Ummy Mwalimu: Kuanzia sasa matibabu ya Joseph Haule(Prof. Jay) yatagharamiwa na Serikali
Baba angu mdogo ali survive long 2010 mpk sep 2020

Kutokana na experiences ya kukaa nae na kufanya nae interview...ni seme wazi wagonjwa wa figo Tz plus umaskini wanapitia jehanamu wakiwa hai...

All in all bado tuna safari ndefuu sanaa ya kuwashinda maadui wetu watatu ambao tumeaninishwa tangu Uhuru.....UJINGA, UMASKINI NA MARADHI
 
Wewe mtu upo Tanzania hii kweli? Mtu mwenye shida ya matibabu akamuone diwani atasaidiwa?
Upo humuhumu Tanzania au?
Ni kweli hujui Kuna watu wengi wanakufa kwa kushindwa kumudu gharama?
Kuna program ya ustawi wa jamii kila hospitali na kama hujui nusu ya mapata ya hospitali nyingi za serikali zina enda kwenye misamaa na serikali hulipa
 
Wewe mtu upo Tanzania hii kweli? Mtu mwenye shida ya matibabu akamuone diwani atasaidiwa?
Upo humuhumu Tanzania au?
Ni kweli hujui Kuna watu wengi wanakufa kwa kushindwa kumudu gharama?
Hujajua ni Kwa Nini nimekuambia hivyo?
Kama wakati wa uchaguzi watu wanahongea khanga ,t-shirt na Elfu kumi kumi Kwa Nini wakikosa Elfu kumi ya Matibabu wasiende Kwa waliowachagua Kwa Hela?

Uzalendo ni vitendo.
Haki , Utu, usawa na maendeleo ya watu ni jambo la msingi.
 
ni hivi kwanza hakuna cheo cha mbunge mstaafu.
Pili kuna wahitaji wengi sana ambao wangeitaji kusaidiwa na serikali tena wao mahitaji yao ni makubwa kulipo huyo mtu ambaye wa miaka 5 2015-2020 aliuwa mbunge na aliingiza kipato cha zaidi ya bilion 1.wa kipindi hicho
kuna watu maskini wanahangaika kwa ajili ya kukosa fedha za matibabu hao ndio seriali ingetakiwa iwasaidie.
Hata sisi waroma tuna sala yetu tunapomuomba Mungu tunamwombia awasiadie kwanza "wenye mahitaji zaidi kulipo sisi"
Neno Mbunge Mstaafu ni neno TU la kumtaja mtu kiuungwana. Haiongezi Wala haipunguzi kitu.
Hao wahitaji wengi hata kule kwenye Hospitali za Kanisa la warumi wanalipa fedha nyingi japo hizo Hospitali zimejengwa Kwa Sadaka na Kodi za watu ulaya na Afrika. Kwa Hiyo rumi na Sala zao achana nazo kabisa wameitawala Dunia tangu Enzi za Kristo lakini ni ubinafsi na roho mbaya TU.

Ni wabinafsi sana wanajipendelea sana. Hawataki wengine wapate, wao TU na ajira na kushika utawala kila mahali.
Wanasema midomoni lakini mioyoni ni dubu Wala watu.

Kuna watu ni waumini lakini ni kama wafuasi wa Yuda Iskari Ote aliyechukizwa kuona Bwana Yesu Kristo Mwana wa Mungu anapakwa mafuta ya thamani kubwa wakati Kuna maskini( Mawazo ya watu wenye roho mbaya za kutamka maneno mazuri midomoni mioyoni wakiwa na sumu Kali kama ya joka la mdimu).

Bwana Yesu alimweleza ukweli bila kuficha," Maskini mnao siku zo yate." Akiwa na maana kuwa wao pia hajakatazwa kuwasaidia Kwa wakati wao. Kwa Sasa serikali imeenda na habari iliyopamba vinywa na Maskio ya watu . Habari ya ugonjwa na gharama zake Kwa Prof. Jay. Hata waliokua wanamchangia hawakukatazwa kuwachangia wahitaji wengine? Na Kwa Nini siku zote wasiwachangie wahitaji hao badala yake wakaanza kumchangia Prof .Jay.
 
Ina maana kama wananchi hawangechanga wasingemtibu

Vipi pesa za matumizi na dawa ambazo muhimbili hakuna ?

Wale malatibu wa ccm wameona hiyo ni siasa ?
 
