Mabonde ya Maji nchi hii practically hayaelewiki kazi yao ni nini. Kiuhalisia ndio walitakiwa watunze/ wahifadhi vyanzo vya maji lakini wao wamekuwa wanaangalia upande wa biashara- kuuza vibali vya matumizi ya maji pamoja na vibali vya ruhusu ya kuruhusu maji yaliyotumika kurudi kwenye mfumo " discharge permits". Ukweli wa mambo ni kuwa kazi ya uhifadhi inafanyika kidogo sana kwa kuweka tu mabango, na elimu kidogo, na inakuwa haina tangible results. Matokeo yake ndiyo haya tunayoona leo. Kwa hiyo ni afadhali kufanya haya haraka.
1. Mabonde yote yavunje kisheria na kazi yake ifanyike na halmashauri za wilaya , manispaa na majiji
2. Watu wa mali asili ya halmashauri, manispaa na majiji wapimwe utendaji wao kwa jinsi wanavyoweza kuhifadhi vyanzo vya maji
3. Kazi ya kutoa vibali vyote ambavyo vilikuwa vinatolewa na mabonde ya maji vitolewe na halmashauri husika
4. Ofisi zote za mabonde husika zichukuliwe pale zilipo na halmashauri husika