Utiaji saini Mkataba wa Tanzania na DP World: Mkataba utakuwa wa miaka 30 na utendaji kazi wake utapimwa kila baada ya miaka 5 na sio miaka 100
Fuatilia yanayojiri kutoka Ikulu kwenye Halfa ya utiaji saini wa Mikataba mahsusi 3 ya uwekezaji Bandari ya Dar es salaam, leo Oktoba 22, 2023.


Kuongeza ufanisi kwa huduma za meli na shehena, kupunguza muda kwa bandari katika kuchakata nyaraka, kuongezeka kwa mapato ya serikali, kupungua kwa udanganyifu, kuimarisha nafasi ya ushindani kwa bandari, kuongeza ajira na kupunguza gharama za usafirishaji wa mizigo kuja bandari ya Dar es salaam.

Aidha, muda wa usafirishaji wa mizigo kutoka mashariki ya mbali utapungua kutoka siku 30 hadi 15.

Haitegemewi kufungwa kwa biashara zozote za wazawa zinazofanyika bandarini.

Wale ropo ropo waje wapayuke tena
 
Pamoja na kelele zote za watanganyika kuhusu bandari yao kuuziwa mwarabu, bado serikali inayoongozws na rais Samia imepuuza na kuwapa bandari warabu wa DP World.

IMG_20231022_115411_734.jpg


Leo mikataba 3 ya DP World inasainiwa rasmi.
 
Kwasababu ya ule walaka wa TEC ilinilazimu kuiunga mkono Serikali kwenye issue ya DP world... nchi haiwezi kutishwa na taasisi za kidini na kushindwa kufanya maamuzi yake.

Serikali ni mali ya watanzania wote, taasisi za dini zisijifanye na kujiona zina nguvu kuliko serikali.

Huu ujinga wa kuendekeza hizi taasisi uko sana huku Africa na hili lipo makusudi kulinda maslahi ya mataifa fulani na vikundi vya watu fulani kuendelea kucolonise nchi masikini.
l
Hizi taasisi nyingine ni tools za wakoloni zilizoachwa kuendelea kusimamia maslahi ya wakoloni na kuendeleza uhuni wa kikoloni
 
Fuatilia yanayojiri kutoka Ikulu kwenye Halfa ya utiaji saini wa Mikataba mahsusi 3 ya uwekezaji Bandari ya Dar es salaam, leo Oktoba 22, 2023.


Uwekezaji huu wa Serikali kupitia TPA utaongeza ufanisi kwa huduma za meli na shehena, kupunguza muda kwa bandari katika kuchakata nyaraka, kuongezeka kwa mapato ya serikali, kupungua kwa udanganyifu, kuimarisha nafasi ya ushindani kwa bandari, kuongeza ajira na kupunguza gharama za usafirishaji wa mizigo kuja bandari ya Dar es salaam.

Aidha, muda wa usafirishaji wa mizigo kutoka mashariki ya mbali utapungua kutoka siku 30 hadi 15.

Haitegemewi kufungwa kwa biashara zozote za wazawa zinazofanyika bandarini.

Kwani TEC wanasemaje?
 
Mkataba una miaka 30 na kila baada miaka 5.

Hizo porojo za kina Padri Slaa miaka 100 walipata wapi.

Hii nchi imejaa wajinga sana na chuki zisizo na maana.

Punguani yule mdude na wajinga wenzake povu linawatoka bure.
Hapa ndo nimepaelewa sana
 
Back
Top Bottom