Tundu Lissu: Rais Samia na Mbarawa wameiuza Tanganyika yetu kwa Waarabu
Kama uzalendo ni kupitisha madawa ya kulevya bandarini, kupitisha baadhi ya mizigo ya wasiotaka kulipa kodi mlango wa nyuma na baadae mpitishaji kupewa chake mtaani na mwenye mzigo...
Dawa ya ulio yaandika ni kuingia mkataba kama huo?

Naona unazidi kuilaumu Serkali.
 
Basi mzee Nyerere atakuwa ametengeneza taifa la hovyo ambalo vijana wake wapo tayari kutumiwa na adui kwa sababu ya vijisent vidogo vya mboga na ujinga wa kutafakari ya kesho.
Naomba usifanye utani hapa.
Unachozungumzia hapa, kuuza nchi unataka kumhusisha Mwalimu na fikra za kijinga namna hii?

Mbona sasa mnatapatapa kiasi hiki?

Mwalimu Nyerere akubali kufanya uchafu huu wa kuinajisi nchi hii kama Samia anavyofanya sasa hivi?

Hivi ulimjua Mwalimu Nyerere wewe? Hata historia ya mambo aliyopambania nchi huijui kwa kuisoma tu?
 
Kama ameshindwa kuwawajibisha wakurugenzi na viongozi wengine kwa rushwa na matumizi mabaya ya mali ya umma kutokana na ripoti ya C.A.G, atawaweza waarabu?.

Pia, kama serikali inashindwa kusimamia sector zake, suluhu ni kubinafsisha?, Sio muda mrefu atabinafsisha hadi ikulu.
 
Mama Samia na Mbarawa wanamiliki hata Apartment au nyumba za kupangisha? Je walishawahi kuwa wapangaji wakajua mikataba ya upangishaji inakuwaje? Binafsi naamini hawana.

Hata biashara hawajui. Mama Samia alisema wana kamedia house kanaitwa Suluhu Media na kanamshinda. Sasa watu hawa unawapaje dhamana kubwa namna hii ya kupangisha bandari zote?

Tunajimaliza wenyewe
 
Hakuna mwanamchi ambaye hapendi maendeleo hilo mlielewe , Ila hofu ya wananchi hasa watanganyika ni huu mkataba DP World ni wakijanja janja , yaani ni ile ile staili ya mtego wa kumkamata panya , unaweka nyama nono kwenye kandoano cha ule mtego wa kukaba shingo, hatutaki kukabwa shingo kwa miaka hiyo ambayo haijulikani , ni 99, ni milele , yaani ni mtego.

Watanganyika wamechoka kuibiwa na kugeuzwa vichwa vya mwendawazimu , Hao DP WORLD Kama ni wenye nia nzuri Basi wasitukabe kihivyo , walekebishe Yale masharti ambayo watanganyika wanayaona ni mtego kwao .

JPEG_20230622_095812_5019593035534662413.jpg
 
"Wamemuungiza mkenge Rais nae kaingia mzima mzima" Tundu Lissu #MkutanoKariakoo

"Anayetetea mkataba wa bandari jua kwamba hana akili au faranga imetembea" Tundu Lissu#MkutanoKariakoo

"Marais uwa hawasaini mikataba ila huu Rais kasaini kumpa mamlaka yake Waziri,Rais anachomokaje" Tundu Lissu #MkutanoKariakoo
 
Tutamlilia mungu na atatusikia.
1. Loliondo
2. Ngorongoro
3. Bandari
4. Misitu
5. Posta
etc etc vingi tusivyojua
 
Back
Top Bottom