Tunduma: Wakuu wa shule wavuliwa nyadhifa kisa wimbo wa Zuchu (Honey)

Aisee nilidhani unatania kumbe kweli bhana, tena mwanzoni tu mwa video.. nchi ngumu sana hii..
Acha tu, nilibaki mdomo wazi wakati naangalia hicho kipande uzuri nilikua peke yangu.... halafu bora kingekua kifupi ila wameweka scene nzima ya verse ya Mbosso iwe hivyo
 
Hao walimu ilitakiwa wachapwe na viboko unaachaje watoto wakate vibuno
 
Huo ni uonevu.. matumizi mabaya ya madaraka....
Warudishe hao walimu
 
Mbona kwenye mbio za mwenge walimu hao hao huwakusanya wanafunzi na kuomba mapambio ya kusifu CCM, lakini hamuwachukulii hatua?
 
Huyu prof nae kichwani sifuri kabisa. Ukiangalia ule wimbo watoto walikua wanaimba kwa ufasaha kabisa sasa swali ni Je! hao walimu ndio waliwakalilisha huo wimbo? NO.. Kwahiyo prof kama angekua na akili angeshajua wapi pa kuanzia na sio kufukuza kazi wazazi wenzie ambao wanatumikia nchi kwa mishahara midogo na wana familia zinawategemea.
 
Unamsema zuchu Maudhui yake wakati anayoyaimba ndio unayoyafanya.. unafiki mkubwa
Nafikiri wewe ndio Mnafiki siujui Huo wimbo ndio kwanza nimeona kwenye hiyo clip.Usifikiri humu Kuna wapuuzi wenzio wanaosikiliza hizo takataka.Kwa Tanzania nyimbo nazosikiliza ni Gospel tu hakuna Cha zaidi.
 
Nimekuelewa sana,hawa batata sijui wapo kwa ajiri gn? Kuna upumbavu mwingi sana unafanyika kwenye nchi hii,lkn mamlaka zipo kimya kbs.
 
[emoji1360]
 

Kabisa nimebidi kwenda kuutazama, nakubaliana na wewe zile scene hazifai kbs. Zinahamasisha kuwafanyia ubaya wanawake kwa kisingizio kisicho na mantiki.
 
Hakuna sababu yoyote ya MSINGI inayoweza kukubalika ya KUWASHUSHA VYEO, tuache tabia za viongozi wa juu kujiona wao HAWAKOSEI .

Waalimu hao kuwapigia simu na kuwaonya INATOSHA KABISA. mambo mangapi MAGUMU wanayopambana nayo katika mazingira yao ya KAZI lkn kwa dhiki iliyogubikwa na UZALENDO KWA TAIFA LAO wanapambana bila ma ung'uniko.

Kwa HESHIMA NA TAADHIMA walimu hao WASAMEHEWE waliamini wanawasahaulisha wanafunzi wao shida walizonazo.
 
Madaraka ya kulevya🤣🤣🤣🤣🤣🪑💺
 
Zuchu sijui Chuchu ni mwanaccm wameshindwa kufungia wimbo wake wanaenda kuwavua walimu vyeo.

Mbona kuna majizi ya pesa za umma hayavuliwi vyeo ndio kwanza yanaitwa waheshimiwa.
 
Huyu profesa kichwani ni sifuri kama baadhi ya members JF.

I don't want peace[emoji3577], I want a problems.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…