miaka 5 iliyopita mh.Katibu Mkuu wa. cHADEMA ndg.John Mnyika amesema kuwa walipata RUZUKU bilioni 12.5....yaani hizi zote zilitumika na kuisha ?!!!
Hati safi ya mahesabu ikatolewa na CAG (Mkaguzi Mkuu wa Fedha za Umma kama ruzuku ), naye bila hiyana chini ya awamu ya 5 ya Magufuli na awamu ya sasa ya sita ya utawala wa rais Samia Hassan, CAG pamoja na kuelekezwa lakini ikawa vigumu na hivyo kwa haki kabisa kutoa hati hizo mwaka hadi mwaka bila kuweka angalizo lolote.
Pia Msajili wa Vyama Vingi Vya Siasa pamoja na kupekua vipengele vya kisheria, kanuni na maagizo lakini hakuona aina yoyote ya kuweza kukibana chama cha CHADEMA kwa kuwa mambo yote yameendeshwa kwa mujibu wa katiba na utaratibu wa chama.
TAKUKURU nao kwa kutumia njia zao za medani hawakuweza kuona dosari yoyote ya matumizi mabaya ya ofisi za chama kikuu CHADEMA ili kupunguza makali ya ushindani dhidi ya Chama Dola Kongwe Tawala CCM.
Uongozi mpya ulioingia sasa inabidi kuwa wabunifu wa kuhamashisha wanachama wengi wajiunge na pia kuwaondoa wafadhili hofu kwamba wanaweza kuichagia CHADEMA michango, donation, charity, matembezi ya kukusanya fedha n.k bila ya kuongopa serikali ya CCM na vyombo vyake kuwasumbua wafadhili wawe wafanyabiashara, matajiri n.k
Hilo la kuwahamasisha watanzania wote, wa madaraja yote ndilo jambo kuu uongozi mpya ndani ya CHADEMA inatakiwa walifanyie kazi kwa haraka sana ili kupata rasilimali fedha.