Uwanja wa Ndege Dar: Mapokezi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu - Julai 27, 2020
Mh tundu lisu dunia imeona ulichofanyiwa na ujio wako umewatia aibu watesi wako.

Mapokezi yako yawape heshima waliokuja kukulaki. Ili waiandike historia Yao ya mapenzi na amani kupitia wewe.

Tal the great
Mwache kidogo apunguze..anahitaji kuongea zaidi ili azidi kupata nafuu na afya ya kiroho

Jr[emoji769]
 
pia ashauriwe asitumie lugha kali za kupandisha hamasa za chuki, bali apambane na ccm kwa sera. Kuna sehemu nyingi sana za kuwazidi ccm, mfano huu rushwa ya juzi kwenye chaguzi zao, ajira, ugumu wa maisha wa wananchi, demokrasia nk. Ni vyema apange vizuri mashambulizi yake kisiasa,
Huu ni zaidi ya ushauri.

Tundu Lissu hana sababu tena ya kupoteza muda mwingi wa kuzungumzia hali iliyompata. Ni nani asiyelijua hilo?

Sasa hivi atumie muda wake mwingi kuwa kama mwalimu, afundishe wananchi kuelewa haki zao za msingi ili wasiruhusu tena haki hizo zichezewe.
Ana haki, na uwezo wa kuzungumzia ulazima wa utawala bora na umhimu wake katika maendeleo ya nchi yetu.

Chaguzi zetu, afundishe watu kujua umhimu wa kuchagua viongozi wao wanaowataka wao bila ya kura zao kuharibiwa. Watu wajitokeze kwa wingi kupiga kura, ili hata kutokuwepo kwa Tume Huru ya Uchaguzi, iwe vigumu kwa tume hiyo kubadili matokeo.

Mahusiano yetu kimataifa, sio jambo la anasa, ni jambo la muhimu sana. Hatuwezi kujitenga kwa sababu uchumi wetu unategemea mahusiano hayo.

Waliopo huko ndani ya CHADEMA, ni wajibu wenu kumpa ushauri Lissu, na hasa kama ndiye atakayekuwa mpeperusha bendera wenu.

Wananchi sasa hivi hawategemei kuona nyinyi ndio mkiwa wachokozi. Mliyotendewa liwe fundisho, lakini msitafute kuchokoza kama njia ya kulipa kisasi. Mtapoteza imani ya wananchi
 
Halima amefanya vyema, si vibaya chama kikatoa shukran rasmi kwa jeshi la polisi, hata kama ni kwa kinafiki. Pia nashauri sana Tundu Lisu ashauriwe kutokwenda kesho msibani. Kwangu bado Lisu ana hasira na lile shambulio, kwa vyovyote atataka kuionyesha serikali na hasa rais Magufuli kuwa amepona. Na mashabiki wake wanaweza kuonyesha furaha iliyopitiliza ambayo itaipa serekali kuchukua maamuzi hasi.

Kwakuwa wamemstahi leo, ni vyema angeachana na huo msiba, kuna nafasi kubwa ya kushindana na ccm. Na kama itawezekana kuanzia sasa Lisu pia ashauriwe asitumie lugha kali za kupandisha hamasa za chuki, bali apambane na ccm kwa sera. Kuna sehemu nyingi sana za kuwazidi ccm, mfano huu rushwa ya juzi kwenye chaguzi zao, ajira, ugumu wa maisha wa wananchi, demokrasia nk. Ni vyema apange vizuri mashambulizi yake kisiasa, kuliko kuonekana anambana na mtu binafsi, kwa ajili ya shambulizi binafsi.
Umeongea vyema sana,hapo kwenye matumizi ya lugha Kali ndo patamletea matatizo,sidhani kama watavumilia swala hilo.Ajifunze aina ya ukosoaji unaofanywa na Zitto.Lugha ngumu itamletea changamoto kubwa na mamlaka jambo ambalo halitakuwa na faida kwake.
 
Lisu asifikiri tumemuogopa, tunamlia "timing" tu
Nguruwe wa Lumumba mnateseka sana na Lissu
JamiiForums-1364449287~2.jpg
 
Hivi wewe unayetoa huu ushauri kwa TL ulishawahi hata kujeruhiwa kwa kisu na vibaka ukatoroka? Unaelewa nini kuhusu risasi kupita mwilini? Unajua nini kuhusu kuwa katika coma kwa masaa 6?

Kama hujui jibu la moja wapo ya maswali hayo basi funga kopo lako kalale. Ushauri huo kawape CCM waliotumwa na shetani kuondoa uhai wa Mtanzania mwenzao bila chembe ya huruma.
Hujui Nguvu za Mungu zinavyofanya kazi katika kusamehe na kukaa kimya!

