Minja Ngalason
JF-Expert Member
- Jan 8, 2017
- 1,284
- 1,839
ni kweli hakikaJambo lililo jema zaidi ni kutowasahau na Watanzania wengine wasio na majina/ maarufu.
Au wao sawa tu wakiachwa wajigharamie matibabu yao wenyewe?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ni kweli hakikaJambo lililo jema zaidi ni kutowasahau na Watanzania wengine wasio na majina/ maarufu.
Au wao sawa tu wakiachwa wajigharamie matibabu yao wenyewe?
Aliyenacho huongezewa, na asiyekuwa nacho hunyang'anywa hata kile kidogo alichonacho. Kumbuka kuwa huyu nae ni mfaidika wa kiinua mgongo cha Tshs. 200m+ alichopata mwishoni mwa 2020.hii sio sawa, anatibiwa kama nani..
gharama za wagonjwa wengine hapo muhimbili wasio na mbele wala nyuma nazo Serikali itazibeba? tuwe serious kidogo.
Kwani alifanya bure, alilipwa zaidi ya bilioni moja kwa kazi hiyo ukijumlisha mishahara,posho za vikao,marupurupu pamoja na pension.HuYu alikuwa Kiongozi na mwakilishi Rasmi wa Wananchi kwa miaka 5. Alifanya Mengi kwa maendeleo ya Wananchi wa Jimbo lake.(Mbunge).
Nadhani gharama zinatakiwa kulipwa na NHIF kwa kuwa ulikwisha changia kwa miaka kadhaa iliyopita.
Mbunge lisu hakutibiwa ndio useme mbunge mstaafu anatibiwa acheni kutetea matumizi ya hovyo ya fedha za umma ndio maana inahitajika katiba mpya haiwezekani rais ajikurupukie tu aseme fedha za serikali zitumike kumtibu mr flani.Anatibiwa kama Mbuge mstaafu we kama hutaki andamana!
Umeambiwa bure au kusaidiwa kama Prof J?? hakuna watu wanasaidiwa na serikali kwenye matibabu??Wewe uo usingizini? Toka lini kutibiwa kansa ikawa bure?
Inshallahpole sana, InshaAllah, Mungu atakufanyia wepesi...
Nadhan suluhisho ni bima kwa wote, kama ilivyowahi kufikiriwa iwe namna hyo, pengine inaweza kuwa na uhafadhali.Hii ni aibu pia kwa serikali, maana ikiwa mtu kama Prof jay matibabu inakua ngumu kuyamudu. Vipi kwa wale maelfu ambao hata buku mbili tu ya kula hawana uhakika?
Siyo huruma prof alikuwa mtu safi sana Hana siasa za maji takaChadema wala familia ya J haikushindwa kumtibu mtu wao , Kujichomeka kwa serikali ili ipate huruma ya wananchi kusikupumbaze .
Tumenyamaza kwa sababu maalum
Hizi ni roho mbaya.Jay anapaswa kusaidiwa ikiwa kakwama, Ila wanachohoji hao pia kina mantiki kwa maana Kuna maelfu ya watu ambao wamekufa kutokana na kushindwa kumudu gharama za matibabu.
Kusema tusubiri apone ndio raisi aambiwe, nadhani huu ni ujinga.
Ina maana raisi hajui watanzania wengi hawawezi kumudu matibabu?
Endeleeni michango ili mkawalipie hao wengine hili la Prof. Jay mama yetu kipenzi amelibeba.Kwani serikali haijui kuna hao 'wengine' wakikata roho kila kukicha hapo hapo Muhimbili (na kwengineko) huku wakikosa hata 10k ya matibabu ?
Wewe uko wapi ?Upo sahihi, lakini vipi kwa wale wasio na uwezo hata wa kulipa elfu 10 kumuona daktari? Wao wanasaidiwa na nani?
Serikali imetumia busara kubwa sana .Maneno Makali sana lakini nakuhakikishia ungepewa hiyo wizara usingeweza kuiendesha hata miezi miwili . Maamuzi yake ni sahihi sana na zipo sababu zilizofanya seeikali Kuingilia hili Suala. Utakakatishaji fedha una njia nyingi sana na fedha za kufanya Uhalifu zina njia nyingi. Serikali ina macho kama imeshaamua kuingilia hili Suala wananchi tukae kimya tufanye mambo mengine mf. Kuhudumia familia yake n.k
Kumbuka kuna maskini wanakufa kwa kushindwa kulipia huduma ya matibabu.Watanzania hatuna jema kwa kweli, kama hadi hili la Prof J kusaidiwa inakuwa nongwa?
Wangemlipia kimya kimya matapeli wangeendea kupitisha michango na kuwaibia watu bila huruma.Ukisikia ule msemo wenye akili hawana power na wenye power hawana akili ndio hiii.
Hivi Serikali inawezaje kutoa statement kama hiyo mbele ya jamii-bora wangemlipia kimya kimya.
Tuna viongozi ambao hawatumii akili kabisa,by the way sisi Wananchi ndio matahira kabisa -acha mambo yaende.