Ummy,
Kwanza kabisa umefanya jambo la maana sana kughramikia matibabu ya Prof lakini labda tu nikwambie umeyasema hayo ktk wakati usio sahihi hata kidogo.
Profesa hana shida kiuchumi hivyo acheni kabisa kuingiza siasa ktk masuala ya msingi. Kuna watu wengi hasa kule Ikungi, Lyankoma, Simiyu wanahitaji matibabu na hawana usaidizi eti leo mnakuja hapa kutuambia kwamba mmeona mgharamikie kupunguza ugumu wa maisha kwa Profesa. Narudia acheni kucheza na maisha ya watanzania kisiasa.
Kama kumsaidia, anzeni kusaidia watu wasio na uwezo na wana magonjwa makubwa makubwa ila hawa wenye uwezo na profle mkitaka kufanya fanyeni kimya kimya. CCM mnakwama sana acheni siasa ktk masha ya watanzania.
Nimemaliza, naamini ujumbe utaupata dk hii hii.