Dah!Wapumbavu ni nyinyi mnaoeleweshwa halafu hamuelewi chochote. Kujiunga humu miaka mingi iliyopita sio wingi wa akili au busara.
Tundu Lissu ni CHADEMA, walioamua kuikomoa bandari ya Tanzania kwa siasa nyepesi za ujira mdogo unaokwisha kesho tu.
Hizi ndio 'talking points' mulizopewa hivi karibuni mkapige propaganda?
Mbona ni pointi mfilisi kabisa.
Hizi labda mzilenge kwa watu wasiokuwa na upeo kabisa wa haya maswala ya mahusiano.
Samia alipokubaliana na Uhuru, halafu baadae na Ruto kupeleka bpmba la gesi kuwanufaisha hao majirani ambao sasa ndio wanaotupiga vita, hata kabla ya huyu Samia kufikiria kuwanufaisha waTanzania na hiyo gesi yao, bila shaka wewe ulikuwa hujazaliwa, au siyo?
Hizi propaganda zilizochoka sana za "vita vya kiuchumi" tafuta wajinga wa kuwapelekea ujinga huo.
Jirani huyo huyo, unaruhusu aingie na malori yake hadi shambani kwa mkulima wako, na kuzoa mazao yote, akihatarisha usalama wa nchi yako; hukuona vita hiyo ya kiuchumi, hadi alipokuja Mwarabu na tende na kashata ndiyo ukaona vita?
Tafuta wajinga wengine wa kuwauzia upuuzi huo unaoutembeza sasa hivi. Usiulete kwa Kalamu.