Kwa hiyo baada ya serikali kukabwa koo awali baada ya kuonekana mkataba huo hauna ukomo ndio sasa ukomo umewekwa wa miaka thelathini na uhakiki wa tathimini ni kila baada ya miaka mitano, hapo sawa ila miaka thelathini ni mingi sana, ni umri wa mtu mziama na pia ni mihula ya maraisi watatu wataendelea kuvumilia mkataba huo. Tathimini ya miaka mitano ni muhula mmoja wa rais kuwa madarakani anaweza akafunika kombe mwanaharamu apite bila kufanya tathimini mpaka anamaliza mihula yake miwili. Je rais atakayefuata atakuwa na jeuri ya kuuchungulia mkataba kuona kama una tija na kama hauna tija auvunje?
 
Nimesikia kuwa maoni yote yaliyotokewa yamezingatiwa, maslahi mapana ya Taifa yamepewa kipaumbele, na ni mikataba mitatu ya awali...
Ukweli au uongo ni jambo jingine.
 
Kuna watu wanafoka, povu linawatoka mpaka wanaanza kututukania Uislam wetu.
wanawatukania uislam wenu kwasababu ninyi mlikuja kwa mgongo wa uislam kutetea waarabu, Rais Samia kawaumbua. sasa inaruhusiwa wawekezaji wengine kujenga bandari zingine bila ridhaa ya waarabu, na mwarabu kapewa kaeneo ka pale DSM port tu, sehemu zingine za bahari na maziwa hana mamlaka nazo, na ni miaka 30 na kila baada ya miaka 5 tutakuwa tunamtathimini. huoni mchango wa kina mwabukusi hapo? dini mmeileta wenyewe kwenye mjadala, na mnalalamika wenyewe tena.
 
kelele zenu zimezuwia nini?
Unafurahi mvaa kilemba mwenzako kuuza bandazi zetu au sio? Kwani hujui mikababa mingine ya kihuni ulaji tu kama iptl, richmond ilivyotuletea hasara? Hata huu utasababisha wizi tu ila tutakapousimamisha hatutawaacha waliyohusika salama. Watawajibishwa.
 
Tatizo siyo maneno mazuri ila maandishi mazuri ya hayo maneno
 
Hivi hawa wanavyosema ukutafukuzwa mtu inamaana watakaoshindwa kuendana na mfumo wa DP WORLD watabaki kama wafanyakazi hewa ????
 
 
Alafu mbona mods hizi nyuzi za dipii woordi wanazifuta tu,kunani??
 
Dharau zenu zitawaponza. Huwa mnaona wengine sio raia wa nchi hii. Tuone hiyo bandari itafika wapi.
Wapinga maendeleo nyie baada ya miaka 3 mtapata aibu Kwa maendeleo yatakayokuwa yamepigwa hapo bandarini, Kwa hiyo mlitaka serikali iache kufanya maendeleo sababu kusikiliza waoga kama nyie?
 
Na bado.

Wameshagusia mbarabara na reli zote leo.
FaizaFoxy, tulijenga barabara, na SGR ili kurahisisha uwekezaji wa watu wote, sio wa dp world tu, wao watafikisha mizigo yetu haraka bandarini, na tunawaruhusu watumie opportunity ya sgr. dp world kwetu ni wa muhimu zaidi kuliko wazungu ndio maana hata mapingamizi yote tuliyeleta, tulilenga vipengele vya mkataba, sio uarabu au vinginevyo. kwasaba, walivyobadilisha vipengele kutokana na maoni yetu, serikali ikamilishe haraka SGR, waboreshe barabara toka hapa hadi mpaka na zambia, mpaka na burundi, mpaka na Rwanda na mpaka na Uganda, kwasababu landlocked zote mizigo yao sasa itapitia hapa.

ila tunamshukuru Rais Samia, ni msikivu (speaking from the bottom of my heart), kile kipengele kuhusu bandari zingine kwamba tuwaambie kwanza wao, kimefyekwa, sasa mwekezaji mwingine anaweza kuja kujenga bandari maeneo mengine ili ashindane na dp world. safi sana.
 
Yule jamaa aliyetaka kulipa tra 400m wakazikataa kabadili upepo kabisa hakuna tena anaepinga ujio wa dpw
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…