Utiaji saini Mkataba wa Tanzania na DP World: Mkataba utakuwa wa miaka 30 na utendaji kazi wake utapimwa kila baada ya miaka 5 na sio miaka 100
MABORESHO YA MKATABA
Wamebadilisha vipengere vyote tata…

1. Mkataba maximum miaka 30

2. Watalipa kodi zote za Serikali kwa mujibu wa Sheria

3. Wamewekewa performance key indicators na watakuwa accessed kila baada ya miaka 5

4. Serikali itachukua 60% ya mapato ya faida

5. Serikali inauwezo wa kuvunja mkataba muda wowote

6. Mkataba huu sio wa gati zote za Bandari ya Dar es Salaam gati ambazo hazipo kwenye mkataba huu zinatafutiwa Mwekezaji mwingine (hata huyu wa sasa)
 
Za ndani ndani zinasema baada ya serikali kutaka kufanya uwekezaji bandari kwa ushirika na dp world ,kanisa katoliki lilitoa onyo kali juu ya vipengere kadhaa vya mkataba baada ya purukushani hiyo serikali iliamua kukaa meza moja na kanisa na habari za ndani zinasema baada ya ubishani kati ya Tec na serikali maridhiano yalifikiwa kwamba wanasheria wa kanisa na serikali washirikiane pamoja katika kurekebisha vipengere muhimu,,,baada ya hapo wakakubaliana sasa uwekezaji uendelee.
Unamaanisha tec au teketeke
 
Waraka uliosomwa kwa wiki sita, umezimwa kimya kimya....😂😂😂
 
MABORESHO YA MKATABA
Wamebadilisha vipengere vyote tata…

1. Mkataba maximum miaka 30

2. Watalipa kodi zote za Serikali kwa mujibu wa Sheria

3. Wamewekewa performance key indicators na watakuwa accessed kila baada ya miaka 5

4. Serikali itachukua 60% ya mapato ya faida

5. Serikali inauwezo wa kuvunja mkataba muda wowote

6. Mkataba huu sio wa gati zote za Bandari ya Dar es Salaam gati ambazo hazipo kwenye mkataba huu zinatafutiwa Mwekezaji mwingine (hata huyu wa sasa)
Roma locuta mnahangaika
 
Inaonekana hujui hata huo mkataba ulikuwa na vipengere gani!!! Kama ni kweli walichosema leo ndio huo mkataba ulivyo kuna mabadiriko makubwa sana!! (hao hawaaminiki) mwanzoni ilikuwa ni kuendesha bandari zote, ila sass ni dar tu, na sio kila sehemu, umri wa mkataba ulikuwa haujulikani lakini sasa ni miaka 30!!!ILA KAMA NI KWELI NDIO MKATABA ULIVYO.
Muda wa mkataba ulikua haujulikani!?..mbona ilikua dhahiri muda utatajwa kwenye hga!?..yaani IGA ilisema hawatolipa Kodi!?..acha uwongo
 
wasingepiga kelele ndio tungekuwa tumeingizwa mjini kirahisi tu
Acha ujinga,wao wafanye kazi yao ya kuwalisha sakrament,wasipende siasa,waamini maadilo hamna,dini mnaacha,wao kutwa na siasa hawaangalii wanawafikia vipi na kuwarudisha msitarini
 
Waraka wa TEC umepuuzwaje kwa mfano hapa? Hebu chungulia hapa
Acheni kujitutimua, hoja ya tec haikuwa marekebisho ya vipengere vya mkataba bali hoja yao ilikuwa ni mkataba ufutwe kabisa na bandari iendeshwe na wawekezaji wa ndani.

Hoja za kufanyia marekebisho vipengere ilikuwa ni ya kkt na bakwata msitake kudandia hoja za wengine ,ndo mjifunze kuacha kujipa umuhimu msio kuwa nao ndani ya nchi hii.
 
Gharama za mizigo zitapanda.

Mtakuja kurejea hii comment miezi au mwaka mmoja baada ya utekelezaji wa mkataba kuanza.
 
Sidhani kama tec wanaweza kupuuzwa kirahisi hivyo
Za ndani kabisa zinasema waraka wa TEC umepuuzwa. Haya TEC ifanye kama inajikuna tuone!!

Jamani tupambane kupata katiba mpya. Kwa katiba hii rais ana uwezo hata wa kuwafunga jela TEC wote na asifanywe kitu
 
Gharama za mizigo zitapanda.

Mtakuja kurejea hii comment miezi au mwaka mmoja baada ya utekelezaji wa mkataba kuanza.
zitapungua. kama wamerekebisha vipengele waacheni tuwape muda wa matazamio wafanye kazi.
 
Acha ujinga,wao wafanye kazi yao ya kuwalisha sakrament,wasipende siasa,waamini maadilo hamna,dini mnaacha,wao kutwa na siasa hawaangalii wanawafikia vipi na kuwarudisha msitarini
wewe ni nani hadi uwaamuru waache kuongea kwa niaba ya waumini wao? yaani kapuku huna lolote unatoa amri kana kwamba una mamlaka ya nchi hii?
 