Hana Sababu ya kufanya siasa za uchochezi mana tayari ameshapata kibali toka kwa Mungu.
Aonyeshe wazi kuwa naye pia hamjui aliyemfanyoa kitendo kile cha kumpiga risasi.
Lakini pia aonyeshe kuwa hana Kinyongo na watesi wake na amemwachia Mungu ili Asili ya viumbe vyote ifanye Kazi yake.
Nani anayejua kuwa waliofanya vile walipata ushauri toka kwa nani?@
Jibu ni kwa wote hatujui isipokua Mwenyezi Mungu ndiye mjuzi wa yote. Kwa nini Lisu asimwachie Mungu yeye apambane na wale waliojiona kuwa wapo Juu ya Uhai wa binadamu?
Damu ya MTU haijawahi kumwacha Mtu salama.

Lakini Pia uungwana atakaoufanya Lisu kuanzia sasa utaepusha wengine pia kujeruhiwa au kuuawa.Tutambue kuwa wabaya zaidi ni wale wanaonufaika na Kumhujumu Lisu kwa namna yoyote.
Hata Mwenyekiti wake kuna wakati anawaza tofauti mana anaona kuwa watu hawakuguswa na tukio lake la kujikwaa kwenye ngazi na kuvunjika Mguu Bali wameendelea kumtizama Lisu Mwana halisi wa Kitanzania.

Tumwombee Lisu awe na Busara,hekima na maarifa ili wote waamue sasa kukaa pembeni na kumwachia jukwaa la kura za Urais 2025-2030 ambapo bila shaka yoyote Katiba mpaya na tume huru itakuwepo.

Kwa sasa ni Mungu Pekee ndiye anayeweza kuitoa Madarakani CCM lakini sio sanduku la Kura.
Viongozi wengi wa dini wamekaa kimya kuhusu uchaguzi huru na wa Haki isipokua Shekhe Mbonda ,Askofu Bagonza na Askafu Mwamakula.

Wasome wote wamejisalimisha CCM, taasisi zote kubwa zinacheza wimbo wa CCM nambari wani.
Na wapinzani wengi wamejisajili CCM ili wapate riziki yao ya kila siku. Hawakumbuki tena kuhusu Haki katika uchaguzi wala Uhuru wa kila MTU kumchagua anayemtaka.

Kanuni za Uchaguzi zilizokuwepo ni kanuni zinazopaswa kusimamiwa na MTU mchaMungu sana na anayeweka Mbele Maslahi ya Wapiga kura na sio yake binafsi.
Kwa bahati Mbaya sana Kanuni hizo zinasimamiwa na watu waliojawa na ubinafsi na Chuki kubwa dhidi ya vyama vya upinzani.
Ni kanuni zinazotegemea huruma za mtu badala ya sheria na katiba ya nchi. Ndio maana wao CCM walishajipa kubwa sana ya ushindi kabla ya uchaguzi kufanyika.

Ujio wa Lisu utumike kumshukuru Mungu kwa yote. Lakini pia asisahau kumshukuru Mungu kwa ajili ya Kumleta Mh. Rais aliyepo mana bila awamu hii kusimamia vizuri suala la Korona na kumkabidhi Mungu Muweza wa yote lao tungepata tabu sana. Kila kitu kingeyumba ikiwa na pamoja na siasa na uchumi.
Kenya walijifanya wao ni wajuaji lakini wamepata wakati mgumu sana kwenye ugonjwa wa Korona.

Lisu ajitahidi kwenda kwenye nyumba za ibada kuwashukuru wote waliomwonbea dua kimya kimya mana walikatazwa wasimuombee kwa wazi.

Chuki inaondolewa na Upendo.
Giza haliwezi kuondolewa na giza bali Nuru huondoa Giza .

Ni ushauri mzuri kabisa kuwa Kesho Lisu asiende Kuaga mwili wa Marehem akiwa ana msafara.
Aende akiwa na baadhi ya watu wachache hao wengine waende kivyao tu bila kuandamana au kufanya msafara mkuubwa utakaoamsha hisia za kisiasa.

Ikumbukwe kuwa kuna watu watataka kumtumia Lisu kama mtaji lakini mioyoni mwao hawamuombei Mema. Hawa hawamuonei huruma kamwe zaidi ya kuwaza umaarufu wao utakaowapa kura kwenye majimbo yao.

Kwa sasa na hali ya hewa na Afya yake ilivyokaa na vyuma vingi mwilini Lisu hapaswi kabisa kukaa Gerezani au hata kwenye mahabusu za Polisi.
Mtu mwenye akili timamu hawezi kumtia Lisu gerezani kwa hali yake ilivyokaa. Lakini ni lazima aepuke Shari inayotokana na uvunjifu wa amani na kutoa lugha mbaya au hata kumsingizia MTU juu ya tukio lake bila ushahidi wa kutosha zaidi ya dhana tu zisizo na ushahidi.

Hakika kama Lisu atasamehe na kufanya siasa kwa wema na amani halafu wakamkamata kwa Chuki tuu na woga tuu, Mungu muumba wa vyote na mjuzi wa yote na mwenyekutenda haki ataingilia kati na kutenda Miujiza yake

Kwa wale waliosoma vitabu vya historia za dini watakubaliana nami kuwa Nabii Musa hakumshinda Mfalme wa Misri kwa nguvu zake Bali kwa nguvu na miujiza ya Mungu Muumba wa vyote.
 
