepo huwa inapigania uwepo wa mapenzi ya jinsia moja kwa kujitengenezea kakichaka.
Tukirudi kwenye mada, Kudhani mwanamke anahitaji ulinzi dhidi ya wanaume makatili pekee ni kutokujua historia.
Dunia haikuaanza tu na mazingira yanayomfanya binadamu anayezaliwa leo awe salama dhidi ya hatari. Majiji yenye umeme, barabara, makazi yanayotoa ulinzi yana historia kubwa sana na mwanaume.
Kabla ya mazingira ya sasa palikuwepo wanaume waliomlinda mwanamke na wanyama wakali, na baridi kali na pengine pasingekuwepo na kiumbe binadamu kama mwanaume asingesimama kwenye nafasi yake, na hata sasa, kijiji kikivamiwa na fisi, Simba, dubu ni wanaume watachukua silaha kwenda kuwakabili.
Mwanamke yeyote anayefikiri akimfuta mwanaume amefuta changamoto ya kuhitaji ulinzi asome historia, ataelewa kwanini mwanaume ni sehemu muhimu ya uwepo wake. Ukijua ulipotoka, ukajua ulipo, utapata picha ya unapokwenda.
Hakupaswi kuwa na vita Kati ya mwanaume na mwanamke. Na Wanawake hawana uspecial wowote kumzidi mwanaume and vice versa, sisi wote ni sehemu ya sababu zinazomfanya binadamu awepo. Kila mmoja asimame kwenye nafasi yake dhidi ya ukatili kwa mwanaume na mwanamke.
Nadharia ya jinsia moja ni nadharia ovu.