Za ndani ndani zinasema baada ya serikali kutaka kufanya uwekezaji bandari kwa ushirika na dp world ,kanisa katoliki lilitoa onyo kali juu ya vipengere kadhaa vya mkataba baada ya purukushani hiyo serikali iliamua kukaa meza moja na kanisa na habari za ndani zinasema baada ya ubishani kati ya Tec na serikali maridhiano yalifikiwa kwamba wanasheria wa kanisa na serikali washirikiane pamoja katika kurekebisha vipengere muhimu,,,baada ya hapo wakakubaliana sasa uwekezaji uendelee.
Kipengele Cha Ajira kwa vijana pale bandarini kuanzia vibarua sijaona kikielezewa sijui kimerukwa,
 
wewe ni nani hadi uwaamuru waache kuongea kwa niaba ya waumini wao? yaani kapuku huna lolote unatoa amri kana kwamba una mamlaka ya nchi hii?
Serikali inahangaika na viwiliwili vya watu wake ambao ni wakatoliki na wengineo,kanisa likitaka lijisajili Kama taasisi ya siasa na maendeleo ya jamii na si dini
 
Habari zenu.

Napenda kumpa pongezi raisi wetu wa Tanzania MAMA SAMIHA SALUHU,Na viongozi wote waliohusika kwenye kupambana mkataba huo.

Kwanza mkataba ni wa miaka 30 sio mkataba wa miaka 100 kama tulivyokuwa tunadanganywa na watu wenye chuki ya maendeleo.

Pili mkataba unabadilika kila baada ya miaka 5,ambapo tunakaa chini na hao D.P WORLD na kudiscuss jinsi ya kuiboresha mkataba kila baada ya miaka 5. Na kama tukiona huo mkataba hautufaidishi tunaweza upiga chini na kuachana nao na hakuna atakuaye pata hasara maana ni kipengele kilichopo kwenye mkataba huo.

Tatu mkataba umeegemea kwetu kwa kiasi kikubwa,asilimia 60 mpaka 70.

. Faida tukazopata kwenye huo mkataba.
1.Uwepo wa ajira za kutosha.
2.Bandari itatengenezwa vyema
3.Pesa tutakazopata zitaenda kuleta maendeleo kwenye sekta mbalimbali,mashuleni,mahospitalini kila sekta itanufaika.

Kwa nchi zinazoendelea bandari ni kitu cha muhimu sana,wenzetu wa Kenya wameboresha bandari yao ya Mombasa vyema na imekua bandari kubwa Africa,na sasa wanajenga nyingine lamu,wanapokea meli kubwa za kila nchi na kuna mataifa wanatumia bandari hiyo kushusha mizigo yao,wametupiga bao sana.

Tumsupport raisi wote,maana anaupiga mwingi.
 
Za ndani ndani zinasema baada ya serikali kutaka kufanya uwekezaji bandari kwa ushirika na dp world ,kanisa katoliki lilitoa onyo kali juu ya vipengere kadhaa vya mkataba baada ya purukushani hiyo serikali iliamua kukaa meza moja na kanisa na habari za ndani zinasema baada ya ubishani kati ya Tec na serikali maridhiano yalifikiwa kwamba wanasheria wa kanisa na serikali washirikiane pamoja katika kurekebisha vipengere muhimu,,,baada ya hapo wakakubaliana sasa uwekezaji uendelee.
TEC walichemka tangu mwanzo kabisa. Mzee wa bapa alipotoa video zake za kupinga wanachofanya maaskofu alikuwa sahihi kabisa ila hakuweza kueleweka miongon mwa wakatoliki.

Kusema kwamba wanasheria wa kanisa wapo na ni tofauti na wa serikali ni kiburi ambacho vitabu vya dini vinakipinga siku zote.

TEC walitaka kutunishana misuli na serikali na mshindi amejulikana ni nani mpaka muda huu. Mengi ambayo tunayajua hivi sasa ni kwamba umefika muda wake wa kujulikana kwa sababu bungeni palipitishwa IGA na miradi ya kibiashara ilikwenda kuandaliwa kule Belgium baada ya kwanza IGA kupita bungeni.
 
Ulichoandika hapa
Za ndani ndani zinasema baada ya serikali kutaka kufanya uwekezaji bandari kwa ushirika na dp world ,kanisa katoliki lilitoa onyo kali juu ya vipengere kadhaa vya mkataba baada ya purukushani hiyo serikali iliamua kukaa meza moja na kanisa na habari za ndani zinasema baada ya ubishani kati ya Tec na serikali maridhiano yalifikiwa kwamba wanasheria wa kanisa na serikali washirikiane pamoja katika kurekebisha vipengere muhimu,,,baada ya hapo wakakubaliana sasa uwekezaji uendelee.
Ulichoandika hapa sio kweli. Kumbuka kilichosainiwa Leo ni HGA na sio IGA. IGA ilishasainiwa na sijasikia imebadilishwa.
 
Za ndani ndani zinasema baada ya serikali kutaka kufanya uwekezaji bandari kwa ushirika na dp world ,kanisa katoliki lilitoa onyo kali juu ya vipengere kadhaa vya mkataba baada ya purukushani hiyo serikali iliamua kukaa meza moja na kanisa na habari za ndani zinasema baada ya ubishani kati ya Tec na serikali maridhiano yalifikiwa kwamba wanasheria wa kanisa na serikali washirikiane pamoja katika kurekebisha vipengere muhimu,,,baada ya hapo wakakubaliana sasa uwekezaji uendelee.
ndo maana bibi ushungi alikuwa hakauki kanisani.

View attachment 2789715View attachment 2789716View attachment 2789717View attachment 2789718
Screenshot_20231022_224021_Instagram.jpg
 
Back
Top Bottom