Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
kwan mie nimesemajeMrisho kaongea ukweli au uongo?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kwan mie nimesemajeMrisho kaongea ukweli au uongo?
Wabongo bana. Unaulizwa swali, nawe unaniswalika. Swali kwa swali.kwan mie nimesemaje
At least they tried,Hakuna cha TEC wala Mwabukusi wote wazinguaji.
Kweli nimeamini wewe una magonjwa Mtambuka, hicho unachosema kupayuka ndiyo kilichopeleekea leo Mkataba usiwe wa mileleBasi sasa akina Mwabukusi waache kupayuka payuka😁
Sawa kabisa fukuzeni tu kanisa na St Joseph mjenge msikitiDP World kuwekeza pia kwenye miundo mbinu ya inayotegemeana na bandari kama reli na barabara.
Wawache yawepo na yaendelee kujengwa tu, yatakuwa misikiti kama kinachoendelea Ulaya sasa hivi.Sawa kabisa fukuzeni tu kanisa na St Joseph mjenge msikiti
Utakwenda kwenye maandamano ya Mwabukusi tarehe tisa novemba?😁Kweli nimeamini wewe una magonjwa Mtambuka, hicho unachosema kupayuka ndiyo kilichopeleekea leo Mkataba usiwe wa milele
Hicho kizungu chako cha ugoko hakinisumbui kitu. Ni ujinga tu na kutokujielewa😁😁😁
Bado tu na ugoko wako; hukomi, ha ha ha lini utaacha ujinga wako?😁😁😁President Samia Hassan's kleptocratic ambitions, if not stopped post-haste, will consign the futures of Tanzanian people to lives of slavish poverty at the hands of her Middle-Eastern accomplices, unimaginable penury, disease, death and disaster.
Kuna ubaya gani mkisema mmedundwa na kitu kizito?Za ndani ndani zinasema baada ya serikali kutaka kufanya uwekezaji bandari kwa ushirika na DP-World, kanisa katoliki lilitoa onyo kali juu ya vipengere kadhaa vya mkataba baada ya purukushani hiyo serikali iliamua kukaa meza moja na kanisa
Habari za ndani zinasema baada ya ubishani kati ya TEC na serikali maridhiano yalifikiwa kwamba wanasheria wa kanisa na serikali washirikiane pamoja katika kurekebisha vipengere muhimu, baada ya hapo wakakubaliana sasa uwekezaji uendelee.
Hukuusoma waraka wote na hitimisho lake.Kama hoja gani wakati wao walitaka DP World asiwepo kabisa Kwa maelezo kwamba tuendeleaa kujenga uwezo wa ndani?
Unajua kusoma bali hujajifunza kutafakali.Kuanzia leo mjijue na tec yenu kuwa ni irrelevant,kaeni mahalia penu pa kusamehe watch dhambi na kuwalisha sakrament
'tafakari'Unajua kusoma bali hujajifunza kutafakali.
Usibishe lengo kuu la DP world kujenga misikiti na kuvunja makanisa!!Wawache yawepo na yaendelee kujengwa tu, yatakuwa misikiti kama kinachoendelea Ulaya sasa hivi.
Kenya yashaanza kubadilishwa huko na kuwa misikiti. Mwenzako akinyolewa na wewe tia maji zako.
Hatuna wasiwasi nayo kabisa tena.
Hawa ndio Watanzania.Diamond anaingiaje kwenye maswala ya msingi ya kitaifa?
😃😃😃😃Duuuu kweli magonjwa ya Mtambuka ni noma, yani bado unaendelea Kutambuka tuUtakwenda kwenye maandamano ya Mwabukusi tarehe tisa novemba?😁
Unataka niache?😁...unaendelea Kutambuka tu
Fuatilia yanayojiri kutoka Ikulu kwenye Halfa ya utiaji saini wa Mikataba mahsusi 3 ya uwekezaji Bandari ya Dar es salaam, leo Oktoba 22, 2023.
