Hakuna mtu makini kwa sasa kuliko Lissu.
Nawe jaribu kujiongeza kidogo, swala hili la Bandari limeongelewa sana humu JF na nje ya hapo. Itakuwia vipi vigumu kutambua hadi sasa kwamba Bandari za Zanzibar hazihusiki? Hujui kuwa anayesimamia bandari Zanzibar ni Zanzibar Ports Corporation,(ZPC) na siyo Tanzania Ports Authority (TPA)?
Kiufupi ni kwamba Samia katika jambo hili anafanya hila za maksudi kabisa kunadi mali za Tanganyika, huku akiwatumia waZanzibar wenzake, huyo Mbarawa na Katibu Mkuu wa Wizara.
Watu hawawezi kupuuza hitimisho la namna hiyo, hasa kutokana na ulaghai mwingi unaoonekana kufanyika kufanikisha jambo hili.
Lakini jambo linaloshangaza hasa ni huyu Samia ujasiri huu wote anautoa wapi? Sidhani kuwa, pamoja na kuwa Rais wa nchi, angeweza kufikia uamzi wa namna hii yeye pekee bila ya kuwahusisha baadhi ya waTanganyika wenye nyadhifa kubwa, au waliowahi kushika madaraka makubwa ndani ya nchi hii.
Nakataa kabisa kabisa, kwamba hii siyo kazi ya Samia na vidagaa vidogovidogo, kama akina Msukuma. Hii ni kazi ya Mapapa haswa. Sasa tunawaona hata akina Roast wakijitokeza kutetea ujinga huu.