Tuliombee sana taifa letu..
Tuwaombee sana Viongozi
Wengi hawalitakii mema hili taifa
Utajiri uliotamalaki kila kona unawatoa mate wengi..
Vyombo vyetu mahsusi viangaze jicho la 7 juu ya yote yanayoendelea..Nadhani ni zaidi ya yanayoendelea..
Wenye kiu ya madaraka makubwa ktk nchi japo hawana Sifa/uwezo,Dhima nyoofu,Uzalendo,Uadirifu stahiki,Maono,Hekima na busara lakini wanapambana sana kushika hatamu Kwa udi na uvumba..
.Nadhani tunahitaji siasa safi ..Kwa wakati sahihi na namna sahihi..Tunahitaji Siasa zenye uwezo wa kuitoa nchi kwenye Lindi la umaskini na udumavu wa kimaendeleo na sio mashindano ya kuiba,Ubadhirifu,Ufisadi..Mbali ya siasa safi tunahitaji wanasiasa wasafi na wenye uwezo (Nia,matamanio,Ufahamu,Uthubutu,Utendaji,Elimu,Exposure)..
Wahuni,Wezi,Mafisadi,Wezi,Wajasiliamali wa kisiasa,Warithi Uongozi..Na wote wanaodhani wana hati miriki ya uongozi wa taifa Wakae ama kuwekwa pembeni na mfumo wa kizalendo..