View: https://www.youtube.com/live/N6izYMjIOaI?si=O_YQZdZcwAOJWWpD
MKURUGENZI MKUU WA TPA, PLASDUCE MKELI MBOSSA
Uwekezaji huu wa Serikali kupitia TPA utaongeza ufanisi kwa huduma za meli na shehena, kupunguza muda kwa bandari katika kuchakata nyaraka, kuongezeka kwa mapato ya serikali, kupungua kwa udanganyifu, kuimarisha nafasi ya ushindani kwa bandari, kuongeza ajira na kupunguza gharama za usafirishaji wa mizigo kuja bandari ya Dar es salaam.
Aidha, muda wa usafirishaji wa mizigo kutoka mashariki ya mbali utapungua kutoka siku 30 hadi 15.
Haitegemewi kufungwa kwa biashara zozote za wazawa zinazofanyika bandarini.
Aidha, Mkeli Mbossa amefafanua kuwa wastani wa meli kukaa nangani ikisubiri huduma ni siku 5 hadi 10 huku bandari ya Mombasa ni siku 1.25 na Bandari ya Durban ikiwa ni wastani wa siku 1.6. Hii inatokana na kukosekana kwa uwekezaji mkubwa wa muda mrefu ambao ungepelekea kuongezeka kwa namba za gati. Pia, gharama za kusafirisha makasha ni kubwa, jambo linalofanya kupanda kwa bei ya bidhaa kwa mtumiaji wa mwisho.
Mikataba inayosainiwa leo ni baina ya Nchi mwenyeji, mkataba wa ukodishaji na uendeshaji wa gati namba 4-7 lakini pia kutakuwa na sehemu ambayo gati 0-3 zitaendeshwa kwa ushirikiano wa pamoja kati ya TPA na kampuni ya DP World kwa shughuli za kibiashara na shughuli za kiserikali.
Mikataba hii haihusishi eneo lote la bandari wala bandari zingine za Tanzania. Upande wa gati namba 8-11, mchakato wa kumpata mwendeshaji mwingine umeshaanza kufanyika na akipatikana mwekezaji mwingine mwenye sifa atakabidhiwa na sio DP World.
Katika mikataba hii, Serikali itakuwa inapata ada na tozo kutoka DPW ambazo zitaongeza mapato na kupunguza gharama za uendeshaji.
Mkataba huu utakuwa wa miaka 30 na utendaji kazi wa DPW utakuwa unapimwa kila baada ya miaka 5 na sio miaka 100. Watumishi wa sasa wa TPA watakuwa na nafasi ya kuchagua kubaki TPA au kuhamia kampuni ya DPW.
Pia, mwekezaji atalipa kodi zote za Tanzania kwa mujibu wa Sheria za Tanzania, sheria za Tanzania ndio zitatumika katika kutekeleza mkataba huu na serikali itakuwa na haki ya kujiondoa kwenye mkataba ikiona inafaa.
SAMIA SULUHU HASSAN, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIARais Samia amesema haikuwa rahisi kufikia makubaliano haya lakini walisikiliza na kufuatilia maoni na hoja za kila mtu hivyo hakuna kundi au sauti ambayo imepuuzwa ambao Serikali iliunda jopo la wataalam kufuatilia maoni hayo.
Kwa ujumla na kipekee kabisa, Rais Samia ameshukuru watanzania wote waliotoa maoni kwani linapokuja jambo jipya ni lazima watu wawe na maoni tofauti.
Amewakaribisha watu wengi zaidi kuja kuwekeza Tanzania ili kuinua uchumi na kupunguza umaskini wa watu.
Mawazo ya wawekezaji wa ndani kupewa bandari ni mazuri na ya kizalendo lakini yapo mbali na uhalisia. Katika kusiani mkataba huu, maslahi mapana ya nchi yamezingatia maslahi mapana ya nchi.