Hivi kwa nini hutaki kuelewa.
Maana ya kuwepo kwa IGA ni nini?
Kuna sababu zipi zinazolazimisha kupoteza muda wa wabunge, na hata kuwahonga pesa na wengine kutishiwa kabisa wasithubutu kupinga hiyo IGA?
Hivi akili unaziweka wapi wewe unapoandika haya unayoweka humu kutetea ujinga?
Na kwa bahati mbaya kabisa, unazo akili za kutambua na Kuuita huo "MKATABA MAMA", lakini bado huoni umuhimu wake?
Tunaiita Katba ya nchi" kuwa ni sheria MAMA", sheria zote zinachimbuka tokana na Katiba hiyo, sasa wewe leo hii, wewe unaona unaweza kutunga sheria amabazo zitakinzana na Sheria Mama"?
Nimejadili na wewe vya kutosha, na inanilazimu niseme yafuatayo kukuhusu wewe, kama wewe:
Ninakuona kuwa ni mtu mwenye busara ya kutosha, asiyechafukwa na akili kwa haraka na kupoteza fahamu (kwa sababu nimekuchokoza maksudi mapema sana, lakini ulibakia kuwa na fahamu zako).
Bila shaka wewe ni mfanya kazi, aliye karibu sana na hili swala la Bandari. Mmepewa majukumu ya utetezi wa jambo bovu kabisa kwa nchi yetu.
Swala la 'uzalendo' uliloliongelea mapema sana, ninakuona kwamba pengine binafsi, wewe halikugusi kwa karibu sana, kutokana na majukumu uliyo nayo na kuyatekeleza, au unufaikaji binafsi unaoupata kutokana na mkataba kama huu.
Ninakuomba sana, wewe kama mTanzania, uweke mbele zaidi maslahi ya nchi yako na maskini wa nchi hii.
Kazi za bandari hazina 'rocket' sayansi yoyote. Hao DP World hawakuzaliwa wakijua kila kitu, na kwamba hata hiyo teknologia wanayotumia sasa siyo wao pekee wenye uwezo nayo. Hata kama inatulazimu kuwaweka hapo watufanyie kazi kwa ubora, ni jukumu letu, kwamba kazi hizo tutazimudu wenyewe katika muda maalum, isiwe zaidi ya miaka 20 tena kama tulivyofanya na TICTS.
Kama taifa, ni lazima tuwe na mpango wa kujitegemea kufanya mambo mengi yanayotuhusu wenyewe. Tusijiweke waziwazi namna hii tunavyofanya sasa kuwa wategemezi kwa watu wengine milele..
Hayo ni baadhi ya maoni yangu tu kwa kifupi kwako, bila kujali maslahi unayoyapigania sasa hivi katika jambo hili linaloendelea.