Tundu Lissu: Rais Samia amenilipa stahiki zangu nilizonyimwa na Magufuli

Tundu Lissu: Rais Samia amenilipa stahiki zangu nilizonyimwa na Magufuli

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amesema Rais Samia amemlipa stahiki zake kama Mbunge ambazo ni kiinua mgongo, Serikali ya Rais Magufuli ilikuwa imekataa kumlipa.

Pia, Serikali ilimuambia aandike barua pamoja na kuambatanisha na nyaraka ili apewe fedha zake za matibabu ambazo Serikali ya Rais Magufuli pia ilikataa kumlipa.

Pia Tundu Lissu amesema wanachama wa CHADEMA ambao walifungwa ama kuwekwa mahabusu kipindi cha Magufuli wameachiwa kasoro kesi chache ambazo nazo zinashughulikiwa.

Tundu Lissu alikutana na Rais Samia alipotembele nchini Ubelgiji ambapo waliongea mambo kadhaa ikiwemo stahiki hizo.

si angekaa kimya kama amelipwa kwani ni lazima auambie umma?shida ya tundu hana siri kila kitu yy ni kuropoka tu.angekuwa huku tz wezi si wangejua ana pesa hivyo wanemvamia kirahisi.atulie mama yuko kazini.
 
Sisi furaha yetu ni kuwa dhalim yuko motoni anateseka, basi.
Ni kujifariji tu kwa sababu hata angekuwa mzinifu au mshirikina tu pia angechomwa moto kama ambavyo labda wewe utachomwa moto kwa ushirikina n.k sasa hapo cha kufirahia ni nini? Kwahiyo si ajabu wewe leo ukafa ukaenda kukutana nae huko mkachomwa wote.

Sasa kama huku duniani alikufanya vibaya na wewe hukuweza kumrudishia halafu huko motoni mnaenda kuchomwa wote hapo cha kufurahi ni kipi?
 
Kwa taarifa yako sio tu Raisi Samia, hata maraisi wengine waliopita waislamu walikuwa na utu angalau, nakukumbusha linganisha uongozi wa Raisi Mwinyi, Raisi Kikwete na maraisi wengine kuanzia Nyerere, Mkapa hadi Magufuli.
Haya ni mawazo yako, na yanaweza kuwa ya upotofu. Kwangu mimi rais bora kuliko wote alikuwa Nyerere na rais mbovu kuliko wote ni Kikwete.
 
Ni kujifariji tu kwa sababu hata angekuwa mzinifu au mshirikina tu pia angechomwa moto kama ambavyo labda wewe utachomwa moto kwa ushirikina n.k sasa hapo cha kufirahia ni nini? Kwahiyo si ajabu wewe leo ukafa ukaenda kukutana nae huko mkachomwa wote.

Sasa kama huku duniani alikufanya vibaya na wewe hukuweza kumrudishia halafu huko motoni mnaenda kuchomwa wote hapo cha kufurahi ni kipi?
Furaha ni kwamba nchi imepona huyu kichaa hawezi tena kuja kuleta usumbufu
 
Mr belgiji kashachukua hela mwambie aondoke sasa kule kwa mumewe amsterdam
Wewe mbona mwaka wa tano huu unaishi Kwa dadako shemeji yako anapomkita unaishi kusonya tu,na bado ilipofika sister akiwa kwenye deiz zake itabidi ukalishwe wewe.
 
si angekaa kimya kama amelipwa kwani ni lazima auambie umma?shida ya tundu hana siri kila kitu yy ni kuropoka tu.angekuwa huku tz wezi si wangejua ana pesa hivyo wanemvamia kirahisi.atulie mama yuko kazini.
Sukuma Gang roho zinawauma ushetani tu umewazidi
 
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amesema Rais Samia amemlipa stahiki zake kama Mbunge ambazo ni kiinua mgongo, Serikali ya Rais Magufuli ilikuwa imekataa kumlipa.

Pia, Serikali ilimuambia aandike barua pamoja na kuambatanisha na nyaraka ili apewe fedha zake za matibabu ambazo Serikali ya Rais Magufuli pia ilikataa kumlipa.

Pia Tundu Lissu amesema wanachama wa CHADEMA ambao walifungwa ama kuwekwa mahabusu kipindi cha Magufuli wameachiwa kasoro kesi chache ambazo nazo zinashughulikiwa.

Tundu Lissu alikutana na Rais Samia alipotembele nchini Ubelgiji ambapo waliongea mambo kadhaa ikiwemo stahiki hizo.

Mpinzani anayetaka kumpunguzia madaraka rais, anashindwa kusema serikali imemlipa, anasema Rais kamlipa.

Kama vike rais katoa hela kwenye mfuko wake.

Inaonekana hata huyu mpinzani hawezi au hataki kumpunguzia rais madaraka.
 
