GE2025 Watibeli tunaiomba Serikali kumuachia Tundu Lissu Septemba kabla ya Septemba 7

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Nakupa Mfano mwingine;
Maana kichwa chako ni kizito na itakuwa faida kwa watu waliokuwa wanachanganya.

Serikali(Mahakama) ikikuhukumu Kwa kosa la Ubakaji kulingana na sheria zilizotungwa na Bunge. Moja kwa moja inasomeka kubwa ulifungwa na serikali ya Tanzania kupitia Mahakama zake
 
Lima mngese wewe kazi lawama tu
Una hasira sana. Tutaelewana kweli sasa kwa mwendo huu?

Halafu usiwapangie watu maisha,kama kulima ni muhimu wewe nenda kalime sisi tutakuwa busy na shughuli zingine.

Punguza matusi jenga hoja.
 
Maridhiano yamemponza,alimtembelea lissu hospital Nairobi,alikutana nae ughaibuni, akaleta maridhiano,lakini rejea kauli za kifedhuli za lissu dhidi ya maza.. yaani maza amuache humo korokoroni asitike mpaka 2031
Zile kauli ni hatari sana kwa umoja wa Taifa letu.
 
Acha washpaze shingo. Wanadhani kuna sauti zitatoka mbinguni ndiyo waamini.
 
Mwishoni umeamua kunifanya nicheke, niwashukuru wazazi wangu kwa kunipeleka shule na kua na uwezo wa kufikiria Nje ya BOX
 
Siku zake ziwe chache, mtu mwingine na achukue kazi yake. ZABURI 109:8.
Zile Novena leo siku ya ngapi mkuu aliyoagiza Askofu iswaliwe kwa ajili yake leo siku ya ngapi na zinaisha lini?
 
Mkuu mboni unataka nicheke? Yaan Serikali ni Mahakama? Serikali inahukumu au Mahakama inahukumu? Mkuu km masuala ya kisheria huyajui usiyaingilie kinyume
 
Mkuu mboni unataka nicheke? Yaan Serikali ni Mahakama? Serikali inahukumu au Mahakama inahukumu? Mkuu km masuala ya kisheria huyajui usiyaingilie kinyume

Serikali ndio inayo hukumu kupitia Mahakama. Kipi huelewi.
Ndio maana ambao hata hawajaisoma
Wanadharau hizo degree zenu za kukariri.

Hivi hata mtu ambaye hajasoma analielewa sasa msomi unashindwaje kuelewa dhana nyepesi kama hizi.

Umeambiwa serikali ni Moja yenye mihimili mitatu inayosaidia kuendesha nchi kiutawala. Hiyo Mihimili imepewa majukumu ya kimamlaka yanayolenga kurahisisha utawala. Yaani Mahakama, bunge na serikali kuu lengo ni moja.
 
Ndio maana inaitwa Mahakama ya Tanzania haiitwi Mahakama ya Serikali ya Tanzania maana yake ni Mahakama Huru ya Nchi ya Tanzania (Judiciary of Tanzania) unaposema Mahakama ya Serikali ya Tanzania ndio unamaanisha Serikali ni Mmiliki Halali wa Mahakama zote za Nchi ya Tanzania, huna tofauti na kusema ni Mahakama ya Chama na Serikali, jambo ambalo sio Kweli Mahakama sio za Chama na Serikali, Mahakama zote ni za Wananchi wa Nchi ya Tanzania, Serikali sio Mmiliki wa Mahakama zote ndani ya Nchi elewa hivyo Serikali ni Taasisi ndani ya Nchi Serikali haitoi Hukumu Mahamani maana katikati ya Mahakama na Serikali kuna Mstari mwembamba unaozitenganisha zisiingiliane ila zisaidiane kuhakikisha si tu haki ikitendeka bali haki ionekane ikitendeka

Soma


Inayotoa hukumu Mahakamani sio Serikali ila Mahakama ya Tanzania ndio inayotoa Hukumu na wewe pia una Haki ya Kuishitaki Serikali inapofanya fyongo na Haki yako na Serikali haiwezi kukuhumu wewe kwa kufanya hivyo ila Mahakama inaweza kuihukumu Serikali inapofanya fyongo na Hukumu ikapita wakiweza wakate rufaa, Serikali inawakilishwa na Mwanasheria wa Serikali (State Attorney) au Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Attorney General) au tuseme inawakilishwa Mahakamani na Principal State Attorney mbele ya Mahakama Serikali inaweza ikasimama km Mtuhumiwa au Mdaiwa pia na ikapigwa Marungu ya Kutosha mfululizo aidha ilipe fidia au faini au vinginevyo kuendana na Mahakama itakavyoamua iwe hivyo kwa hio Serikali haitoi Hukumu ila Hukumu inatolewa na Mahakama, usichanganye madesa kijana
 

Wewe ndio unachanganya madesa huelewi unazungumzia jambo gani.

Huelewi maana ya serikali, huelewi aina za serikali, huelewi Mihimilo ya serikali ni ipi na dhana nzima inayohusu hiyo mihimili. Alafu hiyo ni topic ya kidato cha kwanza Civics.

Hakuna mihimili mitatu ya nchi. Hicho ndicho tunajadili, naona unakimbia hoja yako kwa sababu unajua umepuyanga.
 
Kwa Tanzania, hakuna mamlaka iliyo huru, zote zipo chini ya Rais.
 
Kwa Tanzania, hakuna mamlaka iliyo huru, zote zipo chini ya Rais.
Nchi ya Tanzania ni ya Wanachi wa Nchi ya Tanzania, Rais sio Mmiliki wa Nchi, Rais yupo Ndani ya Taasisi ya Serikali ambayo inafahamika km Taasisi ya Urais ambapo pia Serikali ni Taasisi ya Nchi, Nchi sio Taasisi ya Serikali ila Serikali ipo Ndani ya Nchi na Nchi ni mali ya Wananchi sio Mali ya Taasisi ya Urais au Taasisi ya Serikali, unanielewa vizuri hapo?
 
Kwa hio unataka kusema Serikali ndio hua inatoa zile Hukumu Mahakamani? Twaaafa

Serikali ipi kwa mfano maana Mahakama ni Huru haiingiliwi na Serikali kwenye maamuzi, haya niambie ni Serikali ipi inayotoa Hukumu Mahakamani?

Maana mimi najua Mahakama inasimama km Mahakama na Serikali inasimama km Serikali, haya sema wewee mwelevu Mahakama ipi ambayo Hukumu zake zinatolewa na Serikali na sio Mahakama yenyewe?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…