Neno Mbunge Mstaafu ni neno TU la kumtaja mtu kiuungwana. Haiongezi Wala haipunguzi kitu.
Hao wahitaji wengi hata kule kwenye Hospitali za Kanisa la warumi wanalipa fedha nyingi japo hizo Hospitali zimejengwa Kwa Sadaka na Kodi za
Ni upotoshaji tu na upumbavu hakuna kitu kinachoitwa mbunge mstaafu , Mbunge hastaafu labda hujui maana ya neno mstaafu.
Umeandika maneno mengi ambayo hayana maana ila ukweli kuna wagonjwa kibao wahitaji ambao wanateseka sana kwenye hospitali za serikali, kuna watu wengi maskini wametibiwa kwenye hospitali za serikali ila wamezuiliwa kuondoka hadi walipe bili nyingine ndogo tu haizidi hata laki 5, kunawatu wanazuiliwa kuchukua wapendwa wao waliofariki hospitali za serikali hao ndio wangestahili kusaidiwa na serikali
 
Michango isitishwe sasa
Maana kwenye vimedia uchwara
Naona watangazaji washaanza...
Kuwaomba watu watoe hela

Ova
Lakini hao hao uchwara ndiyo waliolileta nje tukalifahamu usiwaite uchwara
 
Wamemchangia shiling ngapi, kama mtu kapata bahati hiyo yakutibiwa mwacheni MUNGU alipanga hivyo sio kutoka mapovu
mkuu ni dhana potofu kuacha fedha za serikali zitumike kwa mtindo wa bahati,fedha za serikali ni fedha za umma zinatakiwa zitumike kwa kufata taratibu rasmi hususani kwenye suala la matibabu, kuna wahitaji wengi sana tena wengine ni watu masikini sana embu tuacheni mzaha na matumizi ya fedha za umma
 
Ummy,

Kwanza kabisa umefanya jambo la maana sana kughramikia matibabu ya Prof lakini labda tu nikwambie umeyasema hayo ktk wakati usio sahihi hata kidogo.

Profesa hana shida kiuchumi hivyo acheni kabisa kuingiza siasa ktk masuala ya msingi. Kuna watu wengi hasa kule Ikungi, Lyankoma, Simiyu wanahitaji matibabu na hawana usaidizi eti leo mnakuja hapa kutuambia kwamba mmeona mgharamikie kupunguza ugumu wa maisha kwa Profesa. Narudia acheni kucheza na maisha ya watanzania kisiasa.

Kama kumsaidia, anzeni kusaidia watu wasio na uwezo na wana magonjwa makubwa makubwa ila hawa wenye uwezo na profle mkitaka kufanya fanyeni kimya kimya. CCM mnakwama sana acheni siasa ktk masha ya watanzania.

Nimemaliza, naamini ujumbe utaupata dk hii hii.
Mkiona zinanunuliwa ndege kwa wingi mjue lengo ni kuongeza mzunguko wa biashara ili kodi ipatikane kwa wingi. Kupatikana kwa kodi kunaongeza uwezo wa serikali kuhudumia wananchi wake.

Hizi pingapinga zinaikwamisha serikali na kukwamisha wananchi wanaofikiwa na mzunguko wa pesa unaosababishwa na ongezeko la kodi.

Ni wazo zuri kila mtu kupata matibabu kwa gharama sawa na bure lakini wakati uwezo haujaweza kufikiwa cha maana kufanyika ni kuunga mkono mipango ya muda mfupi na mrefu kwa lengo la kubadilisha maisha ya mtanzania wa kawaida.
 
Tumuombee apone salama, nyimbo ni kiashiria cha yajayo
 

Attachments

  • VID-20220212-WA0041.mp4
    502.9 KB
Mkiona zinanunuliwa ndege kwa wingi mjue lengo ni kuongeza mzunguko wa biashara ili kodi ipatikane kwa wingi. Kupatikana kwa kodi kunaongeza uwezo wa serikali kuhudumia wananchi wake.

Hizi pingapinga zinaikwamisha serikali na kukwamisha wananchi wanaofikiwa na mzunguko wa pesa unaosababishwa na ongezeko la kodi.

Ni wazo zuri kila mtu kupata matibabu kwa gharama sawa na bure lakini wakati uwezo haujaweza kufikiwa cha maana kufanyika ni kuunga mkono mipango ya muda mfupi na mrefu kwa lengo la kubadilisha maisha ya mtanzania wa kawaida.
Trekta zinaongeza sana tena kwa haraka zaidi mzunguko mkubwa Sana wa fedha nchini kuliko ndege.Trekta zingesharudisha pesa yote ndege hata robo tu bado kimbembe
 
Na Watanzania wengine walio wagonjwa watagharamiwa na nani?

Kwanza kwa nini agharamiwe na serikali? Ni mtumishi wa serikali kwani?

Ni bora tu wangeacha watu wamchangie na wao kama wanataka kumsaidia, basi wangechanga tu kama watu binafsi.
Point.
 
Watanzania hatuna jema kwa kweli, kama hadi hili la Prof J kusaidiwa inakuwa nongwa?
Hilo sio tatizo, tatizo wengine je? Hii serikali yenyewe inajichimbia shimo, ni vigezo gani Waziri ametumia? Haya mambo ya kukurupuka bila kuwa na sheria madhubuti yanaligharimu taifa. Why them and not others? Shame on them.
 
Back
Top Bottom