Mwananchi
Advertisement

Lissu: Serikali imenilipa mafao yangu ya ubunge​

Thursday June 02 2022​

Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu amesema Serikali imemlipa kiinua mgongo chake aliochukuwa anadai baada ya kutumikia nafasi ya ubunge kwa zaidi ya miaka mitatu.

Lissu: Serikali imenilipa mafao yangu ya ubunge
kiango-data.jpg

By Bakari Kiango
More by this Author

IN SUMMARY​

  • Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu amesema Serikali imemlipa kiinua mgongo chake aliochukuwa anadai baada ya kutumikia nafasi ya ubunge kwa zaidi ya miaka mitatu.
Advertisement

Dar es Salaam. Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu amesema Serikali imemlipa kiinua mgongo chake aliochukuwa anadai baada ya kutumikia nafasi ya ubunge kwa zaidi ya miaka mitatu.
Lissu alivuliwa ubunge Juni 28 mwaka 2019 kutokana sababu mbalimbali ikiwemo ya kutojaza taarifa za mali na madeni na kutokutoa taarifa kwa Spika mahali alipo.
Wakati anavuliwa ubunge, mwanasiasa huyo alikuwa Ubelgiji akiendelea na matibabu baada ya kupigwa risasi 16 na watu wasiojulikana akiwa katika makazi yake Dodoma Septemba 2017.
Kwa muda mrefu, juhudi mbalimbali za kufuatilia kiinua mgongo chake na malipo ya matibabu hazikufanikiwa.
Februari mwaka huu, alipokutana na Rais Samia Suluhu Hassan Ubelgiji anakoishi, Lissu alifikisha kilio hicho baadaye alieleza kuwa ameahidiwa kusaidiwa.
Pia alimuomba Rais Samia kumsaidia kupata hati ya kusafiria, jambo ambalo alisema lilitekelezwa ndani ya muda mfupi.
Jana, akizungumza katika mtandao wa Club House, Lissu alisema miezi miwili iliyopita alipigiwa simu na mtu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango akamweleza kuwa mafao aliyokuwa akidai yameshalipwa kwa kumaliza madeni aliyokuwa anadaiwa na benki.
“Nilikuwa na madeni ambayo nilikopa katika benki mbili na nilishtakiwa na mojawapo ya benki hizo kwa kushindwa kulipa mkopo uliokuwa unalipwa kupitia mshahara wa ubunge.
“Alivyonipigia simu akaniambia nimelipiwa madeni yangu yote kutokana na kiinua mgongo cha ubunge.
“Kwa hiyo naweza nikasema hadharani kwamba (hilo) limefanyiwa kazi na ni jambo jema kwa kweli. Sina madeni ya benki na usumbufu niliokuwa nikiupata,” alisema.
Advertisement
Mlipaji Mkuu wa Serikali, Emmanuel Tutuba alipoulizwa, alisema ni utendaji wa kawaida serikalini kulipa madeni ya wafanyakazi na viongozi hata mafao ya wastaafu.
Tunapolipa huwa tunapeleka kwa ofisa masuuli wa taasisi husika. Kwa mbunge, kuna mfuko wa Bunge. Pesa zinapelekwa huko. Hata hizo za matibabu zinaingizwa huko pia. Ukiwasiliana na Bunge watakuwa na taarifa zaidi kwa sababu wao ndio wanaowajua wanaostahili,” alisema katibu mkuu huyo wa Wizara ya Fedha na Mipango.
Uongozi wa Bunge haukupatikana jana kuzungumzia suala hilo.
Kuhusu fedha matibabu Lissu alisema, “nililetewa ujumbe niandike barua kuomba nilipwe stahiki zangu za matibabu na nimeshaiandaa kukamilika kwa kiasi kikubwa, ingawa bado natafuta nyaraka kwa sababu nimetibiwa Kenya na Ubelgiji.”

Advertisement
MORE FROM MWANANCHI
This page might use cookies if your analytics vendor requires them. Accept
 
Attachments

  • Screenshot_20220602-163043.png
    Screenshot_20220602-163043.png
    134.7 KB · Views: 10
Hivi Ndugai anajisikiaje huko alipo?kipindi kile anasimama bungeni anasema Lissu hadai kitu na nitakuja na mkeka na wale wabwana wanaomsikiliza wanapiga meza kawa kawaida yao.

Mungu ni mwema sana.
 
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu amesema Rais Samia amemlipa stahiki zake kama Mbunge ambazo ni kiinua mgongo, Serikali ya Rais Magufuli ilikuwa imekataa kumlipa.
Ndugu yai analizungumxiaje hili?
 
Una roho na pepo mchafu ndani yako si bure mtanzania mwenzako kulipwa stahiki zake ni kupoteza pesa ya umma?
Mwenye roho mbaya na pepo mchafu ni TAL tu hapa duniani
 
Back
Top Bottom