Msiba ni wa waTZ wote bila kujali hitikadi za vyama vyao, hivyo ni haki yake kwenda kumuaga kiongozi wake wa kitaifa. Hasa ukizingatia kwamba hakuna uhakika bado kwamba Lissu ataweza kwenda kwenye mazishi. Muacheni akatoe heshima zake za mwisho kama raia wengine. Hata waziri mkuu amekaribisha kila mtu mwenye kuweza kutoka kila kona ya nchi aende akaage mwili.

"rushwa, ajira, ugumu wa maisha wa wananchi, demokrasia nk."
Ndio anayo simamia Lissu siku zote, na ni mambo ambayo hayatakiwi kuchekewa. Ni lazima yazungumzwe kwa ukali kwa sababu ndio misingi mikuu ya taifa.

"Ni vyema apange vizuri mashambulizi yake kisiasa, kuliko kuonekana anambana na mtu binafsi, kwa ajili ya shambulizi binafsi."
Hapa kwenye shambulizi binafsi sijakuelewa vizuri. Kwa sababu (a) Lissu wakati anashambuliwa alikuwa mbunge wa bunge la JMT. Na bunge ndilo linalotunga/pitisha sheria ambazo viongozi wanazitumia kuiongoza nchi. Kumshambulia mmoja kati ya wabunge kwa namna alivyoshambuliwa Lissu ndio umeligusa bunge zima na serikali kwa ujumla. (b) Shambulio lile kuna kila dalili kwamba halikuwa la uporaji. (c) Mpaka sasa hivi vyombo vyenye mamlaka havija toa taarifa ya tukio lile.
Haya ya CCM na serikali yake na viongozi wao kuwaonea CHADEMA wananchi wanayajua vyema sana.

Je, hii ndio iwe ajenda ya CHADEMA kwa wananchi - hapana, wanaweza kuwa wanakumbushia hapa na pale, sawa; lakini haiwezi kuwa ndilo jambo muhimu kwa CHADEMA.

Msisitizo wao unaweza kuwa na maana zaidi wakizungumzia 'Mifarakano" inayotokana na kubaguana kwa makundi kulikoonyeshwa ndani ya miaka hii mitano. Sio CHADEMA peke yao walioonekana kutengwa, pamoja na kwamba wao wamekuwa wahanga wakubwa zaidi katika hilo.

Kuna ajenda pana zaidi za kitaifa wanazotakiwa kuziwasilisha kwa wananchi. Watakuwa wameonyesha ukomavu mkubwa wakiweza kufanya hivyo, badala ya kubaki na ulalamishi juu ya maonevu waliyofanyiwa.

Ni muda wa kuanza kuzungumzia zaidi mipango yao wanayotarajia kuitimiza wakipewa ridhaa ya kuongoza nchi.
 
Leo Viongozi wa chadema wakiongozwa na Mbowe wameonesha usaliti kwa mara nyingine. Awali walijiweka kama wanajali wananchi ila leo wamekuwa tayari kuangamiza watanzania kisa Lissu.

Walijivika joho la WHO huku wakihubiri Sera za kubaki ndani maarufu kama Karantini kumbe ni unafiki mkubwa.
Tuwapime, tuwashangae, tuwakatae.

Si mkuu wa nchi alishatangaza kama imekwisha?
 
Kuondoka kwa mkapa!kumemfanya jpm apate baridi yabisi miguuni na ubongoni!!!!Sasa aliekua anampa Back up ya kutumia nguvu nyingi hayupo!!!waliobaki wastaafu sio sadist hawawezi kumshauri utopolo!!
 
Asanteni sana @tanpol !!! Tunawapenda SANA!! SISI ni watu wema!!! Tanzania ni YETU SOTE. Tusiruhusu maslahi ya WATU wachache watuvurugie UPENDO wa ASILI wa TAIFA LETU-Halima Mdee
Huyu jamaa mnafiki sana. Wakati huo huo muda huu a msiba wa Mkapa anapost tweeter watu walioenda kumpokea lissu MALOFA KTK UBORA WETU...if you read btn the line, unaoa kabisa she's nut...
 
Utasikia ni kisukari au shinikizo
Wamekufa wao kwa CORONA na wanaendelea kuambukizana. manina watajua tu kuwa hawajui. Wametumia pesa nyingi kulanghai umma kuwa CDM imekufa kumbe wamekufa wao kwa CORONA.
 
Leo Viongozi wa chadema wakiongozwa na Mbowe wameonesha usaliti kwa mara nyingine. Awali walijiweka kama wanajali wananchi ila leo wamekuwa tayari kuangamiza watanzania kisa Lissu.

Walijivika joho la WHO huku wakihubiri Sera za kubaki ndani maarufu kama Karantini kumbe ni unafiki mkubwa.
Tuwapime, tuwashangae, tuwakatae.
Kafie mbele huko.
 
Back
Top Bottom