Samahani mkuu, lakini siyaamini maneno yako haya kumhusu mhusika.Haiondoi ukweli Magufuli ni mtu wa hovyo hajatokea wa aina yake. Uzuri Samia ana sikia na kushaurika hivyo anaweza kubadilika. Hatupigi kelele kumdhalilisha, laah tunamtaka abadilike na kwa vile ni muungwana atabadilika.
"Usikivu" (feki) ulikuwa na maana yake, sasa umekwisha tambulika kuwa ilikuwa ni hadaa tu ya kutafutia sifa.
Usifikiri ni kazi rahisi kujiondoa katika mtego huu aliomo sasa hivi. Hayuko peke yake ujue, hii ni kazi ya timu maalum (genge).
Na hata akisema ajiondoe, sura yake halisi imekwisha jionyesha, hana njia ya kuiripea na kurudisha imani kwa waTanzania.