Pre GE2025 Tundu Lissu: Tuna upungufu wa kutisha wa fedha kwa ajili ya shughuli za Chama (CHADEMA), msiniulize nimekuta nini, jibu halitakuwa zuri!

Pre GE2025 Tundu Lissu: Tuna upungufu wa kutisha wa fedha kwa ajili ya shughuli za Chama (CHADEMA), msiniulize nimekuta nini, jibu halitakuwa zuri!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hati safi ya mahesabu ikatolewa na CAG na kutoa hati hizo mwaka hadi mwaka bila kuweka angalizo lolote.


Pia Msajili wa Vyama Vingi Vya Siasa hakuona aina yoyote ya kuweza kukibana chama cha CHADEMA kwa kuwa mambo yote yameendeshwa kwa mujibu wa katiba na utaratibu wa chama.
Point....

Kwa hiyo mh.Tundu Lissu anaudanganya UMMA....

Kweli ndugu Lissu amefurutu ada.....
 
Aache kutupigia makelele yake hapa. Naye atafute pesa zake za kuendeshea chama. Si aliona ni rahisi kuendesha chama? Hafahamu kuwa Mwamba alikuwa amejitoa na kujitolea kwa hali na mali kwa ajili ya CHADEMA? Na bado ipo siku atasema chama kimemshinda kukiendesha. Nipo pale 👉nimekaa naangalia mwisho wake
we ulitakaje hovyoo sana ww
 
JPM na Lissu wanatabia za kufanana.

Sema mmoja aliaamini katika matendo na matokeo yanayoonekana.

Mwinginwe anaamini katika maneno.
Kutwa nzima tuongee na kupiga domo.
Ilitakiwa yeyote kati yao awe President na anayebaki awe PM, nchi ingekuwa poa sana
 
Na alisena yeye kama makamu mwenyekiti kuwa Chadema pesa ziko nyingi zinaishia kuliwa makao makuu hazifiki matawini

Akasema akishika atahakikisha hizo pesa zinafika matawini.Azifikishe sasa

Ulaghai una mwisho kampaka matope Mbowe weeee

Atakayechanga atakuwa akili hana aambiwe alizosema zipo ashushe matawi
Kwa maelezo haya inaonesha shida ni elimu hukumuelewa lisu na hutakaa umuelewe
 
Yeye afanye kazi aache siasa za kulalamika,kama hakuna hela aseme chama hakina hela wanachama watachanga na siyo kulalamika kwamba hakukuta kitu wakati anajuwa fika Mwenyekiti mstaafu ndiyo alikuwa mfadhili wa Chama.
Mwenyekiti mstaafu alivyoondoka ofisini akaondoka na hela zake !
Mimi nawaambia ukisikia Lisu anang'ang'ania anataka kuongea na mh Rais anataka kwenda kuomba hela! Sasa tangu awe mwenyekiti mama Samia kampotezea sasa kaona atoke kwa wananchi na kuwaambia ukweli "CHAMA HAKINA HELA!"
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Tuko radhi kuchangia fedha mhe. Mwenyekiti 🙏🏿
....wale mangi wa kariakoo wamesema hamtokuwa nao katika huko kushajiishana michango kwa mwenyekiti "wasiyemuamini kuwa mtekelezaji wa malengo makubwa ya kuanzishwa kwa CHADEMA na mzee Mtei...."
 
....wale mangi wa kariakoo wamesema hamtokuwa nao katika huko kushajiishana michango kwa mwenyekiti "wasiyemuamini kuwa mtekelezaji wa malengo makubwa ya kuanzishwa kwa CHADEMA na mzee Mtei...."
CHADEMA ina wanachama mamilioni tukichanga jero jero tu inatosha.
 
Msiniulize Mwenyekiti umekuta nini huko ulipoingia kwasababu sitajibu na sitajibu kwasababu jibu halitakuwa zuri
Ujanja na utapeli wa Lisu unaanzia hapa
Sasa kama watu hawaambii kakuta kiasi gani ili wajue kuna upungufu kiasi gani ili wachangie

Sasa kusema tu anachangisha bila watu kujua kilichopo na upungufu huo ni utapeli
Aeleze tu
 
Ujanja na utapeli wa Lisu unaanzia hapa
Sasa kama watu hawaambii kakuta kiasi gani ili wajue kuna upungufu kiasi gani ili wachangie

Sasa kusema tu anachangisha bila watu kujua kilichopo na upungufu huo ni utapeli
Aeleze tu
Huyo ni bwana DOMOKAYA tu...
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Hizo ni Propaganda tu,CHADEMA tutaichangia mpunga.
Wewe ni mtu smart na sitegemei ukaipuuza hoja kwa kuwa nimeitoa mimi UVCCM...

Mkuu fanya "analysis" yako pale Kariakoo.....utawajua wale Mangi ambao wamegoma kuendelea kukichangia chama chenu......
 
Back
Top Bottom