Hivi wewe unayetoa huu ushauri kwa TL ulishawahi hata kujeruhiwa kwa kisu na vibaka ukatoroka? Unaelewa nini kuhusu risasi kupita mwilini? Unajua nini kuhusu kuwa katika coma kwa masaa 6?
Kama hujui jibu la moja wapo ya maswali hayo basi funga kopo lako kalale. Ushauri huo kawape CCM waliotumwa na shetani kuondoa uhai wa Mtanzania mwenzao bila chembe ya huruma.
Hujui Nguvu za Mungu zinavyofanya kazi katika kusamehe na kukaa kimya!
Hana Sababu ya kufanya siasa za uchochezi mana tayari ameshapata kibali toka kwa Mungu.
Aonyeshe wazi kuwa naye pia hamjui aliyemfanyoa kitendo kile cha kumpiga risasi.
Lakini pia aonyeshe kuwa hana Kinyongo na watesi wake na amemwachia Mungu ili Asili ya viumbe vyote ifanye Kazi yake.
Nani anayejua kuwa waliofanya vile walipata ushauri toka kwa nani?@
Jibu ni kwa wote hatujui isipokua Mwenyezi Mungu ndiye mjuzi wa yote. Kwa nini Lisu asimwachie Mungu yeye apambane na wale waliojiona kuwa wapo Juu ya Uhai wa binadamu?
Damu ya MTU haijawahi kumwacha Mtu salama.
Lakini Pia uungwana atakaoufanya Lisu kuanzia sasa utaepusha wengine pia kujeruhiwa au kuuawa.Tutambue kuwa wabaya zaidi ni wale wanaonufaika na Kumhujumu Lisu kwa namna yoyote.
Hata Mwenyekiti wake kuna wakati anawaza tofauti mana anaona kuwa watu hawakuguswa na tukio lake la kujikwaa kwenye ngazi na kuvunjika Mguu Bali wameendelea kumtizama Lisu Mwana halisi wa Kitanzania.
Tumwombee Lisu awe na Busara,hekima na maarifa ili wote waamue sasa kukaa pembeni na kumwachia jukwaa la kura za Urais 2025-2030 ambapo bila shaka yoyote Katiba mpaya na tume huru itakuwepo.
Kwa sasa ni Mungu Pekee ndiye anayeweza kuitoa Madarakani CCM lakini sio sanduku la Kura.
Viongozi wengi wa dini wamekaa kimya kuhusu uchaguzi huru na wa Haki isipokua Shekhe Mbonda ,Askofu Bagonza na Askafu Mwamakula.
Wasome wote wamejisalimisha CCM, taasisi zote kubwa zinacheza wimbo wa CCM nambari wani.
Na wapinzani wengi wamejisajili CCM ili wapate riziki yao ya kila siku. Hawakumbuki tena kuhusu Haki katika uchaguzi wala Uhuru wa kila MTU kumchagua anayemtaka.
Kanuni za Uchaguzi zilizokuwepo ni kanuni zinazopaswa kusimamiwa na MTU mchaMungu sana na anayeweka Mbele Maslahi ya Wapiga kura na sio yake binafsi.
Kwa bahati Mbaya sana Kanuni hizo zinasimamiwa na watu waliojawa na ubinafsi na Chuki kubwa dhidi ya vyama vya upinzani.
Ni kanuni zinazotegemea huruma za mtu badala ya sheria na katiba ya nchi. Ndio maana wao CCM walishajipa kubwa sana ya ushindi kabla ya uchaguzi kufanyika.
Ujio wa Lisu utumike kumshukuru Mungu kwa yote. Lakini pia asisahau kumshukuru Mungu kwa ajili ya Kumleta Mh. Rais aliyepo mana bila awamu hii kusimamia vizuri suala la Korona na kumkabidhi Mungu Muweza wa yote lao tungepata tabu sana. Kila kitu kingeyumba ikiwa na pamoja na siasa na uchumi.
Kenya walijifanya wao ni wajuaji lakini wamepata wakati mgumu sana kwenye ugonjwa wa Korona.
Lisu ajitahidi kwenda kwenye nyumba za ibada kuwashukuru wote waliomwonbea dua kimya kimya mana walikatazwa wasimuombee kwa wazi.
Chuki inaondolewa na Upendo.
Giza haliwezi kuondolewa na giza bali Nuru huondoa Giza .
Ni ushauri mzuri kabisa kuwa Kesho Lisu asiende Kuaga mwili wa Marehem akiwa ana msafara.
Aende akiwa na baadhi ya watu wachache hao wengine waende kivyao tu bila kuandamana au kufanya msafara mkuubwa utakaoamsha hisia za kisiasa.
Ikumbukwe kuwa kuna watu watataka kumtumia Lisu kama mtaji lakini mioyoni mwao hawamuombei Mema. Hawa hawamuonei huruma kamwe zaidi ya kuwaza umaarufu wao utakaowapa kura kwenye majimbo yao.
Kwa sasa na hali ya hewa na Afya yake ilivyokaa na vyuma vingi mwilini Lisu hapaswi kabisa kukaa Gerezani au hata kwenye mahabusu za Polisi.
Mtu mwenye akili timamu hawezi kumtia Lisu gerezani kwa hali yake ilivyokaa. Lakini ni lazima aepuke Shari inayotokana na uvunjifu wa amani na kutoa lugha mbaya au hata kumsingizia MTU juu ya tukio lake bila ushahidi wa kutosha zaidi ya dhana tu zisizo na ushahidi.
Hakika kama Lisu atasamehe na kufanya siasa kwa wema na amani halafu wakamkamata kwa Chuki tuu na woga tuu, Mungu muumba wa vyote na mjuzi wa yote na mwenyekutenda haki ataingilia kati na kutenda Miujiza yake
Kwa wale waliosoma vitabu vya historia za dini watakubaliana nami kuwa Nabii Musa hakumshinda Mfalme wa Misri kwa nguvu zake Bali kwa nguvu na miujiza ya Mungu Muumba wa vyote.