Pre GE2025 Tundu Lissu: Tuna upungufu wa kutisha wa fedha kwa ajili ya shughuli za Chama (CHADEMA), msiniulize nimekuta nini, jibu halitakuwa zuri!

Pre GE2025 Tundu Lissu: Tuna upungufu wa kutisha wa fedha kwa ajili ya shughuli za Chama (CHADEMA), msiniulize nimekuta nini, jibu halitakuwa zuri!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Walienda expensive retreat ?

Nooooway😂.
walienda kujipongeza bagamoyo kwa zaid ya siku4 wanaogelea tu kwenye swimming pools za hotel ya kifahari sana, eti ndiyo ilikua retreat ya viongozi wapya dah,

wamerudi , eti saivi account inasoma zero balance na wananchi wamegoma kutapeliwa kwa michango 🐒
 
JPM na Lissu wanatabia za kufanana.

Sema mmoja aliaamini katika matendo na matokeo yanayoonekana.

Mwinginwe anaamini katika maneno.
Kutwa nzima tuongee na kupiga domo.
Serikali ya awamu ya 4 na ya 6 zinafanana sana. WIZI ,UFISADI WA KUTISHA na UNDUGU/USHKAJI.
 
Yeye afanye kazi aache siasa za kulalamika,kama hakuna hela aseme chama hakina hela wanachama watachanga na siyo kulalamika kwamba hakukuta kitu wakati anajuwa fika Mwenyekiti mstaafu ndiyo alikuwa mfadhili wa Chama.
Ruzuku, ada za wanachama na michango mingineyo zilikuwa zinaenda wapi!? Kifupi Lissu kaamua kumstahi mwizi.
 
Tuko radhi kuchangia fedha mhe. Mwenyekiti 🙏🏿
 
Tunajifunza kitu hapa, "usione vyaelea kaka, tabia ya kutamani tamani vitu hii mbaya Sana"
#chama kinamfia mchana peupe!
Ashakum si matusi ,ukitamanitamani hovyo bila kuzitengeneza basi UTACHAPWA nao....vijana wa Lamu na Bamburi wanayajua hayo vyema tu.....

Lissu ni trilionea wa domo hekaya tu.....
 
miaka 5 iliyopita mh.Katibu Mkuu wa. cHADEMA ndg.John Mnyika amesema kuwa walipata RUZUKU bilioni 12.5....yaani hizi zote zilitumika na kuisha ?!!!

Hati safi ya mahesabu ikatolewa na CAG (Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Umma kama ruzuku ), naye bila hiyana chini ya awamu ya 5 ya Magufuli na awamu ya sasa ya sita ya utawala wa rais Samia Hassan, CAG pamoja na kuelekezwa lakini ikawa vigumu na hivyo kwa haki kabisa kutoa hati hizo mwaka hadi mwaka bila kuweka angalizo lolote.


Pia Msajili wa Vyama Vingi Vya Siasa pamoja na kupekua vipengele vya kisheria, kanuni na maagizo lakini hakuona aina yoyote ya kuweza kukibana chama cha CHADEMA kwa kuwa mambo yote yameendeshwa kwa mujibu wa katiba na utaratibu wa chama.

TAKUKURU nao kwa kutumia njia zao za medani hawakuweza kuona dosari yoyote ya matumizi mabaya ya ofisi za chama kikuu CHADEMA ili kupunguza makali ya ushindani dhidi ya Chama Dola Kongwe Tawala CCM.

Uongozi mpya ulioingia sasa inabidi kuwa wabunifu wa kuhamashisha wanachama wengi wajiunge na pia kuwaondoa wafadhili hofu kwamba wanaweza kuichagia CHADEMA michango, donation, charity, matembezi ya kukusanya fedha n.k bila ya kuongopa serikali ya CCM na vyombo vyake kuwasumbua wafadhili wawe wafanyabiashara, matajiri n.k

Hilo la kuwahamasisha watanzania wote, wa madaraja yote ndilo jambo kuu uongozi mpya ndani ya CHADEMA inatakiwa walifanyie kazi kwa haraka sana ili kupata rasilimali fedha.
 
Aache kutupigia makelele yake hapa. Naye atafute pesa zake za kuendeshea chama. Si aliona ni rahisi kuendesha chama? Hafahamu kuwa Mwamba alikuwa amejitoa na kujitolea kwa hali na mali kwa ajili ya CHADEMA? Na bado ipo siku atasema chama kimemshinda kukiendesha. Nipo pale 👉nimekaa naangalia mwisho wake
Lisu msema kweli dunia itachanga pesa ku run shughuli za kilq siku
 
Back
Top Bottom